Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

Aibu sn
 
Sawa toa msaada ila USITUNYANYASE ... Maana hata sisi tuna mioyo.. BLM ...
 
Uzalendo wa CCM ya sasa ni kuwabambikia kesi kesi kuwapiga risasi wapinzani kutafuna pesa za corona na kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu huo ndiyo Uzalendo wa CCM ya sasa
Hilo la uzalendo, ni kuwadanganya wananchi ili waendelee kutafuna nchi na kufanya wanavyotaka! Ni hawa hawa ccm ambao ni mafisadi wa kutupwa, leo hii eti ni wazalendo! Hivi watu wameshasahau kuhusu akaunti zao nje ya nchi na kwenye vile visiwa? Si ni hawa walisema pesa waliozoweka kwenye akaunti nje ile usd milioni moja kuwa ni “vijisenti” endapo za wengine nazo zingechunguzwa? Na nyingine kuitwa “pesa ya mboga” na mmojawapo wa hao mboga mboga!

Leo hii, hata mara baada ya uhuru, wao ndo wameamuwa kuwa wakoloni weusi huku wakilaumu hawa weupe kuwa ndo wanatuletea shida tusiweze kuondokana na umasikini na kuweza kujitegemea!

Mataifa mengine yametupiga bao, ambayo yalikuwa masikini kuliko sisi wakati tu napata uhuru mfano Malaysia na mengine mengi tu.
 
Sawa toa msaada ila USITUNYANYASE ... Maana hata sisi tuna mioyo.. BLM ...
Kwanini na wewe unanyasa watanzania wenzako? Kwanini unakiuka misingi ya ki demokrasia na utawala bora?

Tumia akili, ungana na watanzania wengine kudai katiba mpya ili na wewe uwe na sauti ya kweli kwenye mustakabali wa Taifa lako! Badala ya kusubiri na kumeza matango pori ya “mabeberu” ndiyo wameendelea kutufanya sisi ni masikini!

Hizo ni kelele tu na sababu za kijinga pale mtu anaposhindwa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…