Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Utangulizi: Kwa wanaonifahamu hapa JF, wanafahamu kuwa siasa zangu ni za mkondo wa kulia zenye kuhimiza maendeleo ya watu binafsi na wakati huohuo kulinda maslahi ya wanyonge (ubebari mwema A.K.A compassionate capitalism). Kwa mtaji huu sijawahi kuunga mkono chama chochote cha kisiasa. Na kinadharia nisingeweza kuunga mkono mgombea kutoka CCM.
Lakini kutokana na kufanana kwa ahadi wanazotoa wanasiasa kutoka vyama vyote vya siasa wenye nia ya kuwa rais, nimehamua kuunga mkono nia za Makongoro Nyerere (AKA Mako). Sababu za kufanya hivi nimeziweka kwenye makundi matatu. Kundi la kwanza, iwapo CCM itashinda. Kundi la pili, iwapo upinzani utashinda. Kundi la tatu, iwapo itaundwa serikali ya mseto.
Tuanze na kundi la kwanza: Hata kama wewe ni mpinzani ni lazima uamini kuwa CCM wanayo asilimia fulani ya kushinda uchaguzi. Je CCM ikishinda, ni nani ungependelea awe rais? Kumbuka rais mtarajiwa atakaa madarakani kwa miaka mitano au kumi ijayo. Je unapendelea maumivu yaendelee?
Mako hana uzoefu mkubwa lakini huo ni mtaji na sio upungufu. Kwani hata wasafi walio upinzani hawana uzoefu wa uwaziri, urais au madaraka yoyote makubwa ya kiserikali.
CCM ni mali ya watanzania. Kwa wale wenye upeo mdogo wa historia, wakati wa mfumo wa chama kimoja, watanzania walilazimishwa kukijenga hiki chama. Wakulima, wafanyakazi, na wafanyabiashara walikatwa mapato yao bila kupenda kujenga hiki chama. Dr. Slaa, Mkandara, Lipumba, Seif Ahmed, Warioba, Mzee Mwanakijiji, Mzee Mtei, Kichuguu walichangia hiki chama. Hivyo wakati umefika kukirudisha chama kwa wananchi. Japokuwa wengine tumejitoa kwa matakwa yetu, waliobaki wasikilizwe.
Katika tangazo lake la nia ya kugombea, Makongoro ameonyesha kuwa anafahamu asili ya chama. CCM ni chama cha wananchi na sio wagombea nafasi za uongozi. Ninaamini akipewa nafasi ya kugombea atawakilisha wananchi na sio matakwa yake binafsi.
Kundi la pili, iwapo upinzani utashinda: Upinzani ukishinda, sio mwisho wa CCM. CCM itabidi ijisafishe na kuwa mpinzani wa kweli. Kiongozi wa kuijenga CCM upya ni lazima atoke nje ya kundi lolote la mafisadi na awe tayari kukijenga upya chama. Makongoro anao uwezo huo kwa sababu yupo tayari kusema ukweli. Sio mwoga. Kweli hotuba yake alisema maneno bila kuzunguka mbuyu.
Kundi la tatu, iwapo itaundwa serikali ya mseto: Kwa historia za serikali za kiAfrika uwezekano huu ni mkubwa sana. Uchaguzi unaweza kuja na matatizo ambayo yakalazimisha uundaji wa serikali ya mseto. Wewe kama mpinzani, je ungemtaka nani kutoka CCM awe mwakilishi katika meza ya kuunda serikali ya mseto? Kama viongozi wa sasa wa CCM wanaleta matatizo ndani ya chama chao kwa ubinafsi, hawatasahu ubinafsi wao ndani ya serikali ya mseto. Kwa mtaji huu ni Mako mwenye sifa za kuwakilisha CCM kwenye serikali ya mseto kwa sababu anazosifa sawa na viongozi wa upinzani. Yeye ni outsider katika shughuli za kiutawala.
Wenu Z10.
cc: Mkandara, Jasusi, Mchambuzi, Nguruvi3, Kichuguu, alinda, gfsonwin, Jokakuu, Barubaru, Mag3, etc