Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
- Thread starter
- #21
Hata kama kuna mtu ana nafuu ndani ya CCM bado atazungukwa na uchafu tu na mwishowe naye atachafuka.
Mimi hata ikitokea CCM ikachaguliwa (ingawa siamini kama uchaguzi ukiwa wa huru na haki wanaweza kuchaguliwa hususan kwenye urais) bado nitawapinga tu.
Hilo lichama ndo limetufikisha hapa tulipo leo. Kuendelea kuliunga mkono kisa tu waliyemchagua hana kashfa za ufisadi na/ au keshawahi kutoa kauli za kukemea ufisadi kwangu hiyo haitoshi kwa sababu ni sawa tu na mazingaombwe.
Inavyoelekea ma grand pooh-bah wa CCM washawasoma vizuri wananchi na kubaini kwamba wanazugika kirahisi mno na mazingaombwe na hivyo safari hii watawaletea mtu ambaye yuko 'palatable' kuliko wengine na watu mtaingia kingi kirahisi sana.
Na mwishowe mifisadi papa na nyangumi haitafanywa lolote, sana sana itabadili tu mbinu za kifisadi na ufisadi utaendelea kushamiri huku maendeleo yakizi kudumaa.
Mimi kamwe sitaipigia kura CCM hata kama kwenye upande wa upinzani hakueleweki. Ni heri hata nisipige kura kabisa kuliko kuipigia kura CCM.
Ngabu:
Ingawa hawana nia ya kujenga nchi, CCM ina watu wenye uvumilivu wa kisiasa. Ndani ya CCM kuna watu wanakubali kukaa kimya au kubeba lawama kwa ajili ya chama. Hii sifa ndio inayotofautisha CCM na vyama vingine vya kisiasa nchini Tanzania. Watu wanaharibu mambo na wakipata kashfa wanakaa kimya kwa muda fulani na baadaye kurudi tena.
Changamoto kwa Makongoro kama hatapata nafasi ni kukikisha kuwa hawafufuki kisiasa.