Kwahiyo, Kodi inatumika kwenye mikopo tu?, Vipi kuhusu ulinzi na usalama?, Barabara, huduma za jamii, mitihani, nk.
Mikopo ya elimu ya juu haiwezekani kupewa wote na katika nchi yoyote mwenye nacho anatozwa Kodi kubwa ili kumsaidia masikini. Mikopo ya elimu ya juu imewekwa kwa ajili ya masikini (Si kila anayesoma Shule za umma ni masikini). Rejea wanafunzi wanaosoma TABORA GIRLS na Boys, Mzumbe, Kibaha, MSALATO, Kilakala, Ilboru, nk( hawa baadhi Yao wana uwezo, lakini wanatafuta STATUS). Ila SECONDARY za kata na zile zisizokuwa na majina wengi wao ni masikini.
Na pia wako masikini waliofadhiliwa tu kwenye Shule za private lakini wazazi wao ni masikini. Kwahiyo, kigezo cha kusoma Shule fulani siyo sahihi sana ila ni Kigezo kizuri zaidi (tusije tukawakosesha mikopo wanaostahili).