Kuwafananisha Wachaga na Wakinga ni dalili ya kuchelewa kuijua Dunia

Kwenye madini mchagga hatumuoni. Ni ngosha kwa kwenda mbele. Njoo kwenye uvuvi mchagga hayupo leo anatuambia eti yuko kila mahali. Sasa wachagga wamebanwa mpaka hoteli kubwa ngurudoto zinageuzwa hosteli. Kwadanganye wachagga wenzio.
Fursa ya uvuvi kama hukuzaliwa kando ya bahari, ziwa, bwawa, mito mikubwa kama Ruvu,Rufiji, kilombero, Malagarasi, Ruvuma, Kagera. Mchaga na maji ni mbingu na ardhi na pombe zao zile watafia majini. Wachaga walitangulia ila makabila mengine yana catch up.Sukuma ndio kabila litakalotawala miongo ijayo kwa wingi wao, hasa katika sekta za elimu.

Katika kilimo Sukuma ndio konki kwa hiii nchi.Nakumbuka miaka ya 90+ Pale NMC SHY walikuwa wanakosa eneo la kutunza mazao mpaka wanapeleka uwnja wa kambarage.Zile zama sitazisahau, laana ya msukuma ni kuharibu mazingira hata hivyo msukuma kahamia kila eneo lenye fursa ya kilimo hapa TZ.
 
Hii ni kampuni ya Mkinga huko China. Wachaga acheni kujidai Sana akati kuna watu kama hawa
 
Siyo kweli kwa sasa wakinga wapo juu kibiashara kuliko wachaga, nenda kariakoo kawafananishe wakinga na wachaga utaona mchaga kafeli, wakinga kwa sasa wapo vizuri kwa Elimu na biashara
 
Hawajatembea wapi?

Matajiri wa nchi hii tunawajua wachaga, sasa wewe sijui umetembea wapi huko wasipowajua hao jamaa

Wachaga wanaongoza Karibu kila biashara kubwa uijuayo...
Mimi nimetembea karibia mikoa yote ya Tz, Wakinga
Kwanza ni makosa kufananisha Wachaga(Muunganiko wa kabila la Wamarangu,Warombo,Wamachame,Wakibosho nk) na Wakinga,Unawezaje kufananisha Muunganiko wa makabila na kabila moja tu? nimekaa maeneo mengi ya Uchagani lile sio kabila moja bali ni makabila kadhaa yanayozunguka mlima Kilimanjaro hata Lugha wanazoongea ni tofauti.

Tukirudi kwenye mada,hakuna kabila lolote Tz hii linaloweza kushindana na Wakinga kwenye biashara kuanzia maduka ya jumla mpaka rejareja,Mahotel makubwa mpaka guest house, Usafirishaji wa barabarani,biashara ya Mbao,nk,..wale jamaa wapo mbali sana kwa sasa,kwa kiasi kikubwa wameshikilia uchumi wa nchi baada ya Wahindi na Waarabu. Baada ya Wakinga,ndipo wanafuata Wamachame,Warombo, Wabena, Wahaya, Wanyakyusa, WaSukuma,Wapare,Sambaa nk.
 
Sasa wewe jamaa mbona unajinasibu kwenye uzi wako wa leo ambao umeenda kumtolea mahari nduguyo ukidai wewe ni mchaga.

Hii jf bhana ni vile tu hatuonani bhasi mtu anakaaa nyuma ya keyboard na kuanza kuandika kile anachojisikia
 
Siyo kweli kwa sasa wakinga wapo juu kibiashara kuliko wachaga, nenda kariakoo kawafananishe wakinga na wachaga utaona mchaga kafeli, wakinga kwa sasa wapo vizuri kwa Elimu na biashara
Alietangulia katangulia bwana mdogo
 
Hizi ni pumba umeeendika

Kutofautiana katika kichaga kinachozungumzwa na wamarangu au warombo haimaaanishi kwamba kabila la kichaga ni muuunganiko wa makabila mengi kama unavyozungumza wewe

Wewe Mwenyewe sio mchaga sasa inakuaje utoe description ya kabila ambalo sio lako
 
nitakupinga kwa fact moja tuuu: angalia waarab
 
Nimekaa na hawa jamaa wa nyanda za juuu kusini hawana biashara za udhulumati na janja kama wenzao.

Wachagga zulumati na janja SANA.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kumbuka uarabu sio kabila ni kama uswahili tu...

Mimi ninachopinga hzo fikra za ukabila dhidi ya mafanikio ya kibiashara
unachosema ni sawa ila kwa hapa Tza uarabu ni jamiii anagalia jinsi wanavyotusua just kwa kuwa wao ni waarabu ....ukiingia ktk makampuni yao ndo utajua jinsi wanavyosaidiana kutusua
 
unachosema ni sawa ila kwa hapa Tza uarabu ni jamiii anagalia jinsi wanavyotusua just kwa kuwa wao ni waarabu ....ukiingia ktk makampuni yao ndo utajua jinsi wanavyosaidiana kutusua
Naam nandoma ni kasema kutusua ni ushirikiano na connection + uaminifu na kujituma...

Hao waarabu hivi vitu wanavyo na wanafundishwa tangu utotoni.

So ata mimi na wewe tukiwajenga hivi watoto wetu,mmoja akija fanikiwa ni sawa na wote kufanikisha.
 
ahsante kwa bandiko zuri hakika nimetoka na kitu hapa.
 
kuna jambo la kustukiza sana katika miaka ya hivi karibuni kuanzia 2010, kuna hawa jamaa wanaitwa wakinga wamejipatia umaarufu ndani ya miaka hii michache kwa spidi ya 4g

Ni kabila dogo sana ambalo halifiki hata watu laki 2 lakini ni moto wa kuotea mbali kwenye biashara kwakweli, siongei maneno matupu maana nayashuhudia kwa macho yangu.

Hata mchagga ambae aliiteka kariakoo leo hii kapinduliwa na hawa wakinga, leo hii ukienda pale kariakoo ni ya wakinga, kiukweli inastua.


Kwa mimi binafsi nikiwa chuoni, kuna mkinga flani alimaliza form 4 akaja kuanza certificate, nilioata kumjua, yule dogo hata hakumaliza certificate alianza kuuza mitumba ya nguo ila leo hii ana duka lake la simu hajafika hata miaka 25.

Kuna mwengine alipata ajira, analipwa vizuri tu kama 1.3 M take home na allowances kibao, ila alikaa kazini mwaka moja tu, aliacha hio kazi watu walimshangaa sana akafungua biashara yake, hatua aliyofikia kwa sasa inavutia kwa kweli,

Nafkiri kuna namna tunaweza jifunza kupitia hili kundi,

Kumekua na fununu za ndumba na uchawi ila kwa bidii nayoona waliyo nayo unaona kabisa the juice is worth the squeeze, kama unahisi ni ndumba basi na wewe karoge,!!
 
Umeandika uharo mtupu. Eti wasukuma ni kilimo,ufugaji na biashara kidogo. Wasukuma wamekamata biashara ya madini na wanapiga kitabu kama nini. Isitoshe wasukuma ni wasanii wa ngoma za jadi na wengi wametajirika. Usikariri huu ni wakati mwingine kila kabila sasa limeamka.
 
Hivi muha ana biashara kubwa ? Zaidi ya kuwa wachuuzi tu kwenye masoko
Kweli kabisa hata ukisoma Kozi ya ujasiriamali ngazi ya shahada wanakuambia biashara wakati mwingine inatokana na asili
Kidunia Wahindi ndio wanaongoza kwa biashara, kwa bongo ni wachaga, waha, wakinga
 
Hujafanya utafiti wa kutosha kasome tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…