Kuukosa umakamu mwenyekiti Chadema taifa maana yake ni kukosa fursa, sifa na kipaumbele cha nafasi ya kugombea urais kupitia Chadema 2025

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Je, Tundu Antipas Lisu atavumilia kubaki mtiifu na mvumilivu kuishi katika upweke wa kutokua na nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chadema tunapoelekea uchaguzi mkuu Oct. 2025?

Au atavuka boda na kujiunga na chama kingine cha siasa kujaribu azma na ndoto yake ya kujaribu kugombea urasi tena Oct.2025?

Kama mdau wa siasa za Tanzania, unapendekeza na kumshauri huyu muungwana aelekee chama gani cha siasa, ili kuendeleza azma na ndoto yake ya kutaka kujaribu kugombea urasi tena uchaguzi wa 2025?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Je,
Tundu Antipas Lisu atavumilia kubaki mtiifu na mvumilivu kuishi katika upweke wa kutokua na nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chadema tunapoelekea uchaguzi mkuu Oct. 2025?

Lissu akikosa nafasi ya Mwenyekiti anakwenda kupotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za Tanganyika.
 
Lowasa alikuwa makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA mwaka 2015?
Gentleman,
kwamba unamfananisha hayati Lowasa na Lisu dah!

unawafananisha kwa mdomo na makelele au?

yaani mjumbe wa kamati kuu ambae pia ni mjumbe wa mkutano mkuu taifa, unamfananisha na Lisu asie na nafasi yoyote chadema mpaka kufikia Oct 2025, kweli?🤣
 
Lissu akikosa nafasi ya Mwenyekiti anakwenda kupotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za Tanganyika.
na hata ukikaa kwa kutulia, ukipima vizuri,
kuna mtu wa kumshinda mbowe kweli pale gentleman?🐒
 
Gentleman,
kwamba unamfananisha hayati Lowasa na Lisu dah!

unawafananisha kwa mdomo na makelele au?

yaani mjumbe wa kamati kuu ambae pia ni mjumbe wa mkutano mkuu taifa, unamfananisha na Lisu asie na nafasi yoyote chadema mpaka kufikia Oct 2025, kweli?🤣
We mzee pakachatupu hebu jibu swali maana hoja yako imesawiri vigezo vya kugombea Urais 2025.

Lowasa alikuwa na cheo gani wakati anagombea kupitia CHADEMA?
 
Hizi nyuzi za CHADEMA zinamiminika kwa kasi ya ajabu sana...yaani mama hana lake hatusikii tena mama mama mama🐼
 
Urais kwa maoni yangu si lazima mgombea awe kiongozi wa chama,lakini kwasiasa zetu hasa za Tz,wanakuwa viongozi kwasababu tayari anakuwa anajulikana tofauti na kuja na mtu ambaye inawezekana ni competent lakini siyo maarufu
 
Mwanachama yeyote anaweza ugombea urais siyo lazima awe kiongozi.
Gentleman,
mgombea udiwani, ubunge na urais, Lazima udhaminiwe na chama cha siasa. Hiyo ni kwa mujibu wa katiba.

sasa kwa akili ya kawaida tu,
yaani waachwe kupewa vipaumbele wanachama ambao ni viongozi ndani ya chama hicho, halafu eti upewe wewe usie na nafasi yoyote ya uongozi?

huo muujiza ulitokea wapi labda gentleman kwa faida ya wadau?🐒
 
We mzee pakachatupu hebu jibu swali maana hoja yako imesawiri vigezo vya kugombea Urais 2025.

Lowasa alikuwa na cheo gani wakati anagombea kupitia CHADEMA?
alikua mjumbe wa kamati kuu 🐒
 
Urais kwa maoni yangu si lazima mgombea awe kiongozi wa chama,lakini kwasiasa zetu hasa za Tz,wanakuwa viongozi kwasababu tayari anakuwa anajulikana tofauti na kuja na mtu ambaye inawezekana ni competent lakini siyo maarufu
nafurahi umeeleza vyema, na kukiri bayana, kwamba kwa mila utamaduni na desturi kwenye chaguzi nyingi Africa na Tanzania kwa ujumla,

vipaumbele vya kugombea uongozi hupewa zaidi viongozi waandamizi wa chama kuliko mwanachama asie na nafasi yoyote japo ni mwanachama wa chama husika 🐒
 
Je,
Tundu Antipas Lisu atavumilia kubaki mtiifu na mvumilivu kuishi katika upweke wa kutokua na nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chadema tunapoelekea uchaguzi mkuu Oct. 2025?

Au atavuka boda na kujiunga na chama kingine cha siasa kujaribu azma na ndoto yake ya kujaribu kugombea urasi tena Oct.2025?

Kama mdau wa siasa za Tanzania, unapendekeza na kumshauri huyu muungwana aelekee chama gani cha siasa, ili kuendeleza azma na ndoto yake ya kutaka kujaribu kugombea urasi tena uchaguzi wa 2025?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Lissu anawanyoosha vizuri sana mpaka hamlali
 
Hizi nyuzi za CHADEMA zinamiminika kwa kasi ya ajabu sana...yaani mama hana lake hatusikii tena mama mama mama🐼
Gentleman,
wale walio na kazi na majukumu ya kitaifa na kimataifa kwa maslahi mapana ya waTanzania wote, ni muhimu sana wakaongeza bidii na weledi katika kazi ya kuwatumikia waTanzania,

na hawa ambao wanapambana na chaguzi zao za ndani kitaifa, wakapewa nafasi na fursa ya kufanya hivyo kwa amani bila makasiriko, huku wachambuzi wabobevu na wataalamu wa siasa za vyama wakaendelea kuwahabarisha na kuwelewesha wadau mambo mbalimbali juu ya uchaguzi huo.

kwani kuna ubaya wowote gentleman?🐒
 
Lissu akikosa nafasi ya Mwenyekiti anakwenda kupotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za Tanganyik

Lissu akikosa nafasi ya Mwenyekiti anakwenda kupotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za Tanganyika.
Ndiyo anaweza potea kwenye siasa lakini kumbuka kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza, kwa uwezo wa Lissu popote atakapokuwa lazima tu atashang'ara tu. Na chadema wakimfukuza au wasipompa nafasi yeyote watashangazwa sana kwa kumpoteza mtu resources full kama huyo, yaani itakuwa ni kama wanataka chama kiongozwe na watu wakawaida sana. Na mi nilichokiona nadhani Mh Lissu ameona mdudu mengi ya siri na sasa anashindwa kuvumilia hizo sarakasi
 
Back
Top Bottom