Kuvunjika kwa kundi la vichekesho la Orijino Komedi

Kuvunjika kwa kundi la vichekesho la Orijino Komedi

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,699
Reaction score
4,117
Habari zenu

Tukiwa hapa kijiweni Bamaga, tukipiga story mbili tatu anakuja jamaa Mshikaji wetu anayefanyia TBC ambapo Ni mmoja kati ya waendesha kipindi fulani...Baada ya kupiga story mbili tatu tumejikuta tunamwuliza kuhusu hili kundi baada ya kupotea ghafla katika ramani ya vichekesho.

Naye alichotujibu ni anasikia kundi limevunjika Kimyakimya kila mtu anapiga issue zake..

Kuna mwenye habari zaidi kuhusu Kuvunjika Kwa Group Hili???
 
uwenda maana siwaoni siku hizi
ila pia kama ni kupumzika kwa muda wangetangaza
 
Kwahiyo nani anafanya nn kwa sasa. Si mnataka tujadili watu?
 
uwenda maana siwaoni siku hizi
ila pia kama ni kupumzika kwa muda wangetangaza

Jamaa yetu hapa anadai inawezekana wamewekeza vya kutosha binafsi kiasi kwamba hawaoni tena haja ya kuendelea na kipindi kwani huwenda kipato wanachokipata mtu mmojammoja ni kikubwa kuliko kundi kwa ujumla...(Bado Ni Tetesi)
 
Kwahiyo nani anafanya nn kwa sasa. Si mnataka tujadili watu?

Lengo si kujadili mtu Jile79 ila ni mashabiki wao kupata uhakika kama kundi limevunjika ama?
 
Last edited by a moderator:
chezea udhamini!! Wachekeshe kipi wakati wapo chini ya mdhamin mkuu.
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe kwani Kwa Mfano tu Hai Ambao Nina Uhakika Nao Mtu Kama Joti Sidhani Kama Atakuwa na Hamu Tena Ya Kuendelea Na Comedy Wakati Kwa Kufanya Kwake Matangazo Makubwa Mawili tu Yale Ya Tigo Amepata AU Amelipwa Jumla Ya Tsh Milioni 80, Milioni 40 Kwa Kila Advert na Kuna Lingine Nalo Amelifanya Mwezi Uliopita ambapo Amelipwa Tsh Milioni 15 na Pia Tusisahau ile Picha Yake Ya Comedy ambayo Iliingia Sokoni Mwezi May Mwaka Huu Na Wahindi ( Wasambazi ) Wamlipa Tsh Milioni 50 na Sasa Mzigo Wote Wanausimamia Wao. Hivi Kwa Jumla Ya Pesa AU Malipo hayo Lukuki Atakuwa tena Na Hamu Ya Kutufanya Tucheke Kwa Comedy Zake? Sasa Wana Hela.
 
Hivi yule aliyekuwa anamuigiza mrema yuko wapi jamani. Mara ya mwisho ilisemekana ameenda matibabu India. Mwenye kujua tafadhali
 
chura je? uzuri wa hao jamaa wote ni kwamba, wameshajitangaza, wanaweza kuuzika kwenye eneo lolote lile. hata wakipigika leo wakiamua kuingia kwenye bongo movie watu watanunua tu iyo cd ili wawaone.siwaoni kwenye matangazo wakuvanga, mpoki, chura, masanja namwona kwenye gospel na injili, yule aliyekuwa anaugua sijui ameishia wapi.
 
Hawa jamaa kila mtu ana investment zake zinawaingizia sana hela,Joti amepata sana dili za matangazo mbalimbali
Masanja analima sana mpunga Mbeya na Shinyanga na ana kampuni ya ulinzi inaitwa OK security pia ni mchungaji
 
"ni utoto tu wakikua wataacha" kwa hiyo sasa wamekua wakubwa!! Vigogo !!
 
Duh.....mkuu hapo kwakweli hawezi rudi kundini kabisa!!
 
Nasikia jamaa bado anaumwa sana tu!!
 
Back
Top Bottom