Kuwa na wazo la kumiliki kiwanda

Kuwa na wazo la kumiliki kiwanda

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kama una kipato kiasi, na una ndoto ya kuja kumiliki kiwanda cha ukubwa wowote lakini hujui pa kuanzia; Jaribu kutembelea mitandao mbalimbali inayouza mashine, unaweza kuanza na alibaba na mingineyo. Kutazama tu mashine zilizopo, kuna wazo litakujia ufanye nini. Ila ukitazama bidhaa, unaweza kujikuta wewe ni mnunuzi wa bidhaa mpaka mwisho wa uhai wako.

Nb: Kama una uwezo wa kukopa benki laki mpaka mamilioni kwa jili ya kununua vitu vya anasa; kwanini usitumie fedha hizo kununua mashine/mitambo?
 
Kama una kipato kiasi, na una ndoto ya kuja kumiliki kiwanda cha ukubwa wowote lakini hujui pa kuanzia; Jaribu kutembelea mitandao mbalimbali inayouza mashine, unaweza kuanza na alibaba na mingineyo. Kutazama tu mashine zilizopo, kuna wazo litakujia ufanye nini. Ila ukitazama bidhaa, unaweza kujikuta wewe ni mnunuzi wa bidhaa mpaka mwisho wa uhai wako.
Kipato cha kiasi!!? Kiwanda cha ukubwa wowote pita mitandao mbalimbali??

Ok naona siku umekuwa motivesheno spika ila unaweza japo mawe yako hayajitoshelezi anyway mkumbushe na kupita pita mtaani pia

Amani iwe nawe.
 
Nina Wazo la kutengeneza counter books kwa ajili ya wanafunzi

Nishamaliza design

Naitaj kuanza kufwatilia JINSI gan ya kufanya Printing na biashara ikoje ya upande wa kuuza counter kwa wanafunz

Plan ni kuanza kuuza kuanzia 9/2022,

Ushaur wowote juu ya hii Wazo mkuu
 
Usipende kufikiria 'negative'
  • Kuna mashine na mitambo ya kila namna, kuanzia laki mpaka mamilioni
  • Wapo wanaokopa benki na kununua magari ya misele, ingawa wangeweza kununua mashine na kuwekeza
  • Wapo watu walioamka na wanatekeleza
  • Mashine za juisi zipo, za kutengeneza mabati zipo, za misumari zipo n.k
 
Wazo zuri mkuu, Mashine pamoja na vitendea kazi ulishanunua?
 
Kumbe unazungumzia vile viwanda vya mwenda zake at vyerehani ni kiwanda Apo sawa sina tatizo na wewe.
 
Wazo zuri mkuu, Mashine pamoja na vitendea kazi ulishanunua?
Bado mkuu... kwa sasa nmewaza tu kuanzia sehem kama jamana au fiveStar

Kujua gharama zao Za kutengeneza counter..

Sasa kwa sababu sinaufaham wa kutosha nkaona nliweke apa ...ili kuongeza Maarfa kdogo
 
Ni kweli sikuhizi kiwanda sio lazima uwe na jengo kubwa kama mabanda ya Mr.Kuku unaweza ukanunua mashine zako zikawepo ndani ya nyumba ya room 3 tu ukawa na production, office na stoo ya kuhifadhia mzigo na malighafi!
 
Gharama si kubwa sana; kwa anayeanza, piga hesabu ya malighafi pamoja na bei ya kuuza bidhaa sokoni hasa kuwashinda hao washindani, kama iko sawa; anza kuagiza mashine
 
Ni kweli mkuu, na wenzetu ndio wanafanya hivyo
 
Nina Wazo la kutengeneza counter books kwa ajili ya wanafunzi

Nishamaliza design

Naitaj kuanza kufwatilia JINSI gan ya kufanya Printing na biashara ikoje ya upande wa kuuza counter kwa wanafunz

Plan ni kuanza kuuza kuanzia 9/2022,

Ushaur wowote juu ya hii Wazo mkuu
Anzia Sokoni. Fanya Market Study ya kina.

Angalia hivi vifuatavyo.

1. Soko lipoje kwa sasa kwa maana Market Value of exercise books and stationaries at large

2. Nani ni washindani wako, unaweza kujua kiasi gani wanauza kwa mwaka?

3. Distribution Channel ipo ya hao washindani, je wewe utakuwa na distribution channel ipi?

4. Gharama za machine? Je ni lazima uanze na mashine?

5. Utahitaji wafanyakazi kiasi gani? Gharama ipoje?

6. Malighafi ya kutengenezea counter je?

7. Sheria zinasemaje?

8. Mengi na mengine mengi. Kwa leo anzia hapo
 
Gharama si kubwa sana; kwa anayeanza, piga hesabu ya malighafi pamoja na bei ya kuuza bidhaa sokoni hasa kuwashinda hao washindani, kama iko sawa; anza kuagiza mashine
Gharama ni kubwa sana, sana tena sana. Huwezi shindana na mtu mwenye output ya units 10,0000 kwenye kakibanda kako ka kutoa units 200. Someni hata PESTEL/PESTLE Analysis na SWOT/C Analysis ambayo hata Diploma wanasoma. Ukiichambua vizuri utajua ugumu wa kushindana kibiashara ukiwa mgeni.

Unless kama gharama unazosema ni capital peke yake. Kwenye biashara haizingatiwi capital tu kuna vitu kama cost of production ni muhimu sana kwani ndio vitaamua bei yako ya faida
 
Anzia Sokoni. Fanya Market Study ya kina.

Angalia hivi vifuatavyo.

1. Soko lipoje kwa sasa kwa maana Market Value of exercise books and stationaries at large

2. Nani ni washindani wako, unaweza kujua kiasi gani wanauza kwa mwaka?

3. Distribution Channel ipo ya hao washindani, je wewe utakuwa na distribution channel ipi?

4. Gharama za machine? Je ni lazima uanze na mashine?

5. Utahitaji wafanyakazi kiasi gani? Gharama ipoje?

6. Malighafi ya kutengenezea counter je?

7. Sheria zinasemaje?

8. Mengi na mengine mengi. Kwa leo anzia hapo
Shukran sana mkuu
.. nazfanyie kaz hizi...
 
Pagumu hapa naona ni garama za mashine tu, kuhusu soko lipo, ila changamoto ni bei atakayoileta sokoni ili kuwapiku washindani
 
Gharama ni kubwa sana, sana tena sana. Huwezi shindana na mtu mwenye output ya units 10,0000 kwenye kakibanda kako ka kutoa units 200. Someni hata PESTEL/PESTLE Analysis na SWOT/C Analysis ambayo hata Diploma wanasoma. Ukiichambua vizuri utajua ugumu wa kushindana kibiashara ukiwa mgeni.

Unless kama gharama unazosema ni capital peke yake. Kwenye biashara haizingatiwi capital tu kuna vitu kama cost of production ni muhimu sana kwani ndio vitaamua bei yako ya faida
Ni kweli, gharama ya uzalishaji ndio itakayompa bei ya kuuza sokoni; anachotakiwa kufanya ni kutathmini gharama za uzalishaji
 
Pagumu hapa naona ni garama za mashine tu, kuhusu soko lipo, ila changamoto ni bei atakayoileta sokoni ili kuwapiku washindani
Unaweza kuona soko lipo kwa sababu waliopo wanauza. Unajuaje labda wanauza kwa credit(mali kauli)? Je yeye ataweza kuuza bidhaa kwa kuanza kwa mali kauli? Na kwa muda gani?

Hatakiwi kuruka principles za biashara hata moja. Kufanya hivyo ndio kuna pelekea biashara nyingi kufeli.

Njia pekee ya kujua kama soko lipo au halipo aende kwa manufacturer na anunua kiasi kidogo aanze kutafuta masoko na kuuza kabla ya kuwa na kiwanda.
 
Ni kweli, gharama ya uzalishaji ndio itakayompa bei ya kuuza sokoni; anachotakiwa kufanya ni kutathmini gharama za uzalishaji
Boss ndio bado narudi pale pale, aangalie soko kwanza. Kuna counter book zinauzwa 6000-10000 na watu wananunua. Hivyo anaweza kuzalishwa bei ikawa tofauti na hizi nyingine lakini akauza kwa sababu kuna soko linahitaji hizo counter books.
 
Kuna kitu kinaitwa 'massive production' unakuwa unazalisha kwa wingi kwa gharama zako, wakati huo idara ya masoko inafanya kazi yake, ndivyo wanavyofanya kwenye viwanda, huwa hawazalishi kwa order maalumu, bali wao wanazalisha kwa sababu bidhaa inahitajika na idara ya masoko itafanya kazi. Kwa huyu anayeanza anatakiwa atathmini uwezo wake wa kuzalisha pamoja na bei ya sokoni ulioianisha hapo juu 6000-10,000
 
Back
Top Bottom