Hiyo unayosema 'Big G' ni rtv (room temperature vulcanizing) silicone gasket inatumika kuunganisha 'cylinder head' na 'valve cover' badala ya valve cover gasket.
Hiyo 'rtv' imeharibika (imeacha ka upenyo) na kuruhusu 'oil' kutiririka nje wakati engine ikiwa kwenye mzunguko mkubwa (high rpm).
Matengenezo
Kwa kutumia rtv
Unatakiwa kuibadilisha, kwa kufungua 'valve cover' na kuikwangua ile (Big G) ya zamani na kuipaka mpya.
Zifunge hizo nati kwa vidole mpaka ziwe ngumu kukaza, ziache kwa dakika thelathini ili hiyo 'Big G' isambae kidogo halafu tumia wrench/spanner kuzikaza kwa robo mzunguko (a quarter turn).
Wakati unafunga nati fuata mfululizo maalumu wa hiyo injini (torque sequence).
Ipe kama masaa 24 ikauke vizuri halafu washa moto.
Kwa kutumia gasket
La sivyo, badala ya kutumia rtv nunua valve cover gasket na kuiweka. Hii haita hitaji kusubiri muda wa kukauka. Lakini lazima ufuate toque sequence kukaza nati