Umeuliza swali zuri sana. Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inafanya yafuatayo kuhakikisha Nchi yetu inatumia vyema nafasi yake ya kijiografia.
1. Imeimarisha bandari ya Tanga kwa kuiongezea vitendea kazi hususani mashine za kushusha na kupakia mizigo
2. Inajenga barabara ya Mtwara-Tandahimba-Newala (barabara ya uchumi) itakayorahisisha biashara na nchi jirani za Malawi, Zambia hata DRC.
3. Imefunga taa na inakamilisha ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe ili ndege ziweze kutua muda wote na abiria wapate mazingira rafiki.
4. Imekamilisha ujenzi wa bandari ya Kalema (Wilaya ya Tangayika),Ujiji na Kibirizi (Kigoma) zote zipo mwambao wa Ziwa Tanganyika. Hizi zitarahisisha biashara baina ya Tanzania na Burundi na DRC
5. Inakamilisha ukarabati wa meli ya kubeba mafuta ya MT Sangara ziwa Tanganyika pamoja na kuanza ujenzi wa meli mbili mpya ya kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo katika ziwa hilo la Tanganyika zitakazoganya safari zake kati ya Sumbawanga, Tanganyika, Kigoma na Nchi jirani za DRC na Burundi.
6. Inakimbizana kukamilisha mradi wa reli ya kisasa SGR Dar-Morogoro-Dodoma-Singida-Tabora-Kigoma na Tabora-Kaliua-Mpanda. Hii yote ni kukuza biashara na nchi jirani.
Ndio maana tunasema Mama anaupiga mwingi