Kiranga sagaciR Suala la ndoa ni muunganiko unaohitaji ridhaa ya mwanaume na mwanamke (au wanawake kama ndoa ni ya mke zaidi ya mmoja). Lord Kenyon katika kesi ya
Atchinson v. Baker alisema, nanukuu;
“….it would be most mischievous to compel parties marry who could never live happily together.” Maneno haya yanadhihirisha kua hakuna sheria au mamlaka yoyote inayoweza kulazimisha watu kuoana, isipokua kwa ridhaa yao na pia kuzingatia misingi na vigezo vingine vilivyowekwa na kutambuliwa kisheria. Kimsingi, andiko hili linalenga kukupa mwanga juu ya namna gani suala la kuvunja ahadi ya ndoa (breach of promise to marry) linatambulika na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hasa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kueleza kwa kifupi haki za wahusika katika uchumba huo pindi ahadi kuoana inapovunjika.