Kuwa makini mwanaume mwenzangu unapoingia saluni za Sinza

Kuwa makini mwanaume mwenzangu unapoingia saluni za Sinza

Kwahiyo ukawa unaitikia tu[emoji3][emoji3]

Kuna jamaa kkoo alipewa bill 120k...

Mimi huwa nafanya huduma ambayo nimeiplan,hawaezi nishawishi kwa lolote!
 
"Karibu brother"
"Asante, nataka kunyoa ndefu tu na kupunguza hizi za pembeni"

Unamaliza, anaitwa binti akuingize kwenye chumba, unajua unaenda kuoshwa, lakini anakukalisha kwenye kiti.
"Nikufanyie skrabu"
"Hapana, labda siku nyingine"
"Inaonekana hujafanya skrabu siku nyingi. Hapa tuna skrabu ya coffee, ni nzuri sana. Ngoja ujaribu leo. Halafu nakuweka na chumvi."

Unatulia.
"Nikimaliza nitakupaka asali kwa dakika 10 kisha nakuosha"
"Inasaidia nini?"
"Uso wako una mafuta sana, sasa asali inasaidia kuondoa mafuta na chunusi"

Anakuminyaminya pale weee, kisha asali twiii. Halafu unasikia,
"Sasa hapa inatakiwa ukae kwenye stima kwa dakika kama kumi na tano hivi"
"Hiyo ya nini tena?"
"Inafanya uso wako uwe laini, na inaondoa makunyanzi"
"Okay"

"Pia tunafanya masaji ya kichwa, maana naona una mba kweli"
"Ohh"
"Pia tunaosha na miguu. Tunakata kucha"
"Ahhh, hiyo tutafanya siku nyingine"

Unamwachia uso na kichwa, anakuminyaminya mabega, unamaliza anakuosha, anakupaka tulosheni usoni, tumafuta kichwani anakupulizia na kale kasprei.

Anajipukuta, unauliza bei.
Anakusimamia mbele kama anataka kuanguka na tule tumatege, anaongea kama jambo la kawaida vile,
"Elfu sitini"

Mwenyewe ulipanga unyoe ndefu na kuchonga kwa elfu tano.

NB:
*Msisahau kuhakikisha kama majina yenu yamo kwenye daftari la wapiga kura.*
Nilikutana nayo jijini Mwanza hii trick, naona imesambaa nchi nzima, sio Dar tu. Nilikataa massage na scrub kwa sababu binafsi
 
Nimecheka sana walai[emoji3][emoji3][emoji3] hii ilinikuta mimi na niliambiwa nilipe elfu 20 yani kunyoa, wakaniambia scrub na kukata kucha... Ila niligoma nikatoa elfu 10... Alafu sasa achana na mitego yao aisee yani kaingiza cotton sikioni alafu anaizungusha taratibu na kitako chake mara apite aniguse guse nikamwambia siunaona pete kidoleni aisee nimeoa fanya fasta nisepe!!! Aaah aliosha kwa hasira ile mbaya
 
Natamani kuonja hiyo raha ya kushikwa kichwa pesa makaratasi tu
 
"Karibu brother"
"Asante, nataka kunyoa ndefu tu na kupunguza hizi za pembeni"

Unamaliza, anaitwa binti akuingize kwenye chumba, unajua unaenda kuoshwa, lakini anakukalisha kwenye kiti.
"Nikufanyie skrabu"
"Hapana, labda siku nyingine"
"Inaonekana hujafanya skrabu siku nyingi. Hapa tuna skrabu ya coffee, ni nzuri sana. Ngoja ujaribu leo. Halafu nakuweka na chumvi."

Unatulia.
"Nikimaliza nitakupaka asali kwa dakika 10 kisha nakuosha"
"Inasaidia nini?"
"Uso wako una mafuta sana, sasa asali inasaidia kuondoa mafuta na chunusi"

Anakuminyaminya pale weee, kisha asali twiii. Halafu unasikia,
"Sasa hapa inatakiwa ukae kwenye stima kwa dakika kama kumi na tano hivi"
"Hiyo ya nini tena?"
"Inafanya uso wako uwe laini, na inaondoa makunyanzi"
"Okay"

"Pia tunafanya masaji ya kichwa, maana naona una mba kweli"
"Ohh"
"Pia tunaosha na miguu. Tunakata kucha"
"Ahhh, hiyo tutafanya siku nyingine"

Unamwachia uso na kichwa, anakuminyaminya mabega, unamaliza anakuosha, anakupaka tulosheni usoni, tumafuta kichwani anakupulizia na kale kasprei.

Anajipukuta, unauliza bei.
Anakusimamia mbele kama anataka kuanguka na tule tumatege, anaongea kama jambo la kawaida vile,
"Elfu sitini"

Mwenyewe ulipanga unyoe ndefu na kuchonga kwa elfu tano.

NB:
*Msisahau kuhakikisha kama majina yenu yamo kwenye daftari la wapiga kura.*
Haya umeyajua leo?
Sio Sinza pekee
 
Popote palipoandikwa "Blaah Blaah Barbershop" huwa siingii. Tena nyingi zina vinyozi wanaoshindwa na wale wa "NiYeye Haircutting Saloon.

Na kwa tuliooa kwenda hizo barbershop ni mwanzo wa kuchepuka.
Unforgetable
 
Hakuna value for money.

Labda ufanye mara moja kwa miezi mitatu.

Nunua scrub, mkeo/demu wako atakufanyia.

Kucha kata mwenyewe, miguu osha mwenyewe.

Nunua dawa ya mba uitumie nyumbani kwako.

Utaokoa vingi sana.
 
Kuna ki saloon kipo Bariadi kwa wenyeji kipo karibu na NCHUBI.Ni wapumbavu sana eti kila scrub ina bei yake inaanzia alfu3 hadi alfu 20.Dada anaekufanyia scrub kakomaa mikono kwa kukata michembe halafu anajifanya kuongea lafudhi ya pwani ili kuondosha ile lafudhi yake ya kisukuma basi nilikuwa nacheka sana.Nawaambia hayo mnataka kunifanyia mke wangu anayaweza yote kasoro kunyoa kichwa chenye macho mawili ndo hawezi.
 
[emoji16][emoji16][emoji16] alikufanyia nini madame
Acha tu, usingizi wangu karudi kama jana mwaka hayupo, tunafika humo turekebishe kichwa na ndevu, sasa kule kuingia huko kumfuta nywele, kaanza ohoo sijui nini nami naingia nilimuwakia kama mwewe .
 
Wewe kila kitu unasema sawa, weka, fanya halafu bili mwishoni unataka kuikimbia
 
Back
Top Bottom