Blessed Tajiri
Member
- Dec 16, 2023
- 57
- 82
Utangulizi
Ili mtu uweze kufanya mambo yako vizuri na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa unatakiwa kuwa na afya njema ya mwili na akili. Tanzania bado masuala ya afya ya akili hayajaeleweka vizuri na hata juhudi za serikali bado ni ndogo, japokuwa kwa sasa uelewa unaongezeka tofauti na zamani.
Hali ikoje kwa sasa
Miaka ya karibuni tumeshuhudia matukio ya kikatili na kusikitisha yakiongezeka kwa kasi, kuanzia watu kujitoa uhai ambapo hali imekuwa mbaya kwani hata watoto wamekuwa wakikatiza maisha yao, ukatili kwa wenza umeongezeka ambako wanaume ndio wanaongoza kuwafanyia ukatili wenza wao, bila kusahau ukatili kwa watoto. Kutokana na ripoti ya Haki za Binadamu 2023 iliyotolewa na LHRC kwa kushirikiana na ZAFAYCO matukio 50 ya ukatili kwa wenza (wanawake) yaliripotiwa ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022, 90% wakiwa wamefanyiwa ukatili pamoja na kuuawa, vitendo vya ukatili dhidi ya wanaume pia vimeongezeka kufikia 10%, pia kuna ongezeko la watu kujiua ambapo kwa mwaka 2023 matukio 57 yalirekodiwa, ikiwa ni ongezeko la matukio 35 ukilingisha na mwaka 2022 ambapo sehemu kubwa ya waliojiua ni wanaume ambao hasa ni vijana.
Kwa sasa kuna huduma ya bure ya simu (116) ya ushauri na kupokea matukio mbalimbali ya ukatili yanayowakumba watoto inayofanywa na taasisi ya C-SEMA kwa kushirikiana na Serikali, ambapo baada ya kubaini tatizo, kesi hupelekwa Ustawi wa Jamii au Polisi kuendelea na hatua nyinginezo kulingana na changamoto iliyowasilishwa, ambayo kwa kiasi fulani imepunguza matukio ya ukatili kwa watoto.
Upande wa watu wazima hakuna huduma hii lakini pia bado uelewa ni mdogo si tu kwa Serikali bali hata kwa wananchi. Bado kwa baadhi ya sehemu mtu akiwa na tatizo la afya ya akili anaonekana kalogwa, au ungonjwa kuonekana ni wa hadhi kubwa kuliko yeye, mtu akiomba msaada hasa kwa wanaume huishia kuchekwa na kukejeliwa kuwa wamelegea kama wanawake na kuhusishwa na vitendo vya ushoga, wengine hufanya mzaha kuwa mwenye tatizo anahitaji fimbo za kutosha ili aache ujinga, polisi wakati fulani baada ya tukio la mtu kujua alisema watu watoe taarifa polisi wakigundua kuna mtu anataka kujiua ili akamatwe (changamoto nyingine kwenye sheria yetu)! Yaani mtu anahitaji msaada wao wanatishia akamatwe! Japo kama nilivyotangulia kusema awali, sasa hivi hali kidogo imeimarika kuliko mwanzo, japokuwa kazi na juhudi kubwa bado zinahitajika kuboresha hali hii.
Sababu mbalimbali zinatajwa kusababisha matukio haya ikiwa ni pamoja na wivu wa mapenzi, changamoto za makuzi katika familia, Imani za kishirikina na changamoto za kukosa ajira. Si kwamba mambo haya yalikuwa hayatokei zamani, huenda hata yalikuwa kwa kiwango kikubwa kuliko sasa ila kwa kuwa sasa huduma za mawasiliano zimeboreka na mitandao ya kijamii kuanzishwa ikiwa na watumiaji wanaoongezeka kila siku, matukio yanatufikia wengi tofauti na zamani.
Kabla ya kufika kwenye huduma bure ya ushauri na msaada kwa njia ya simu, serikali inatakiwa kwanza kuitambua Saikolojia kama Kada rasmi kwenye mfumo wa ajira. Maisha yetu kwa asilimia kubwa yanaendeshwa na Saikolojia, Afya ya Akili ni sehemu katika Saikolojia. Kwasasa kuna Chama cha Wanasaikolojia nchini; Tanzanian Psychological Association (TAPA) ambacho kinafanya kazi mpaka Zanzibar na Zanzibar kuna Zanzibar Psychiatric Association (ZPA) ambao wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo za kitabibu kwa Zanzibar pekee. Hizi zote ni NGO ambazo zinafanya kazi kwa kutegemea michango (donations), juhudi zimefanyika kuishawishi serikali ili kada hii itambulike ramsi lakini bado hazijafua dafu, na hivyo kuzorotesha juhudi za kupunguza matatizo yanayotokana na saikolojia ikiwemo matatizo ya afya ya akili. Japokuwa wanatoa huduma kwa gharama nafuu bado huduma hizo ni ghali sana kwa wananchi.
Kutambua Saikolojia kama Kada rasmi kuna faida zifuatazo;
Wakati mchakato wa kuifanya Saikolojia kama Kada rasmi ukiendelea, huduma ya bure kwa ajili ya wananchi kupata ushauri wa masuala ya afya ya akili kwa njia ya simu inaweza kuanza na kuendelea kuboreshwa kadri siku zinavyoenda, ambapo Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Wanasaikolojia watapanga mfumo mzuri kwaajili ya huduma hii kutolewa na malipo kwa wanasaikolojia hao kutoa ushauri.
Jinsi huduma hii itakavyofanyika
Serikali kwa kushirikiana na Wanasaikolojia pamoja na Wadau watatakiwa kushirikiana kuhakikisha huduma hii inapatikana, ambapo namba za kutoa huduma zitagawanywa katika makundi 3;
Baadhi ya watu changamoto zao zitaishia katika hatua hii (kwenye ushauri), kwa ambao watahitaji uchunguzi zaidi pamoja na mpango wa matibabu wataelekezwa kwa daktari mahususi atakayeweza kutibu ugonjwa wake. Wakati bado mchakato unaendelea (kurasimisha kada) mgonjwa atatakiwa kugharamia matibabu yake, na kwa kesi ambazo zimefika hatua mbaya na mgonjwa hana uwezo wa kujigharamia serikali itatakiwa kugharamia matibabu hayo kuokoa maisha ya mgonjwa huyo.
Naamini hii ni njia bora (wadau, wasaikolojia na serikali inaweza kuboresha zaidi kutoka hapa) ya kukabiliana na changamoto zinazoletwa na matatizo ya afya ya akili na saikolojia kwa ujumla na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya ukatili yanayoendelea sasa.

- Gharama za matibabu zitapungua: Sasa, watu wengi hawawezi kumudu gharama za matibabu wanapopata changamoto, na kwa wanaomudu bado gharama ni kubwa sana. Kama itakuwa kada rasmi, serikali na wadau watashirikiana kutoa huduma na hivyo kupunguza mzigo kwa wananchi ambapo watu wengi watajitokeza kupata matibabu.
- Unyapapaa kupungua: Hii ni kwasababu watu wataelewa zaidi changamoto/magonjwa hayo baada ya kuwa serikali imetoa elimu ya kutosha. Imani za kishirikina zitapunguza pia kuhusishwa na matatizo haya, lakini pia fedheha (bullying) kwa watu wanaofunguka juu ya matatizo haya zitapungua.
- Matukio ya ukatili kupungua, hii ni kwasababu wagonjwa watakuwa wanapata msaada mapema.
- Kuwa na jamii yenye watu ambao afya ya akili imeimarika na hivyo kushiriki kikamilifu katika shughuli za kujenga taifa na maisha yao binafsi.
Wakati mchakato wa kuifanya Saikolojia kama Kada rasmi ukiendelea, huduma ya bure kwa ajili ya wananchi kupata ushauri wa masuala ya afya ya akili kwa njia ya simu inaweza kuanza na kuendelea kuboreshwa kadri siku zinavyoenda, ambapo Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Wanasaikolojia watapanga mfumo mzuri kwaajili ya huduma hii kutolewa na malipo kwa wanasaikolojia hao kutoa ushauri.
Jinsi huduma hii itakavyofanyika
Serikali kwa kushirikiana na Wanasaikolojia pamoja na Wadau watatakiwa kushirikiana kuhakikisha huduma hii inapatikana, ambapo namba za kutoa huduma zitagawanywa katika makundi 3;
- Huduma ya dharura kwa watu wanaotoka kujiua
- Huduma ya dharura kwa wanaopitia ukatili wa majumbani na unyanyasaji wa kijinsia
- Huduma kwaajili ya changamoto nyingine kama msongo wa mawazo, sonana, nk.

Upvote
6