landless
Member
- Mar 6, 2009
- 81
- 9
Jamani,nipo stranded kama wiki tatu sasa zimepita tangu wamespray na kunivunjiwa kioo cha gari,ilikuwa siku ambayo sunami ingetokea,siku ambayo mvua ilinyesha sana hapa mjini,mida ya saa tatu usiku,maeneo ya UPANGA,NYUMA YA SCOUT WANAPAITA COCONUT PUB,nahisi jamaa walikuwa na Tax nyeupe,wameniibia begi langu,likiwa na laptop mbili(HP pavilion dv5 {imekufa display ya inch 14.5),toshiba),external harddisk aina ya SEAGATE(250MB),original driving licence,kadi 2 za benki(NBC and CRDB),camera (Sony)ya pink,documents za office,kazi za consulting nilizotakiwa kudeliver a week before sijaibiwa.Worse enough ni external HDD niliyokuwa naitumia kama the only back up,ambayo nilitembea nayo ili nikahifadhi data zangu nyingine toka kwa office ina back up of almost four years works done.Im almost broke!!!.Nimejaribu kufuatilia nimeambiwa kuna jamaa wanaweza kunipatia taarifa nzuri maeneo ya kariakoo au posta.Nimefuatilia kupitia jamaa yangu mmoja(1) ambaye alifanikiwa kupewa namba ya hao jamaa wa mishemishe(2) wa kariakoo,wakamwambia watampatia jibu,last time wamemjulisha kuwa huo mzigo upo kinondoni wanapouza/kuhifadhia vifaa vya dili kama hivi,hivyo wakamjulisha(1) kuwa wanafuatilia huko nijiandae kwenda kugomboa,lakini hii sasa ni wiki ya pili jamaa(2) mda mwingine hapatikani,mara ya mwisho alimjulisha jamaa huyu (1)yangu kuwa mda mwingine inabidi azime simu kwa sababu ya inshu zake zinamfanya anatafutwa sana.Hivi jana nimepita maeneo hayo nikaiona ile Tax nliyokuwa naihisi,ikiwa inaodoka nikaanza kuikimbiza,lakini ghafla ikakata kona na kuingia mitaani,nimeifuatilia usiku,kuna mahali ikawa imepotelea sikufanikiwa kushika namba za gari,sasa naona kama uwezekano wa kuvipata unazidi kuwa mgumu.So wadau plz anyone mwenye ushauri namna gani ya kufanya au mwenye experience kwenye hili au na maeneo haya ya COCONUT PUB naomba ushauri kitu gani kingine naweza kufanya nikavipata hivyo vitu,muhimu zaidi ni ile external HDD.