Huyu aliyeandika hapa sijui kama ni wakili, au ni mwananfunzi anayesoma sheria chuo flani na yupo law shool au hata bado hajafika Law School.
Samahani sana msomi maana siamn kama ww ndio umeandika ujumbe huu. sina maana mbaya na ww (don't take it personal) ila kuna vitu haviko sawa.
Kama ulifika law school na hiki ulichokiandika hapa unakimaanisha nakuhakikishia ulifeli unless ulibadili mtazamo wako kwasababu:
1. Kusema law school sio shule ya vitendo nimekosa tusi zuri la kisomi kuzungumzia hii kwasababu ni upotoshaji mkubwa. Kuna watu wanamaliza LL.B hajui hata plaint inafanana vip. Ila anajua mtu akitaka kusue anaandaa plaint na kupeleka mahakaman. Plaint inafananaje hajui. Anajulia wap? law school.
2. Kuhusu field ni kwel marks haihusiki kwa GPA lkn ukifaulu somo la field hauhesabiwi umefeli bado unakuwa umefaulu vilevile.
3. Ungekuwa ushaingia law school ungejua angalau kwamba kuna firms za watu wasio zidi 30 na hao 30 wakifika firm wanagawanywa zaidi kwenye makundi madogo madogo ambako hakuna zaidi kinachofanyika zaidi ya practice tena ya mtu mmoja mmoja plus moot courts ambazo zinafanyika mara kwa mara kama hatua za kujifunza.
4. Refers aya ya 3 hapo juu.
5. Ulichofundishwa RUAHA UNIVERSITY ulifundishwa land, law school unafundishwa conveyancing, sasa usipoijua tofauti ndio maana nakuambia utafeli asubuhi tu.
6. Baadhi mtihani inapewa hadi masaa saba ya kufanya mtihani (WPE) mmoja. Yani unaingia kwa mtihani unafanya research, unapumzika saa moja, unarud tena unafanya pepa 3 hrs. Ulitaka mtihani mmoja ufanywe kwa masaa mangapi? Au ulitaka mtihani mmoja ufanywe siku tatu.
7. Siwez hata kuingolea maana ni hearsay. Ila kikubwa kama utaingia law school unadhani ukisalimia mtu (secretary) utafaulu, utaliwa kichwa asubuhi tu, unadhani secretary anamchango gani kwenye mitihani yako. Hii ni tofauti sana na vyuo vya chini huko, ambako mtu anafaulu kwa njia tofauti tofauti mbali na kusoma, LST camera hadi uani. Kuna vyuo hasa private (sivitaji kulinda bland zao) mwanafunzi maadamu amelipa ada tu, basi ashafaulu. unakutana na mtu ana GPA ya 4+ kichwani hakuna kitu.
8. Kwan hakimu anajua kila kitu? Vip kuhusu Human rights, accounting, basic health for lawyers (km bado lipo). Kwahyo kama atafeli masomo ambayo hayapo kwenye himaya ya uzoefu wake.
9. I think this is good fact. No comment.
10. Sina ushaidi wa kutosha.
11. Uongo wa waz waz. Mm nilisoma UG masomo zaidi ya 40 lkn law school ni masomo 11 Unawezaje kusema uongo wa wazi kiasi hiki. Mfano mwingine land law UG ni topics 12 lkn LST ni topic 5 to tena kwa vitendo. Only documents. Hivo hoja hii ni upotoshaji mkubwa.
Mm nipende kuwaasa vijana hasa wanaotaka kuwa wanasheria professional, wasiogope idadi ya watu wanaofeli na maneno ya mtaani. Hakuna kitu ambacho hakiwezekani. Waliotoka first sitting kwani wao wana nn? Hawakuzaliwa nao.
Sijisifii ila naona mfano huu utawasaidia. Wakati ss tunasoma LST nilikuwa nakaa meza ya mbele kabisa na wadada wengine watatu (mkaka peke yangu) mdada mmoja nilitoka nae chuo kimoja na wale wawili wote walitoka UD. Hatukuwa na maakili kiviiiile. Ila tulikuwa na mkakati wetu maalumu wa
kusoma kuelewa, kusoma kumalizia na mwisho wa siku wote wanne tulitoka
first sitting
ukweli hsiopingika nilisoma sana Law School sijawahi kusoma vile toka dunia iumbwe (sio Primary, secondary, UG wala LL.M). Ilifika sehem nimemaliza law school nilikuwa wamoto, madini kichwani ni kiasi cha kuona miaka yangu mitatu ya Mzumbe ilikuwa ni kunitoa ujinga wa HKL tu na sio kunifanya niwe mwanasheria professional.
Mwezi mmoja baadae nilipoingia mtaani kuomba kazi, interview ya kwanza tu niliyofanya mwajiri hakutamani kunipoteza. Sio kwasababu nilikuwa anakili sana ni kwasababu law school ilinipika nikapikika. Mfano, moja ya swali nakumbuka niliulizwa kuelezea parts za afiidavit. Nilikuwa n alijibu swali hilo hadi natabasamu.
Leo minavyoongea wale madada watatu mmoja ni hakimu, mwingine ni wakili wa serikali taasisi fulani (soon after LST) , mwingine ni wakili mzuri wa kujitegemea. Yote hii ni kwasababu tuliizingatia LST na tulisoma.
Ukisoma vizur hata ikitokea ukafeli hautafeli kama ambao hawajasoma.(japo naamn bahati mbaya huwa zipo mtu anaaamka vibaya, imani za upande wa pili nk.).
Wito wangu kwa watumishi wa LST waendelee kutenda kazi kwa uadilifu mkubwa, na wasimhofie yoyote kwa kigezo cha kuogopa makelele, kama mtu msuli wake mdogo arudie hata km ni zaidi ya mara 40. Taaluma zote ni kawaida sana, km vile jamaa zetu wa CPA na wengine, hali ni hii hii.
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile