Kuwa makini mwanaume mwenzangu unapoingia saluni za Sinza

Kuwa makini mwanaume mwenzangu unapoingia saluni za Sinza

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
"Karibu brother"
"Asante, nataka kunyoa ndefu tu na kupunguza hizi za pembeni"

Unamaliza, anaitwa binti akuingize kwenye chumba, unajua unaenda kuoshwa, lakini anakukalisha kwenye kiti.
"Nikufanyie skrabu"
"Hapana, labda siku nyingine"
"Inaonekana hujafanya skrabu siku nyingi. Hapa tuna skrabu ya coffee, ni nzuri sana. Ngoja ujaribu leo. Halafu nakuweka na chumvi."

Unatulia.
"Nikimaliza nitakupaka asali kwa dakika 10 kisha nakuosha"
"Inasaidia nini?"
"Uso wako una mafuta sana, sasa asali inasaidia kuondoa mafuta na chunusi"

Anakuminyaminya pale weee, kisha asali twiii. Halafu unasikia,
"Sasa hapa inatakiwa ukae kwenye stima kwa dakika kama kumi na tano hivi"
"Hiyo ya nini tena?"
"Inafanya uso wako uwe laini, na inaondoa makunyanzi"
"Okay"

"Pia tunafanya masaji ya kichwa, maana naona una mba kweli"
"Ohh"
"Pia tunaosha na miguu. Tunakata kucha"
"Ahhh, hiyo tutafanya siku nyingine"

Unamwachia uso na kichwa, anakuminyaminya mabega, unamaliza anakuosha, anakupaka tulosheni usoni, tumafuta kichwani anakupulizia na kale kasprei.

Anajipukuta, unauliza bei.
Anakusimamia mbele kama anataka kuanguka na tule tumatege, anaongea kama jambo la kawaida vile,
"Elfu sitini"

Mwenyewe ulipanga unyoe ndefu na kuchonga kwa elfu tano.

NB:
*Msisahau kuhakikisha kama majina yenu yamo kwenye daftari la wapiga kura.*
 
Nakumbuka hela kubwa kutumia kunyoa saluni ilikuwa ni Tsh 2,000/- ilikuwa mwaka 2015 Nyanda za juu kusini humu humu nchini Tanzania.

Sisi tuna saluni zetu wenyewe.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kunyoa ndovu na nywele inafika 5elf?
Buku inatosha
 
Mimi huwa nawaambia kabisa kuwa sitaki kingine zaidi ya kunyoa.. na bei unauliza kabisa.
 
Back
Top Bottom