Kuwa makini sana ukifanya biashara na mtu aliyeficha Last seen na Read Receipts kwenye WhatsApp

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
56,205
Reaction score
79,515
Umuofia Kwenu wana JF,

Kwa uchunguzi na utafiti nilioufanya,wengi wa watu walioficha Last seen na Read receipts kwenye whatsapp wana makandokando katika mishe wanazofanya...Ukitaka kujua mtu kama ni wa magumashi angalia whatsapp ,kama kaficha last seen na read receipts kuna kitu anakimbia.

Kama unafanya biashara na mtu mkapeana namba kama ana whatsapp angalia LS na RR ,ukikuta zimefichwa basi cheza naye kwa tahadhari.

Kwanini wanaficha last seen na read receipt? Kwanza hataki maswali ya nimekutumia ujumbe whatsapp mbona haujajibu? Pili akificha last seen hauwezi kujua kama alikuwa online muda gani,hivyo ni rahisi kukupiga tantalila.

Kuwa makini sana na watu wanaoficha last seen na read receipts hasa kwenye kufanya nao biashara ,(Baadhi)most of them uaminifu ni zero!

GUMASHI.png

Minjingu.
 
Kuna ukweli kiasi fulani
Kabisa wengi ambao nafanya nao bizness za mkaa huku minjingu ,wasumbufu wote wameficha RR na LS!! Ni ukweli 100% ukifanya bizness na mtu ukiona kaficha RR na LS tambua hapo kuna "TANTALILA".
 
Nimeficha zote hizo mpaka status na dp yangu nimeruhusu watu wachache tu kuona,, naona ni maamuzi binafsi tu ndo maana wenye app yao hiyo wakaweka hayo machaguo
 
Hii tupo pamoja mimi mpaka ku view status kuna wengine hawawezi kabisa, sema kwenye option ya kuficha dp ionekane kwa wachache ninaowataka mimi hii ndio imenishinda mkuu nipe maujanja.
 
Kwenye settings nenda privacy, halafu utaona options za dp, status nk, ingia dp chagua ionwe na contacts wako tu maana yake ni kwamba km hutaki mtu aone dp Basi hakuna kusave namba yake ktk simu yako. Au chagua nobody na hakuna yeyote ataona dp yako kwisha habari
 
Umuofia Kwenu wana JF,

Kwa uchunguzi na utafiti nilioufanya,wengi wa watu walioficha Last seen na Read receipts kwenye whatsapp wana makandokando katika mishe wanazofanya...Ukitaka kujua mtu kama ni wa magumashi angalia whatsapp ,kama kaficha last seen na read receipts kuna kitu anakimbia.

Kama unafanya biashara na mtu mkapeana namba kama ana whatsapp angalia LS na RR ,ukikuta zimefichwa basi cheza naye kwa tahadhari.

Kwanini wanaficha last seen na read receipt? Kwanza hataki maswali ya nimekutumia ujumbe whatsapp mbona haujajibu? Pili akificha last seen hauwezi kujua kama alikuwa online muda gani,hivyo ni rahisi kukupiga tantalila.

Kuwa makini sana na watu wanaoficha last seen na read receipts hasa kwenye kufanya nao biashara ,(Baadhi)most of them uaminifu ni zero!

View attachment 1624825

Minjingu.
Aisee upo sahihi kabisa mimi wiki mbili zilizopita nimetapelewa elfu 30,na jamaa mmoja hivi eti wanajiita mikopo rahisi kwa kifupi wana matangazo mengi Instagram. Ndipo nikastest kama kukopa laki moja aisee akasema nitume taarifa whatsup. Ili atume form nijaze ila sharti nitume 30,000tsh ya ada ya form.nimetuma tu kaniblock kote.Ni nikapiga simu halopesa ili wamfuatilie huyo tapeli naambiwa ashatoa pesa yote. Nikasema no sweat leo nami nimekuwa mjinga.Ila ushauri wangu ukiona matangazo ya insta sijui mikopo rahisi ni matapeli wakubwa.
 
Ulipigwa kizembe sana 😃😃😃😃
 
Ulipigwa kizembe sana 😃😃😃😃
Sawa mimi nimepigwa kizembe, ila sitaki yaliyonikuta yamkute mwingine.ingia Instagram search mikopo rahisi.Ndo utamjua huyo jamaa tapeli.Nilipost uzi jf moderators wakaufuta sijui kwanini? Kutoa tahadhali zidi ya huyo jamaa
 
Back
Top Bottom