Kuwa Mbunge kwenye eneo moja isizidi miaka 10 na Mawaziri wasitokane na Wabunge isipokuwa Waziri Mkuu

Serikali kuu ndiyo msimamizi wa shughuli za kila siku za serikali kupitia Waziri mkuu,so inatakiwa kuongozwa na Wananchi,hivyo rais na mawaziri kupitia uwakilishi,bunge kutunga sheria kwa niaba ya Wananchi, mahakama kutafsiri sheria zilizotungwa na bunge
 
Baraza la mawaziri likiongozwa na Rais ni uwakilishi wa wananchi katika kufanya maamuzi mazito ya kinchi,kutaka Waziri asitokane na mbunge maana yake hutaki uwakilishi wa wananchi juu ya mustakabali wa nchi yao, rejea maana ya demokrasia
Kwani hao mawaziri SI watakuwa miongoni mwa watanzania?? Unafahamu nchi hii Ina mihimili mitatu ambayo haitakiwi kuingiliana kabisa?? Mhimili wa bunge, serikali na mahakama havitakiwi kuingiliana..Sasa vipi mtendaji wa serikali ambayo ni mhimili mmoja atokee kwenye ubunge ambao ni mhimili mwingine ambao kazi yake ni kutunga SHERIA na kuishauri na kuisimamia serikali??
 
Mtu akiwa katibu mkuu Simba na mkurugenzi rasilimali watu nssf,hapo Simba na nssf zimeingiliana?
 
Mbunge wa kuchaguliwa kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki, hata akihudumu miaka 25 ni sawa tu, mradi atumikie aliyotumwa na wananchi wake vizuri.

Basi hata hiyo itumike Kwa Rais. Muhimu uchaguzi huru na wahaki na atumikie wananchi wake Vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…