Hungry investor
New Member
- Apr 12, 2018
- 1
- 0
Sina shaka hapo ulipo kuna watu wamekuzunguka kwa maana unahusiana nao kindugu,kiurafiki, ujirani wafanyakazi wenzio pia hata wafanyabiashara wenzako.Katika hao watu wanaokuzunguka wapo wenye mwenendo mzuri na wenye mwenendo mbaya pia.
Asilimia kubwa ya mambo tunayoyafanya ni kwa sababu ya watu tuliwahi kuwanao karibu.Hata hicho unachofanya ni kwa sababu uliona mahali au ulishaona ndugu ama rafiki akifanya,haijarishi ni kizuri au kibaya. Unauza nguo kwa sabab ya aina ya watu uliozungukwa nao, unauza kahawa kwa sababu ya watu uliokutana nao. Inawezekana hukuwahi kuwaza katika maisha yako kuwa utafanya kitu cha namna hiyo ila umejikuta unafanya.
Anayevuta bangi hakuanza tu kuvuta hivi hivi lazima Kuna watu alikutana nao taratibu taratibu akaanza kujifunza hatimaye nae ni mwalimu Katika Hilo eneo. Ili Kutoka kule anahitaji aina ya watu wengine tofauti na anaohusiana nao sasa hivi na neema ya MUNGU pia inahitajika kufanya aondokane na hamu ya bangi.
Kwa hiyo ni muhimu Sana kuwawaangalifu sana na watu wanaotuzunguka kwan wanayo nafasi ya kutupeleka mbele au nyuma endapo tutawapa nafasi hiyo. Yaani Kuna namna unaweza kuitengeneza badae yako ikawa nzuri au mbaya. Maana yake Kama tunataka mawazo mapya tunahitaji pia kukutana watu wapya.
Ukikaa Sana na wanaofanya biashara ya maduka utaanza kuelewa kuhusu hiyo biashara hata kama hutafanya ila Kuna namna fulani utakuwa umepata vitu vinavyohusiana na biashara hiyo. Ni sawa pia Katika kilimo, elimu,siasa na nyanja nyingine zote. Ingawaje unaweza kupata mawazo mwenyewe kwa tafakar ya muda mrefu kitu ambacho nitakizungumzia wakati mwingine panapo majaliwa lakini asilimia kubwa ya mawazo tuliyonayo ni watuzungukao na yatuzungukayo.
Mwisho nikuulize msomaji wangu mpendwa, tabia mbaya au nzuri uliowahi kufanya ulijifunza kwa nan? Unatushaurije na sisi? Kazi unayoifanya unaipenda? Nan alikupa wazo Hilo?

Upvote
0