Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi ni kazi sana

Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi ni kazi sana

ranjan

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
338
Reaction score
288
Pledges za michango yote ni milioni 18, harusi ni mwezi huu wa tatu mwishoni, hadi muda huu watu wachache wametoa, cash iliyopo ni milioni moja kasoro. Bwana Harusi kachanganyikiwa kaniachia mipango yote nipange mimi, nafanyaje?

Bwana Harusi aliahidi kutoa milioni tano lakini katoa laki tano tu, nyingine hajatoa, anamtaka MC Garab wakati uwezo hana, yaani ni kama ndugu wamemsusia, simu hawapokei, nimemshauri asifanye sherehe ni kama haelewi, sijui itakuwaje.
 
Tafuta mkeka, unga wa ngano kilo 15, mchele kilo 50 na nyama kilo 25 alafu vunga anza kutembea na chupa ya maji kubwa akikuuliza kila kitu kipo sawa? Kohoa kdogo fungua maji kunywa funda moja alaf muonyeshe ishara ya kutulia kwa mkono.
 
Ujinga mwambie bwana harusi achanganyikiwe mpaka atembee uchi, ka pledge 5M katoa laki5, anataka mambo makubwa asiyo na uwezo nayo

Alitangaza hivyo mwisho wa siku zawadi ingetokea kwenye hela aliyojitangazia, angesema tiyari kawekewa kwenye account, fool!

Aende kanisani akitoka hiyo laki5, aende fungate na mkewe siku 2, wakirudi, maisha yaendelee.

Atakoma kama anaoa wadada wa Instagram.

Everyday is Saturday................................😎
 
Pledges za michango yote ni milioni 18, harusi ni mwezi huu wa tatu mwishoni, hadi muda huu watu wachache wametoa, cash iliyopo ni milioni moja kasoro. Bwana harusi kachanganyikiwa kaniachia mipango yote nipange mimi, nafanyaje?

Beans harusi aliahidi kutoa milioni tano lakini katoa laki tano tu, nyingine hajatoa, anamtaka MC Garab wakati uwezo hana, yaani nikama ndugu wamemsusia, simu hawapokei, nimemshauri asifanye sherehe ni kama haelewi, sijui itakuwaje.
Bwana harusi amehaidi kumalizia michango lini? Unaweza kuwashauri wapeleke harusi mbele, au la wafanye sherehe ndogo ya kishikaji, hakuna atakayewalaumu.

Binafsi nilikuwaga sipendi makubwa kwenye harusi yangu, kilichotokea hakuna aliyekubali, kila mtu alinipinga, kila mtu.

Micahango ilichangwa, Vinywaji vililetwa vya kila aina, gharama za kamati zilikuwa kidogo sana, vitu vingi vilifanywa nje ya kamati na kamati ilibaki na cash, cash ikanirudia.
 
Back
Top Bottom