Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wakati huu Leo tarehe 27/11/2024 ninapoandika hapa, tayari CHADEMA wametoka taarifa za kuuawa kwa wanachama wao wawili.
CHADEMA wameripoti kuwa kwenye Kata ya Mkwese, Jimbo la Manyoni aliyekuwa mgombea wao kwenye kitongoji kinachoitwa "Stendi" amepigwa risasi na kufariki.
Lakini pia CHADEMA wameripoti kuwa mwanachama wake anayejulikana Kwa jina la Stephen Chalamila ameshambuliwa usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake huko Tunduma, na kufariki Dunia.
Zipo habari pia za kuvamiwa Kwa mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Gairo Bw. Ernest Mkami kushambuliwa na watu wanaohisiwa kuwa ni Wana CCM.
Inatafakarisha Sana kuona viongozi na wanachama wa CHADEMA imekuwa ni kawaida hasa nyakati za chaguzi, kufanyiwa mashambulizi.
Hali hii inaashiria nini?