Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Nafikiri kuna umuhimu wa kubadili sheria na kuweka sheria mpya kuwa Mbunge wa eneo Fulani asiongoze eneo hilo Kwa zaidi ya Miaka Kumi. Awamu Mbili zinatosha Kabisa kuwakilisha wananchi wa Jimbo Husika.
Sioni tija ya Mbunge kukaa Miaka nenda rudi. Kama nia ni kuwakilisha Wananchi Vizuri Miaka Kumi inatosha Kabisa.
Kwa upande wa Mawaziri, ni Vizuri Mawaziri wasitokane na Wabunge labda Waziri Mkuu pekee ndiye anaweza akatokana na wabunge kama mwakilishi wa mhimili Serikali ndani ya Mhimili wa Bunge.
Mbunge kuwa papohapo Waziri ni kuwakosea Wananchi wa Jimbo husika na kumweka Mbunge huyo katikati asijue awawakilishe wananchi au serikali. Na kikawaida binadamu hupendelea kumwakilisha mwenye nguvu.
Lakini pia itaondoa uchawa Kwa wabunge wanaotaka kujipendekeza Kwa Serikali ili wapate teuzi za Hapa na pale kama vile Uwaziri.
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.