Kuvuja oil katika Cylinder head.

Kuvuja oil katika Cylinder head.

Babafetty

Senior Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
107
Reaction score
108
habar wadau,

nina gari aina ya starlet, nlinunua kwa mtu, muda kidogo umepita, injini yake iko poa, ila katika cylinder head katika vile vimrija kama pameungwa na bigijii ngumu hv,(nahis gari ilichemka akafungua injini) sasa ktk maungio hayo huwa kuna injini oil inatoka kwa mbali hasa nkienda mwendo mrefu.

je naweza kutatuaje tatzo hilo?

ni madhara gan yanaweza jitokeza km ntaendelea kutumia gari ikiwa katika hali hii?

6ee766f40e3a817abd9933acb99a1a3e.jpg
20171230_221004.jpg
 
Kwangua vizur hiyo bigijii iliyogandikwa na pakaushe vizuri paka bigijii nyingine,hiyo ni leakage tu.
 
Cylinder head itakuwa na crack
 
Nina tatizo hilo pia kwa gari yangu. Plz mtaalam atushauri ili kutatua tatizo hilo

Msaada wa kiufundi unategemea na maelezo ya tatizo.Mada husika haijakidhi maelezo.Mfano anasema kwenye "mirija ya clynderhead" Sasa hapo utaelewa nn kiufundi!! Lkn baada ya kuzoom picha nimegundua kwenye cylinder head cover ndio penye tatzo.
 
Oil imefikaje kwenye cylinder head mpaka ikavuja?

Oil pump ndio yenye jukumu la kuhakikisha oil inafika sehemu zote za engine kulingana na mfumo wake.Sasa unapozungumzia Oil pump,ni Chombo ambacho kinakimbiza kwa nguvu mafuta (oil).Kutokana na nguvu ya oil kutafuta eneo husika panapopatikana mpenyo(leakage) lazima oil ipitie hapo.
 
Oil pump ndio yenye jukumu la kuhakikisha oil inafika sehemu zote za engine kulingana na mfumo wake.Sasa unapozungumzia Oil pump,ni Chombo ambacho kinakimbiza kwa nguvu mafuta (oil).Kutokana na nguvu ya oil kutafuta eneo husika panapopatikana mpenyo(leakage) lazima oil ipitie hapo.
oh,
thanks,
solution ni nn ktk hilo..
 
Solution; angalia vizuri hiyo top cover hasa hapo panapovujisha oil.Dhibiti kwa gundi (Arladite).Kama bado panapuliza oil..,basi badirisha hiyo top cover.
oh,
thanks,
ni wazo zuri, ntaanza na kuziba.
 
Hiyo unayosema 'Big G' ni rtv (room temperature vulcanizing) silicone gasket inatumika kuunganisha 'cylinder head' na 'valve cover' badala ya valve cover gasket.

Hiyo 'rtv' imeharibika (imeacha ka upenyo) na kuruhusu 'oil' kutiririka nje wakati engine ikiwa kwenye mzunguko mkubwa (high rpm).

Matengenezo

Kwa kutumia rtv
Unatakiwa kuibadilisha, kwa kufungua 'valve cover' na kuikwangua ile (Big G) ya zamani na kuipaka mpya.

Zifunge hizo nati kwa vidole mpaka ziwe ngumu kukaza, ziache kwa dakika thelathini ili hiyo 'Big G' isambae kidogo halafu tumia wrench/spanner kuzikaza kwa robo mzunguko (a quarter turn).

Wakati unafunga nati fuata mfululizo maalumu wa hiyo injini (torque sequence).

Ipe kama masaa 24 ikauke vizuri halafu washa moto.

Kwa kutumia gasket
La sivyo, badala ya kutumia rtv nunua valve cover gasket na kuiweka. Hii haita hitaji kusubiri muda wa kukauka. Lakini lazima ufuate toque sequence kukaza nati
 
Hiyo unayosema 'Big G' ni rtv (room temperature vulcanizing) silicone gasket inatumika kuunganisha 'cylinder head' na 'valve cover' badala ya valve cover gasket....
Thanks sana kk.
 
Cylinder head inaweza ikawa imepinda so kainyooshe haina shida haswa kama ilikua inachemsha joto limeifanya ipinde
 
Hiyo unayosema 'Big G' ni rtv (room temperature vulcanizing) silicone gasket inatumika kuunganisha 'cylinder head' na 'valve cover' badala ya valve cover gasket...
Asante sana Mkuu. Japo kuwa ni kiporo.
 
Japo kiporo ichi lakini kwa yoyote mwenye tatizo ilo ajue hio ya juu ni top cover, ni rahisi kufix, unaifungua unaweka gasket maker nyengine unafunga unasubiri ivuje tena urudie process. Oil kuvuja kwenye head shughuli yake ni pevu. Exhaust itakuhabarisha
 
Back
Top Bottom