Kuunganisha DR Congo na Tanzania

Kuunganisha DR Congo na Tanzania

Panatakiwa pawe na meli za mizigo na za mafuta huko ziwa Tanganyika.

Pawe na bandari nzuri Tanzania ya Karema. Na bandari ya Kalemie Drc. Pia pawe na Barabara au reli toka Kalemie Drc mpaka Lubumbashi. Au pawe bandari ndogondogo drc labda Mutindi, Kafifi, Basenga, zongwe na n.k
 
Okay wacha nikueleweshe plan ya america walitoa hela kutengeneza lami ya tdm sumbawanga then kasanga! Huko kote tumejenga imebaki km chache matai to kasanga port, pale ilitakiwa iwe ferries za maana kuvuka ziwa halafu upande wa Kongo nao wapige lami mpaka Lubumbashi!
Sasa kilichotokea upande wetu tumefanya vizuri mno cause tumebaki na kama km 30/40 tuu sasa ba Kongo aisee walikula hela hawajafanya lolote! Kwao ilitakiwa watengeneze km kama 500 hivi sasa jamaa hata km Moja hawajatengeneza!
Daraja across Lake Tanganyika lingekuwa zawadi nzuri kwa Africa kuliko reli ya Tazara.
Lingeunganisha bahari mbili za Hindi na Atlantic. Pia lingeikata Africa katikati.

Niliona mahojiano kati ya Fareed Zakaria na meya wa mwisho wa kiingereza wa Hong Kong. Alisema hiyo ndiyo zawadi kubwa ambayo China ingetoa kwa Africa.
 
Serikali ya nchu hii ni kichwa cha mwendawazimu bro..Mimi na elimu yangu ya pangu pakavu kichwani nina plan kibao ambazo kutokana na Rasilimali zilizopo nchi hii zinaweza kurahisisha suala la usfirishaji wa mizigo kiurahisi kwenda Congo..lakini huwezi kuta wanauchumi wanajadili hiki kitu pamoja na kwamba Congo drc ni mdau mkubwa sana katika kuimarisha uchumi wa nchi hii
DRC yenyewe iko hoi kiuchumi unategemea nini ?
 
Acha porojo zisizo na msingi,jiografia ipi hiyo itakayofanya mizigo ya kwenda Lubumbashi ipite Sumbawanga?

Huu uzushi sijui nani aliwadanganyaga.
Karema mkuu Kuna bandari moja kubwa Sana but haijaanza kufanya kazi kwaiyo jiografia inarhusu vizuri Sana
 
Kote huko ni mwenyeji,unazijua bandari kubwa Sana wewe kweli?

Haya kuna bandari hakuna barabara na upande wa pili hakuna bandari Ndio inakusaidia nini?

Ziwa pia halina meli inayofanya Kazi Sasa hapo ndio inasaidia nini?

Imarisheni usalama DRC na toeni pesa wajengee bandari,barabara nk mtalipana mbele ya safari,ndivyo hata Uganda Wamefanya..

Mwisho Serikali iwashawishi Zambia wajenge barabara ya kutoka mpulungu na kutoka Kasesya Ili kuunga hadi Kasama ndio zitafanya Mkoa wa Rukwa upate biashara za maana lakini kujenga upande wetu wakati wao hawana interest haisaidii kitu inakuwa tembo mweupe.
 
Ni vijiji vya wapi nimetaja? Muunganiko wa Karema na Kelemie unaujue vizuri?

Unajua potential ya hayo maeneo kama yakitukiwa effectively according to geographical Locations?
Narudia kukuambia kwamba Karema na Kalemie vyote ni Vijiji havina biashara yeyote ya maana..

Eti potential,hizo ni potential za mdomoni mwenu maana kungekuwa na potential kama unavyosema hiyo Kalemie yako ingekuwa Mji mkubwa kama ilivyo Uvira,Butembo na Goma..

Mwisho sio tuu ni Vijiji bali hakuna hata Barabara ya Kutoka Kalemie kwenda sehemu yeyote ya maana huko Msituni na mbaya zaidi huo upande wa DRC Usalama ni zero,sasa biashara zipi zitafanyika na meli kwenye Ziwa hakuna?
 
Naomba kujua hii serikali ya sasa inaendeleaje na mkakati wa kuunganisha DR Congo na Tanzania Ili mizigo ya DR Congo isipitie Zambia bali ipitie Tanzania na kufika DR Congo kupitia Sumbawanga

Hili ni wazo zuri, iwapo kwa upande wa pili hao umejipanga kimiundombinu kusafirisha mizigo mikubwa.
 
DRC yenyewe iko hoi kiuchumi unategemea nini ?
Haipo hoi kiuchumi kivile kama unavyotaka kuipimia tumewaacha kidogo tu hata ukiangalia GDP yao ni almost $53 Billion sisi tukiwa na $62 Billion..DRC isingekuwa na Warlords kila kona ya nchi ingekuwa bonge la nchi Africa hii kama wangetumia rasilimali za vizuri,suala la kuunganisha TZ na DRC lipo ndani ya uwezo wetu ikizingatia pia sisi ndio tunawahitaji sana DRC kuliko wao wanavyotuhitaj sisi maana wana option kibao
 
Kote huko ni mwenyeji,unazijua bandari kubwa Sana wewe kweli?

Haya kuna bandari hakuna barabara na upande wa pili hakuna bandari Ndio inakusaidia nini?

Ziwa pia halina meli inayofanya Kazi Sasa hapo ndio inasaidia nini?

Imarisheni usalama DRC na toeni pesa wajengee bandari,barabara nk mtalipana mbele ya safari,ndivyo hata Uganda Wamefanya..

Mwisho Serikali iwashawishi Zambia wajenge barabara ya kutoka mpulungu na kutoka Kasesya Ili kuunga hadi Kasama ndio zitafanya Mkoa wa Rukwa upate biashara za maana lakini kujenga upande wetu wakati wao hawana interest haisaidii kitu inakuwa tembo mweupe.
Ujenzi wa barabara kutoka Matai kwenda Kasesya tayari imeanza,
Kaz kwao Zambia.
 
Naomba kujua hii serikali ya sasa inaendeleaje na mkakati wa kuunganisha DR Congo na Tanzania Ili mizigo ya DR Congo isipitie Zambia bali ipitie Tanzania na kufika DR Congo kupitia Sumbawanga
Umeuliza swali zuri sana. Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inafanya yafuatayo kuhakikisha Nchi yetu inatumia vyema nafasi yake ya kijiografia.

1. Imeimarisha bandari ya Tanga kwa kuiongezea vitendea kazi hususani mashine za kushusha na kupakia mizigo

2. Inajenga barabara ya Mtwara-Tandahimba-Newala (barabara ya uchumi) itakayorahisisha biashara na nchi jirani za Malawi, Zambia hata DRC.

3. Imefunga taa na inakamilisha ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe ili ndege ziweze kutua muda wote na abiria wapate mazingira rafiki.

4. Imekamilisha ujenzi wa bandari ya Kalema (Wilaya ya Tangayika),Ujiji na Kibirizi (Kigoma) zote zipo mwambao wa Ziwa Tanganyika. Hizi zitarahisisha biashara baina ya Tanzania na Burundi na DRC

5. Inakamilisha ukarabati wa meli ya kubeba mafuta ya MT Sangara ziwa Tanganyika pamoja na kuanza ujenzi wa meli mbili mpya ya kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo katika ziwa hilo la Tanganyika zitakazoganya safari zake kati ya Sumbawanga, Tanganyika, Kigoma na Nchi jirani za DRC na Burundi.

6. Inakimbizana kukamilisha mradi wa reli ya kisasa SGR Dar-Morogoro-Dodoma-Singida-Tabora-Kigoma na Tabora-Kaliua-Mpanda. Hii yote ni kukuza biashara na nchi jirani.

Ndio maana tunasema Mama anaupiga mwingi
 
Haipo hoi kiuchumi kivile kama unavyotaka kuipimia tumewaacha kidogo tu hata ukiangalia GDP yao ni almost $53 Billion sisi tukiwa na $62 Billion..DRC isingekuwa na Warlords kila kona ya nchi ingekuwa bonge la nchi Africa hii kama wangetumia rasilimali za vizuri,suala la kuunganisha TZ na DRC lipo ndani ya uwezo wetu ikizingatia pia sisi ndio tunawahitaji sana DRC kuliko wao wanavyotuhitaj sisi maana wana option kibao
michakato inaendelea.
wawe wapole.
Tuna mpango wa kupiga lami kutoka kigoma hadi kalemii kupitia Moba na Potwe.
 
Umeuliza swali zuri sana. Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inafanya yafuatayo kuhakikisha Nchi yetu inatumia vyema nafasi yake ya kijiografia.

1. Imeimarisha bandari ya Tanga kwa kuiongezea vitendea kazi hususani mashine za kushusha na kupakia mizigo

2. Inajenga barabara ya Mtwara-Tandahimba-Newala (barabara ya uchumi) itakayorahisisha biashara na nchi jirani za Malawi, Zambia hata DRC.

3. Imefunga taa na inakamilisha ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe ili ndege ziweze kutua muda wote na abiria wapate mazingira rafiki.

4. Imekamilisha ujenzi wa bandari ya Kalema (Wilaya ya Tangayika),Ujiji na Kibirizi (Kigoma) zote zipo mwambao wa Ziwa Tanganyika. Hizi zitarahisisha biashara baina ya Tanzania na Burundi na DRC

5. Inakamilisha ukarabati wa meli ya kubeba mafuta ya MT Sangara ziwa Tanganyika pamoja na kuanza ujenzi wa meli mbili mpya ya kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo katika ziwa hilo la Tanganyika zitakazoganya safari zake kati ya Sumbawanga, Tanganyika, Kigoma na Nchi jirani za DRC na Burundi.

6. Inakimbizana kukamilisha mradi wa reli ya kisasa SGR Dar-Morogoro-Dodoma-Singida-Tabora-Kigoma na Tabora-Kaliua-Mpanda. Hii yote ni kukuza biashara na nchi jirani.

Ndio maana tunasema Mama anaupiga mwingi
Kabisa kada
 
Back
Top Bottom