Kiongozi na Mzalendo Mushi nimekupa vizuri Mkuu;
Kwa maoni yako, suppose tunataka kuanza kutekeleza maoni yako, nilichopenda kujua tunaenda vipi kimikakati in terms of actions mpaka tufanikiwe? Nadhani hilo ndo kubwa kubwa na muhimu.
Kuna wanaosema viongozi wetu/politics ni wala Rushwa hivyo ndio maana Tanzania ni masikini,
sawa ndio lakini hivi duniani kuna nchi kusiko na Rushwa?one of the most succesfull economies are also the most corrupt.
nionavyo mie,we have problems with our system.hii ndio inalea hawa wanasiasa wala rushwa,lets work on fixing the system not leaders/leaders will come and go,the system will be there to stay.
i believe we don't need a kikwete to fix poor services in public offices,do we?
Tunamlaumu sana kikwete,lakini the guy will come and go,even worse leaders than him will come.
swali kwa TPN,mmeandaa any specific solution ya tatizo Lolote lile ili wengine wafuate mfano wenu?
Wengine wanatafuta channel za kutokea hapo
Wengine wanatafuta kuonekana nao wamo
Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi.
Kiongozi na Mzalendo Mushi nimekupa vizuri Mkuu;
Kwa maoni yako, suppose tunataka kuanza kutekeleza maoni yako, nilichopenda kujua tunaenda vipi kimikakati in terms of actions mpaka tufanikiwe? Nadhani hilo ndo kubwa kubwa na muhimu.
Wakati tumeanza harakati hizi nilikiita hiki tunachokifanya kuwa ni "mapambano ya kifikra".. Natumaini wanataaluma na watu wengine wanazidi kuona ukweli huu na jinsi gani ilivyo vigumu kubadilisha fikra.
Mzalendo Sanctus,
Usipoteze muda wako adimu hapa. Wewe endelea na mikakati yako. Mwishowe nawe utaonekana "kichaa". Kaa chonjo.
Ni ushauri tu. Ila kama unao muda wa kupoteza hapa, basi endelea kujibu ....
Wakati tumeanza harakati hizi nilikiita hiki tunachokifanya kuwa ni "mapambano ya kifikra".. Natumaini wanataaluma na watu wengine wanazidi kuona ukweli huu na jinsi gani ilivyo vigumu kubadilisha fikra.
MKJJ;Nguzo kuu ya umasikini Tanzania ni mentality,ni mambo ambayo yanatia huruma ukiafikiria kwa undani zaidi...Mwalimu aliliona tatizo hilo mapema sana,na ndio maana na yeye akaja na siasa za ujamaa na kujitegemea,ile mentality ya kwamba "Hatuwezi" "Sisi ndivyo tulivyo" nk ndivyo vilivyomfanya atake kupambana na ile mentality ya kuomba omba na imani kwamba we can't do nothing,na kwasababu siasa zake zile zilikufa,kukawa na loophole,na sasa siasa zimekuwa kama michezo ya kipuuzi kwasababu as a nation hatuna vision wala mission.
Utani convince vipi kwamba tunaomba ili tuendelee?Kuna kiongozi wetu ambaye ameonyesha kuwa ana nia ya kuwazindua wananchi kwamba they can determine their future and that the can make a difference?kwamba their success is within their capacity?Mentality ya kuomba omba inawapumbaza wananchi na kuona kweli hatuna kitu,na wakati in reality rasilmali zinauzwa kwa bei chee.
Na kwahivyo basi mapambano haya ya kifikra yanahusisha kampeni mahsusi yatakayo ignite mapinduzi ya kijamii na kifikra,wananchi wajuwe kuwa wana uwezo wa kuwawajibisha viongozi wenye ku act against the National interests.Tuna wanasiasa wazalendo lakini hawajui namna ya kudeal na issue hii,mwalimu alikuwa ni mtanzania,na alikuwa ni mpigania uhuru,hilo tu lingetosha yeye kutangaza tu kwamba anagombea na wananchi wampigie kura,lakini haikuwa hivyo,alienda kijiji by kijiji kata by kata,siku hizi hata hao ambao ndio wazalendo wameishia kwenye press conference tu,hakuna massive campaign to reach the people,ile ya ki "uhuru uhuru"na kwasababu ya mixture ya vyombo vya habari vya mafisadi vikiwemo,basi wananchi are totally confused na sidhani kama wanajuwa tofauti wanapoangalia hayo vs ze comedy...Kujua kuwa kipi ni comedy na kipi real...Wafanye kampeni waondoke huko maofisini,kampeni ya kuwaelimisha wananchi,kwamba we need change in direction and in the way we think,and that yes we can....Wananchi hawajui connection ya umasikini na uamuzi wao kwenye sanduku la kura kwasababu si wanaambiwa sisi ni masikini to begini with?Sasa kama kazi yetu kuomba omba unataka wasimchaguwe mtu mwenye personality ya JK?Wananchi hawajui kulinganisha ufanisi wa uongozi na impact yake kwenye maisha yao either a kila siku ama hata ya generation to generation.
Kwenye kuhusu ujamaa sijasema "Kunyanyua fikra" Nimesema ni jitahada za mwalimu kuwajengea watanzania mentality ya kujitegemea,kwamba they can do it by themseleves,aliliona hilo tatizo,nimefuatilia baadhi ya hotuba zake na nimegundua kuwa hilo lilikuwa tatizo na kuomba omba ama masharti ya kiugandamizaji alipingana navyo sana.Ninacho amini mimi ni the whole system is rotten,na hizo incentives kwa mfano kiuchumi zinzpatikana vipi?Unaweza kuwa na bidhaa za uzalishaji lakini wananchi wasiweze kuafford,hatuwezi kufanikiwa kama incentives tunazotegemea ni nje ya soko letu la ndani,incentive for more innovation ni a successfull marketing,kwamba mwishowe utauza,nijambo la maana umerecognize hilo la incentive,kwasababu lack of incentive ndio mazingira hayo tunayozungumzia yenye kusababisha wataalam legit washindwe ku utilize utaalam wao kwa maendeleo ya Taifa....Na kwa kumalizia tu ni kwamba statement yako haijakamilika unaposema "They will do things on their own" kwasababu if there is incentives invlolved then they just cant do it "on their own"Jmushi1:
Watanzania na miradi yenu ya kumuinua mtu kifkra (mentality), mnapoteza muda na resources tu. Na ujamaa kilikuwa sio chombo cha kunyanyua fikra za mtanzania.
Kukiwa na incentives za watu kujifunza au kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao, they will do a lot of things on their own.
Preamble
Tanzania is among the poorest nations of the world where more than fifty percent of her population live below the poverty line; and that the main cause of poverty is under development which can be expressed in terms of unemployment, underproduction, high rate of illiteracy, low level of Science and Technology and imbalance in its trade balance caused by among others unmanageable external debt and lopsided international trade practices.
Hii preamble hata hivyo inanipa matatizo kidogo - Ni kweli kuwa Tanzanaia ni kati ya nchi masikini duniani lakini umasikini wetu ni mavuno ya zao kutoka shamba tulilolifyeka na tukalilima sisi wenyewe. Baada ya hapo tulipanda mbegu, tukapalilia, tukamwagilia na sasa tunavuna tulichopanda. Kwa kifupi tumeendelea kujenga utamaduni wa kuuona huu umasikini kama jadi yetu kiasi cha kutokuona haya kuwa omba omba. Bado hatuuoni huu umasikini kama adui wa kupigwa vita kwa nguvu zetu zote badala yake tunaona fahari kuendelea kuukumbatia.
Tulipofikia maazimio pekee hayawezi kuleta mabadiliko kwani mfumo ambao umewezesha status quo uko pale pale - intact. Kongamano, semina, warsha na vikao vilivyoota kama uyoga mpaka sasa vime contribute positively nothing katika maendelao ya taifa. Kinachohitajika ni utekelezaji lakini chini ya mfumo wetu, tunajidanganya kama tunafikiri tutafanikisha lolote bila mabadiliko ya msingi - KATIBA. Vyombo vyetu vinaongozwa na wataalamu waliobobea lakini utendaji wao unatawaliwa na maslahi binafsi - kubwa ikiwa kulinda nafasi zao.
Katiba imeweza kumwagilia na kurutubisha mindset ya ubinafsi katika taifa na hivyo kuwalinda waajiriwa(viongozi) wasiweze kuwajibishwa na mwajiri mkuu(wananchi) na hivyo kuwapa kiburi cha ajabu. Wengi wa wanataaluma na wasomi wetu kwa woga na tamaa wakaamua kuvaa miwani nyeusi na kuweka rehani taaluma zao kwa kujiunga na staus quo. Ningefurahi zaidi kama kongamano za aina hii zingejikita zaidi katika kuangalia mapungufu na muundo wa Katiba na kudai iandikwe upya - Shamba lazima lifyekwe kwanza kabla ya kupanda zao.
Hivi WATAALUMA ndio kina nani na ni sifa zipi wanazopaswa kuwa nazo ili watambulike hivyo? Isije ikawa mambo ya Wasomi wapinga halafu unakuta ni wanafunzi ambo hata degree moja hawajaipata bado...
omarilyas
?1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara