KERO Kuuziwa bites ndani ya treni ya SGR ndio utaratibu mpya au wafanyakazi wameanza hujuma?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Akibinafisisha mtaongea tena
Kuongoza mtu mweusi ni kazi sana
 
Hilo laweza kuwa ni nufaika la huo ubaradhuli.
Lipo mkupiga kampeni za kifisadi tu hapa!
 
Nijuavyo mimi huwa kila ofisi huwa na meneja je katika safari hiyo mwisho wake uliweza kuongea na meneja wa hicho kituo kumuuliza haya?

Accountability ndio kitu kimewashinda watanzania
 
Nadhani kwenye malalamiko tungeweka zaidi ya ile huduma yenyewe ya usafiri, ili tusikilizwe na kutatuliwa kwa haraka na huduma ya usafiri kuimarika.

Lakini, tukianza kuchanganya na malalamiko ya kuuziwa maandazi na sambusa badala ya kupewa bure, tunaweza kuonekana tuna hila.

Labda, kwa wakati huu ambao TRC wanataka sana maoni/ malalamiko yetu ili kuboresha usafiri huu mpya, tujikite kwenye zile shida za msingi.

Ova
 
Masanja Kadogosa weka msemaji wa shirika awe anatoa ufafanuzi wa kila huduma kwenye SGR.
Watanzania tuna maswali mengi yanayohitaji majibu ya Shirika.
 
Watanzania wacheni kulalamika katika kila jambo dogo AISEE.
Hadi bites mnalalamikia!!???
Wacheni kujiendekeza banaa badilikeni.
Mzee, siku ukilipa 10k kununua luku wakakuletea unit 8 badala ya 28, utalalamika au hautalalamika..??
 

je walikuandikia kwenye ticket yako kwamba unastahili kupata bites bure?
 
In the capitalist system there is no free services
 
Hizi train sijui kama zitamaliza mwaka.Maana hazijamaliza hata mwezi lakini changamoto lukuki.tiketi shida,mara msimame njiani sababu ya umeme
 
Treni za umeme za majuu pia zina huduma za kulipia bites na meal ni kama Mambo ya fast jet.

Kwa experience yangu treni nilizopanda nje ya Tanzania Hakunaga mambo ya free meal kwenye train nyingi. Vyakula huwa wanauza.
Wabongo unaweza kuwauzia kitu kwa bei chini ya operational cost, kwa government subsidy, halafu pia bado wakalalamika.
 
Muwe makini sana na hivyo vyakula mnavyoletewa au kuuziwa humo kwenye treni, muwe waangalifu.

Possibly, it's "Another Game of Russian Roulette."
 
Umenikumbusha nilikosa korosho ndani ya Air Tanzania (Dom-Dar). Waligawa korosho na ziliishia kwa watu waliokaa seats za mbele yetu nikadhani wataenda waongeze zingine, ikawa ndio nitolee hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…