Kuwa makini kabla ya kutoa idhini kwa Programu Wezeshi kwa aina zote za maelezo inayoomba

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Kuruhusu programu kupata taarifa binafsi kama vile eneo, kamera, na namba za simu "Contacts" inaweza kuwa na madhara, kwani zinaweza kukusanya na kutumia taarifsa zako binafsi bila mtumiaji kujua au kutoa ridhaa.


Pia inaweza kuongeza matumizi ya data na kupelekea chaji ya simu kuisha haraka, kwani programu inapata ruhusa za kutumia vipengele vingi zaidi kuliko inavyohitajika.

Aidha, kuna programu ambazo haziwezi kufanya kazi bila kuwa na ruhusa za baadhi ya taarifa zako kwa mfano Google Maps inashauriwa kuchagua "Ruhusu wakati tu wa kutumia programu" (Allow only while using the app) ili uweze kutumia programu hiyo
Namna ya Kudhibiti Ruhusa za Programu Wezeshi kwenye Simu za Mkononi:

1. Kwa Android:
a. Fungua Mipangilio (Settings)> Gusa Programu Wezeshi (Apps)


Chagua programu husika


Bofya Ruhusa (Permissions)


Chagua, ama Uliza kila muda au Ruhusu unapotumia Programu


b. Fungua Mipangilio (Settings) > Gusa ‘App Management’ > Chagua ‘Permission Manager’ > Chagua kitu kinachohitaji Ruhusa > Chagua Programu husika > Ruhusu, ama Uliza kila muda au Unapotumia Programu

2. Kwa iOS:

Fungua Mipangilio (Settings)


Bofya Programu Wezeshi (Apps) >

Chagua Programu husika


Chagua kitu kinachohitaji Ruhusa > Ruhusu, ama Uliza kila muda au Unapotumia Programu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…