Kuwa sehemu ya historia ya katiba mpya kwa kuweka maoni yako hapa

Hapa umeweka mawazo yako ambayo yanainesha wazi chuki ulizonazo kwa wabunge ungejikita kwenye Mambo ambayo yanamgusa mojakwamoja mtanzania siyo kwanini mbunge apate hiki huyu apate kile hayo ni mawazo ya wivu jikiye kwenye maslahi ya mtanzania hapo sijaona point kabisa
 
Bunge bora lazima haya yawepo:
1. Rais akitoka chama A spika lazima atoke chama B.
2. Mawaziri wasiwe Wabunge.
Hii itakuwa ngumu maana chama B kwamfano kwa sasa hakuna wamesusa waliobaki hawawezi kugombea uspika wakashinda maana wako wachache katiba ielekeze chama Cha siasa kikisusa kifutwe
 
Haimaanishi kama wewe hujaona point basi iwe ni pointless.. Haya ni yangu mimi nawe jitahidi uweke ya kwako.. Ukosoaji wako hautabadili hata nukta wa kile nilichoandika
 
Umeweka fumbo hakuna mtu atajuwa ulikuwa na maana Gani hayo mazingira ni yapi?
 
Tuwe na katiba ambayo Kila mtu yupo chini ya sheria kuepusha haya tunayoyaona Sasa[emoji1545]
Mtu anakuambia anafuata katiba kwa maneno lakini kiuhalisia hafanyi kwakuwa Yuko madarakani utafanyaje? Cha msingi kiangaliwe kitu kinachochochea uchumi na kuahusha garama za maisha basi katiba ni siasa na siasa ni mchezo mchafu Kenya unasifia wanakatiba mpya inawasaidia nini?
 
Haimaanishi kama wewe hujaona point basi iwe ni pointless.. Haya ni yangu mimi nawe jitahidi uweke ya kwako.. Ukosoaji wako hautabadili hata nukta wa kile nilichoandika
Utakuwa bado hujawaelemisha watu juu ya nini unakitaka zaidi utaonekana mchochezi
 
hakuna haja ya kuanza kupoteza pesa kwenye kutengeneza katiba nyingie, ile ya warioba ilikuwa hela za kutosha, wachukue tu ile webandike tuanze kuitumia. ni nzuri na inatibu maswali mengi.
 
Wazo murua kabisa na hapa ni mahali pake sahihi kwa kila raia
 
Nadhani hujaelewa ama hujui nini maana ya KATIBA..! Ndugu SINGLE WINDOW katiba sio siasa .. Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Utakuwa bado hujawaelemisha watu juu ya nini unakitaka zaidi utaonekana mchochezi
Siko hapa kumuelewesha yoyote bali kila mmoja awe sehemu ya katiba mpya kwa ajili ya kuweka mawazo yake hapa..hebu rudi mada kuu usome muktadha wake tafadhali
 
Point safi lakini sasa likishavunjwa lipangweje? Wamo humu wanasima ilikujuwa raia wanamaoni Gani liweje unavyofikiri ukisema livunjwe tu bado hujaeleweka
Katiba mpya haitengenezwi na polisi bali na wananchi wote kupitia wawakilishi wao kwenye makundi mbali mbali ndani ya jamii
 
Lakini jamani hizi zingine zitakuwa ni ndoto hakuna katiba itakayokuja kuweka usawa kati ya mpiga kura wa kwa mtogole na mwanasiasa wa masaki never hebu tuangalie vya maana
Tabaka ziko kwenye jamii lakini zisisababishwe na ukwasi wa kisiasa.. Wala siasa isiwe uchochoro wa kujipatia utajiri
 

Hivi majuzi nilitakiwa na DW nitoe maoni kuhusu miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania tangu 1992. Ni suala ambalo naulizwa mara nyingi ila majibu yangu hayazingatiwi au hupuuzwa, pamoja na ukweli au uhalisia wa hoja zangu.

Ukweli na/au uhalisia ni kwamba Tanzania haina mfumo wa vyama vingi vya siasa na haujawahi kuwepo tangu hiyo 1992. Ila tuna "mfumo wa chama kimoja cha siasa" wenye vyama vingi vya siasa. Vyama vyote vimo ndani ya mfumo wa chama kimoja! Hata katiba inayotumika sasa ni ile iliyoundwa na chama kimoja 1977

Kipengele kinachoruhusu vyama vingi vya siasa kilichomekwa tu ndani ya katiba ya chama kimoja kinachotamalaki kila pembe. Hata serikali huitwa ya CCM, si taasisi ya umma!

CCM ni chama dola na kinadumu kwa kutegemea zaidi dola. Tunahitaji tuwe na katiba mpya inayoweka mfumo, mazingira au uwanja sawa wa vyama vingi vya siasa.

Nahitimisha kwa kusema tena katiba mpya ije sasa itakayokidhi na kutoa haki kwa wote, pamoja na vyama vingi vya siasa.
 
CCM ni chama dola na kinadumu kwa kutegemea zaidi dola. Tunahitaji tuwe na katiba mpya inayoweka mfumo, mazingira au uwanja sawa wa vyama vingi vya siasa.

Nahitimisha kwa kusema tena katiba mpya ije sasa itakayokidhi na kutoa haki kwa wote, pamoja na vyama vingi vya siasa.[emoji1545][emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…