Kuwa mwizi, kahaba /Malaya Ni tabia ya mtu wala sio ugumu wa maisha

Wewe ni mwanamke ?
Kama siyo unawezaje kuelezea matamanio ya wanawake kwa kujiamini kiasi hicho ?
Mimi ni mwanaume mkuu..
Kama uamini tukutane live live alafu kwanza nitataka tupigane maana naona dharau wazi wazi..
.oky kuhusu kuelezea matamanio ni vile nafanya research nakumbuka mwaka wa mwisho namaliza chuo pale mlimani tulipewa kazi ya research ambayo nimefanya ndani ya miaka miwili.

Mkuu cha kuingezea tu ni kuwa unaongea na mwana saikolojia ambaye degree yangu nimemalizia udsm na kujiendeleza zaidi upande wa haki za mama na watoto ....kwa sasa nafanya kazi kama kaimu katibu chama cha wanawake tanzania..

Karibu sasa.. ..
 
Asante mtaalamu
 
Siku hizi watu hawaishi kwa tabia zao ila wanabadilika kulingana na maisha yanavyobadilika. Watu unaowaona wana maadili mema kimsingi wamekosa tu nafasi na uwezo wa kutenda maovu.
Kuna mambo hata life likuchape namna gani, uwe mazingira gani huwezi kubali kulifanya.
Wapo ambao kuua kwao ni dhambi na hawezi kuua ni kheri umuue yeye.
Ni misimamo tu mkuu.
 
Shuhuda za wanawake wazuri wenye misimamo ipo kibao tu, ila tu ni vile wazee wa excuses hawakosi visababu.

Kuna binti kamuuguza mumewe kwa almost miaka miwili na yeye (ke) ndo provider mkuu, watu wa nje walikua wakimshangaa kwa uzuri ule kwanini aendelee kubaki na jamaa maana hadi familia ya mchizi ilimtenga alibaki na mkewe tu.

Mpaka mume kaja kupata nafuu mke hakuonesha dalili zozote za utovu wa nidhamu wala umalaya.

Umalaya ni tabia, utaificha ila utaitafutia sababu tu.
 
Hao unaowaita mastar hawana chochote huoni wanaugua Malaria wanachangisha michango?!
Ni mfano tu ukisema hawana chochote unakosea wengi wao walao Wana uhakika wa kula. Hizo mbwembwe zote unazowaona nazo za kupalamia maisha ya juu ndo tamaa yenyewe kamwe wewe hata ukilala njaa huwezi fikiria Wala kuwaza ukajiuze au uingiliwe kinyume na maumbile eti ule au ununue simu huwezi kamwe iwapo utaweza tu hiyo ni tabia Yako na hata kama ungekuwa na Mali kiasi Gani Bado ungekuwa tu
 
Naungana nawewe mkuu. Mimi bro mwenyewe Huwa anatutambia kabisa Kwa kusema nitafanya ujinga wote lkn huyu mwanamke hakika ni WA kipekee sana.

Kwa Hali yoyote Ile mwanamke akikuambia eti anafanya umalaya Kwa ugumu wa maisha sio kweli ni tabia yake tu wangapi wamama wazuri wazuri tunawaona wanaponda kokoto na ni ma single mother?

Huwa sikubali na sababu yoyote.

Imagine jamaa aliyefukuzwa alikuwa anaiba copper wire anaweka kwenye viatu (safety boots) anakusanya akifikisha kilo ndo auze 15k na amefanya Kwa muda mrefu.

Mwingine nae alikuwa anaiba zile soldering wire (Sina hakika na spelling) mitaani zinajulikana kama risas hutumia mafundi wa electronics

Naye ilikuwa kazi yake pamoja na Kwamba analipwa zaidi ya m2
Kama sio tabia Yako huwezi kwanza utatetemeka mno
 
๐–๐š๐ง๐š๐ฌ๐ž๐ฆ๐š ๐ฎ๐ ๐ฎ๐ฆ๐ฎ ๐ง๐๐จ ๐ฎ๐ง๐š๐ฌ๐š๐›๐š๐›๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐ก๐š๐ฒ๐จ ๐ฒ๐จ๐ญ๐ž
 
Wizi ni tabia mkuu.

Nina mdogo wangu alikua anaiba vitu vya ajabuajabu kweli.
Mara mkipika kuku aibe paja, aibe maziwa mtindi, kuchomoa vichenji ndio usiseme.

Na sio kua hivyo vitu hapati, anapata sana tu, na ana watu kibao wakumpa hela kila akiomba, mpaka shangazi zake wakahisi ana "mapepo" ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ