Kuwa makini na Apps za Mikopo

Kuwa makini na Apps za Mikopo

Hao pesa x nimewakopa jana 12,000, ngoja niwakope na hao cashx
Hauwezi kupata, kwa sababu ni wale wale.

Hilo la kwanza, la pili ni kuwa kitendo cha kudownload app yao tayari umeshawachangia.

Kwa mfano ukidownload app ukaanza kuaply mkopo kisha wakakueleza umekosea masharti, hiyo app uliyodownload inaabort, lazima uifute kisha udownload upya hata kama ni mara10 ama zaidi unakataliwa lazima udownoad upya!

Kwanza nashangaa ulipataje mkopo!

Maana hata kama umepatia lazima wakukoseshe.

Na kama ulipata, basi ni kwa kuingiziwa kiwango kidogo sana ambacho haujaomba!

Hao ni matapeli kuliko hata Tianshi!
Wanaingiza pesa ndefu kwa kuuza app kitapeli pekee.

Wanavimajina vingi, mara PesaX, mara Umoja loan nk nk, lakini ni wale wale.

Na ukitaka kuamini nikisemacho, kosa mkopo PesaX, muda huo huo nenda kuomba Umoja loan, utakuta kwamba wanakutambua.

Ukiwakopa usiwalipe kufidia pesa wanayopora kwa wengine.

Kwanza nikupe hongera kwa kuwabahatisha hata kwa kidogo hicho walichojisahau kukukopesha!
 
Back
Top Bottom