Kuuliza Multiple Choice Question katika University Exams: Tunapima nini?

Kuuliza Multiple Choice Question katika University Exams: Tunapima nini?

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Wadau, salaam!

Nimekutana na karatasi ya Maswali ya Mtihani uliopita mwaka wa 3 (Final Year) pale UDSM una maswali ya multiple choice kama 20 hivi na kila swali lina marks 1, hivyo mtu akipata maswali yote hata kwa ku-guess tu ana marks 20 tayari kati ya 60 anazotakiwa kupata katika University Exam (UE). Swali langu ni kwamba, wa level ya Chuo Kikuu (University) tena Mwaka wa 3 anayepewa multiple choice kweli tunaanda wataalamu wa aina gani?

Rai Yangu:
Ningeshauri vyuo vikuu vibadili mtindo huu wa kutunga maswali (Multiple Choice) maana unavutia (encourage) kubahatisha (guessing) bila kufikirisha akili ya mwanafunzi.

Najua hapa watakuja watu kuutetea, ooh idadi ya wanafunzi wamekuwa wengi ndo maana lecturers wanatunga multiple choice questions ili iwe rahisi kusahihisha lakini sababu hiyo tu haitoshi kuharibu wanachuo hawa ambao baada ya kumaliza hapo, wanaenda kupambana na wasomi wa Kenya, Uganda, Afrika Kusini & dunia nzima
 
MCQ yanahitaji uweze fikikiria sana na ina discourage kukariri

tofauti na short answers au essay qns ambazo wanafunzi wana shusha notes kama zilivo kwenye handout

mcq
match item
short answer
essay qns
bado ni format nzuri tu kwa elimu yetu
 
Multiple choice inapima usahihi wa uelewa wa mtu.

Kwa hiyo si jambo la ajabu kabisa maswali ya mitihani ya chuo kikuu kuwa ya multiple choice.

Kuna nchi ambazo vyuo vyake vikuu maswali mengi ya mitihani huwa ni ya mtindo huo.
 
Mutiple Choice katika level ya University ni level ya chini wa kumtest mwanafunzi jamani je lecturers wanashindwa kutunga maswali ya Essay etc na si MCQ?
 
inaonesha wengi hatujui haswa dhima ya assessment, hakuna ubaya wa multiple choices questions!
 
Ndugu kidole007 unasema Multiple Choice Question inadiscourage kukariri??? unaelewa unachoongea kweli? hebu fikiria tena ndo uandike upya.

sasa unataka nikubaliane na wewe kinguvu bila facts

next time ukipinga hoja una weka hoja mbadala

MCQ ni sahihi kwa elimu ya chuo

una sema eti watu wana guess reallly??

Out of 5 choices kwa kila swali out of 50 uta guess ngap??
 
Kama ni hivyo basi elimu ya vyuo vikuu vya Marekani ni mbovu kabisa!!!!!!!!!!!!!!!

mkuu Nyaningabu
salaaam
ni kweli usemayo watu hawaelewi aina za maswali na malengo yake.... hawajui objectives zinapimwa vipi hivyo ni vigumu mtu kutambua umuhimu wa aina mbalimbali za maswali. objective questions like multiple choice items zanachukua sehemu kubwa ya upimaji wa content kwa urefu.
 
Last edited by a moderator:
Kwel wote ni vilaza . Multiple choice ukitungiwa hapa udsm ni bora essay kuliko hivyo wewe! Kati ya 15 unapata mbili au tano juzi kat kuna paper la history kuna had 0 . Wewe nahisi haujui
 
MCQ siyo kitu kibaya kwenye assessment ya mwanafunzi na kwa mwalimu anayejua jinsi ya kutunga siyo mtihani rahisi hata kidogow
 
Mutiple Choice katika level ya University ni level ya chini wa kumtest mwanafunzi jamani je lecturers wanashindwa kutunga maswali ya Essay etc na si MCQ?

FYI essay ndio zinafanya watu wa kariri
unakuta swali write an essay concerning sexually transmitted disease

hapo wanafunzi watashusha essay kama ya kwenye hand out

mcq are always tricky acha ku force tukubaliane na wewe
 
Mutiple Choice katika level ya University ni level ya chini wa kumtest mwanafunzi jamani je lecturers wanashindwa kutunga maswali ya Essay etc na si MCQ?

It is next to impossible mtu ku-guess na akayapata maswali yote 20! MCQ yanatumika worldwide, Inategemea ni somo gani. Umeshawahi kuona maswali ya GRE au GMAT?
 
Wewe labda chuo kingine udsm haupat yote ukipata yote .mie najiuzulu kuwa jamii fr. Fact ni kwamba inategemea na type ya lecture na chuo gan ? Sio kama maswal ya sekondar chuo majibu yote ya kwel lakn la kweli zaid linakuwa lip
 
watu ni vigeugeu sana.Juzijuzi nyie wenyewe mlikua mnamlaumu na kumponda mama Ndalichako na NECTA kwamba kwa nini anawapa wanafunzi maswali ya MULTIPLE CHOICE leo kwa kua pepa ya aina hiyo wamepewa UDSM mnatetea! Tena sababu za kutetea ni zilezile walizokuwa wakitoa Necta. Ha huu unafki huu!
 
watu ni vigeugeu sana.Juzijuzi nyie wenyewe mlikua mnamlaumu na kumponda mama Ndalichako na NECTA kwamba kwa nini anawapa wanafunzi maswali ya MULTIPLE CHOICE leo kwa kua pepa ya aina hiyo wamepewa UDSM mnatetea! Tena sababu za kutetea ni zilezile walizokuwa wakitoa Necta. Ha huu unafki huu!

Nani alimponda huyo mama?
 
blessings

we tatizo lako nini?
kuna aina mbili za maswali.
1. Subjective: hii inaangalia uwezo wako wa kupapanua mambo na maswali yake sio ya kuchagua.
2. Objective questions. haya ni maswali yanapima uelewa wako kwenye core objective ya somo haya huja kwa njia ya kuchagua. kumatch na kupangilia

Mitihani mingi ya kimataifa hua ya mtindo huu kwa tuliopiga CISCO. Oracle wanajua.

Kikubwa we soma uelewe na umeze sio unataka maswali yako ya kuongeza chumvi za uongo tehe tehe (Smart student doesn't ask type of question)
 
Last edited by a moderator:
Hamna paper nilizokuwa naziogopa na kuzipenda kama za multiple choice. Huwa hakuna usanii na longolongo kwenye majibu yake, tofauti na mitihani ya kujieleza. Unaweza ukapata maswali yote au kukosa.
 
Back
Top Bottom