Kuvuruga derby ya Simba na Yanga ni kuvuruga usalama wa Taifa na kuhujumu juhudi za Rais.

Kuvuruga derby ya Simba na Yanga ni kuvuruga usalama wa Taifa na kuhujumu juhudi za Rais.

DISHI LINGINE LINALOHITAJI FUNDI HASA Simba na yanga inavurugaje usalama wa Taifa katika masuala ya kitaifa vitu vinavyoleta mtafaruko ni 1.Vifo vya mara kwa mara 2. Hali ngumu ya maisha 3. Magonjwa
 
Rais Samia amebadilisha uelekeo wa soka letu kwa kutia juhudi binafsi kusuma michezo Tanzania. Hakuna asiyefahamu kuwa watu wa taifa letu wamegawanyika kwenye ushabiki wa simba na yanga kwa mamilioni.

Mtu kuahirisha mechi ya simba na yanga bila shaka anadhamiria yatokee mambo mabaya sana kwa taifa kisiasa, kimichezo, kiuchumi na kiusalama, hafai kuwepo hapo alipo kama yeye ni kiongozi wa mpira au serikali.

Lazima deep state ihangaike na watu hawa kama inavyohangaika na magaidi; maana iko siku watasababisha maafa makubwa sana nchini. Tusipende kusubiri yaharibike ndio tutoe vichwa vyetu mchangani.

Mchelea mwana kulia atalia yeye.
Chukua hii: ilikuwa ni siku ya wanawake duniani, raisi aalihutuba na Chadema/TAL alihutubia. Ujumbe ni NOREFORM NO ELECTION. Ili ujumbe wa lisu usisikike na kupokelewa na watanzania ahirisha mechi ili watu wajadili mechi badala ya ujumbe wa lisu.
 
Vipi Yanga na Simba wangecheza Ile Machi 8, 2025, Mhe. SSH angetrend katika kilele cha siku ya wanawake pale Arusha?! Siku ya wanawake ingekuwa historia na story ingekuwa matokeo ya mechi ya Yanga na Simba.
CCM siyo wajinga kiasi cha kufelisha kampeni yao wenyewe?!🤣🤣🤣🤣🤣
Daaah kakaaa!!! mechi yenyewe ilikuwa tarehe 8 tena usku wa manane baada ya sherehe za Arusha kukamilika. Kuahirisha mechi ndio kungefunika kabisa sherehe yenyewe kama ni hivyo, maana tukio lile walizungumzwa sana kuliko hata matokeo yangekuwa. Simba kala uyonyaaa, kona, chaka, nyambui, duma, swala. Waliona bora lawama kuliko fedheha ya kufungwa mara 5 mfululizo; machale yaliwacheza
 
Back
Top Bottom