enzo1988
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,838
- 7,346
Siyo kwa lengo baya wala majungu, fitina, chuki , husuda n.k.! Kwenye utawala wa Kikwete jina la Ridhiwani lilivuma mno lakini likiegemea zaidi upande hasi! Yaani ilitengenezwa picha kwamba mtoto ni bonge la fisadi!
Pia kwenye utawala wa Samia kuna jina la Abdul limeshika hatamu kwenye kila nyanja! Jina linavuma kwenye upande hasi! Yaani unatengenezewa picha mpaka unaogopa!
Najua siasa ni mchezo mchafu iwe kwenye nchi zilizoendelea na zisizoendelea! Inawezekana maadui na mahasimu wao wa kisiasa wanachezesha kete!
Sitaki kufahamu kama ni kweli au si kweli, ila huwa naona kama taasisi ya urais huwa kama inachafuka mno na kutia aibu!
Wazazi wao huwa hawalioni hili? Washauri wao huwa hawalioni hili? Watoto wenyewe huwa hawalioni hili? Wanaolinda hadhi ya taasisi huwa hawalioni hili?
Naomba nikumbushwe na kusahihishwa kama mtoto wa Nyerere, Mkapa na Magufuli walivumishwa sana kama hawa wawili! Kwa Mwinyi mke alivuma sana!
Nb: Ni mtazamo tu, lete wa kwako!