Kuuza wazo la biashara kwa bank

Kuuza wazo la biashara kwa bank

Tuliwonda

Senior Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
121
Reaction score
35
Salam wakuu,
Mimi ni mjasiliamali, hivi karibuuni nikiwa katika harakati zangu za kujigomboa na umaskini, nimekutana na fursa nzuri, ambayo itawahusisha bank na hao wateja!! Sasa nnachoomba wakuu mnisaidie jinsi ya kulifikisha wazo langu kwa wahusika wakuu. Mimi ningependa sana kuliuza wazo hili, kwa bank ya crdb. Please msiniuluze kwa nn crdb? manake itabidi nianze maelezo mengine, ila kwa ufupi ni kwa sababu ndo bank ya kizalendo nnayoiona inajitahidi kwenda na wakati kwenye kila nyanja za huduma zake... niliwaza kuwaona ma branch manager wa banks zilizo karibu nami, ila naogopa kupigwa juu kwa juu!! Mwisho una shangaa wazo linafanyiwa kazi, branch manager kapandishwa cheo, wewe hakuna hata anaekujuwa!!! Tafadhali nisaidieni connection za kulifikisha wazo kwa wakubwa ikiwezekana kwa Mr, Kimei mwenyewe. Pia naomba ieleweke kwamba ni wazo la biashara ambalo litainufaisha bank na wananchi wahusika. Ikitokea crdb hawatalikubali, basi ntarudi kuwataarifu na kuomba tena mnisaidie connection kwa bank nyingine. Ila naamini lazma crdb walikubali. Natanguliza shukrani za dhati, ndimi katika kujikwamua na umaskini.
Dada Tully.
 
Kiongozi kweli unatakiwa uwe makini na hawa Loan Officers juzi nilitoka kutekeleza hatua zangu za kuchukua mkopo yani yule Branch Manager alikua ananiuliza na kunichimba sana ila nilimpa tu highlight juu juu naona alikua anataka kucopy na kupest.
 
Salam wakuu,
Mimi ni mjasiliamali, hivi karibuuni nikiwa katika harakati zangu za kujigomboa na umaskini, nimekutana na fursa nzuri, ambayo itawahusisha bank na hao wateja!! Sasa nnachoomba wakuu mnisaidie jinsi ya kulifikisha wazo langu kwa wahusika wakuu. Mimi ningependa sana kuliuza wazo hili, kwa bank ya crdb. Please msiniuluze kwa nn crdb? manake itabidi nianze maelezo mengine, ila kwa ufupi ni kwa sababu ndo bank ya kizalendo nnayoiona inajitahidi kwenda na wakati kwenye kila nyanja za huduma zake... niliwaza kuwaona ma branch manager wa banks zilizo karibu nami, ila naogopa kupigwa juu kwa juu!! Mwisho una shangaa wazo linafanyiwa kazi, branch manager kapandishwa cheo, wewe hakuna hata anaekujuwa!!! Tafadhali nisaidieni connection za kulifikisha wazo kwa wakubwa ikiwezekana kwa Mr, Kimei mwenyewe. Pia naomba ieleweke kwamba ni wazo la biashara ambalo litainufaisha bank na wananchi wahusika. Ikitokea crdb hawatalikubali, basi ntarudi kuwataarifu na kuomba tena mnisaidie connection kwa bank nyingine. Ila naamini lazma crdb walikubali. Natanguliza shukrani za dhati, ndimi katika kujikwamua na umaskini.
Dada Tully.
Nenda mahakamani ukaliwekee haki miliki wazo lako,then ndio ulipeleke bank.
 
Kwa Maelezo yako tu hata mie sikupi.
Maana ukiangali kwa kina kujieleza kwako ni kwamba umeishakata tamaa ya maisha na pesa ukizipata zitakukoma.
Business Ideas watu wanazo nyingi sana na sio useme kwamba lazima Crdb watazikubali.Maana hakuna jipya utalopelekea wao wawe hawana watu kama wewe walioplekea mwazo yao.
Wazo linaangalia zaidi na uhalisia wako binafsi,mie naweza kuwa na wazo kama laki ila mie nikakosa mkopo wewe ukapata,na ndio maana baada ya kusoma huwa wanakuuliza maswali.
Na pia faham kwamba mikopo haitoki kienyeji kama unavyofikiria,kuna teams ambazo zinawatu wenye uhusika na sehem husika watajua kwamba ukweli upo wapi.
Business Ideas hata uki Google unazipata kibao.

Ukipenda kujita maskini wakati mungu bado anakupa pesa ya kula basi jue unamchukiza sana mungu.
Kama unapata kula hata milo miwili kwa siku wewe sio maskini.Maskini waliotajwa hata kwenye vitabu ni wale wasijiweza na wenye mlo wa kubahatisha.lakini wewe hadi pesa ya kulipia mtandao unayo.
Weka mawazo kwamba umaskini ni mapito tu,basi hapo iutafanikiwa,lakini ukikalia kuuimba kama wimbo na wenyewe utakuzoea.
Mie Binafsi,naapa mbele ya mungu sio Maskini,na wala sio tajiri.Ila naamini mungu siku yoyote anaweza kunipitisha kwenye njia ya umaskini kama mapito.
 
Mkuu zanzibar spices: unaposema kujieleza kwangu ni kwamba pesa nikizipata zitanikoma manake nn? Hivi pesa kazi yake ni nini? Dreaming is believing na believing is achieving!! Nikikwambia nilipotoka hadi hapa nilipofika leo!! Basi itabidi ubadili hizo negatives zako zote na kuweka ma positive matupu! Kwenye issue ya kujiita maskini, wapi nimesema mimi ni maskini? Au kusema najigomboa kutoka kwenye umaskini ndo kosa? Hizo si ni lugha tu kama vile mtu kuita billions vishilingi!! Vp kama hii internet nimeomba simu ya jirani yangu? Plz tuache kuwa na majibu ya kukatisha watu tamaa na badala yake tupeane moyo au kusahihishana kwa hoja zenye mashiko.
 
Niliwahi kuuliza hilo suala ka kusajili wazo la biashara humu jf Ila ckupata majibu ya kuridhisha,..
 
Nasikitika kuona tunakatishana Tamaa Watanzania.
Huyu anahitaji connection apeleke wazo lake aliuze, na siyo kupewa Mkopo.

FUATA HATUA ZIFUATAZO
  1. Andaa Business Concept yako vizuri kwa Mtiririko wa jinsi itakavyofanyika mwanzo mpaka mwisho. Ikiwa na mawasiliano yako.
  2. Bind Business Concept yako vizuri
  3. Kama Idea ni yako peke yako andaa si zaidi ya Elfu themanini (Tsh.80,000/-)
  4. Kama Idea ni ya kikundi,kampuni au partnership andaa si zaidi ya Laki moja na elfu kumi (Tsh.110,000/-) pamoja na barua ya makubaliano baina ya mtoa wazo mkuu kuthibitisha kuwa wazo sasa siyo lake bali ni la kikundi,kampuni au partnership.
  5. Nenda COSOTA (Ofisi zao zipo Morroco kwa sasa), kuna forms watakupa utajaza. Then utakusanya wao watazipitia zile forms na kuipitia Business Concept yako kwa kuangalia kama ilisha sajiliwa ama laa.
  6. Kama haijasajiliwa utapewa usajili wa Idea yako na Certificate.
HAPO SASA UTAKUWA NA UWEZO WA KUIPELEKA HIYO PROPOSAL POPOTE OPEN NA ISIIBIWE

KWA MAELEZO NA UFAFANUZI ZAIDI JUU YA MAMBO HAYA WASILIANA NASI
AfriNet Core Tanzania
Sinza Makaburini - Igesa Road
Mob: +255 755 257 508 / +255 713 741 758
Email: info@afrinet.co.tz/ corneliousbk@gmail.com

JIFUNZE KUFUATA TARATIBU KWA USALAMA WAKO

Hauwezi kusajili wazo la biashara, kwa mfano hakuna mtu anayeweza kusajili wazo la kutengeneza soda, unachoweza kusajili ni zile unique process kama formula ya CocaCola etc. Hizi zinaitwa patents.

Pili niseme mawazo almost always ni useless na watu wana mawazo kibao, tatizo ni utekelezaji. Na ungejua jinsi benki zilivyokuwa slow kutekeleza hata idea zinazotoka kwa ma CEO wao basi chance zako sio nzuri hapa.
 
Mkuu zanzibar spices: unaposema kujieleza kwangu ni kwamba pesa nikizipata zitanikoma manake nn? Hivi pesa kazi yake ni nini? Dreaming is believing na believing is achieving!! Nikikwambia nilipotoka hadi hapa nilipofika leo!! Basi itabidi ubadili hizo negatives zako zote na kuweka ma positive matupu! Kwenye issue ya kujiita maskini, wapi nimesema mimi ni maskini? Au kusema najigomboa kutoka kwenye umaskini ndo kosa? Hizo si ni lugha tu kama vile mtu kuita billions vishilingi!! Vp kama hii internet nimeomba simu ya jirani yangu? Plz tuache kuwa na majibu ya kukatisha watu tamaa na badala yake tupeane moyo au kusahihishana kwa hoja zenye mashiko.

Mpotezee huyo
 
Back
Top Bottom