Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Msingi wa mvutano wa serikali (ya CCM) na Wananchi kuhusu maandamano yao ya kuonyesha masikitiko kuhusu Utekaji, kupotea na mauaji na polisi kuhisiwa kuhusika ni kutaka wahusika wakuu wawajibishwe.
Yaani Waziri yule Mzanzibari Masauni na mkuu wa Polisi IGP Wambura.
Katika uwajibikaji, hata wao walipaswa wajiuzulu wenyewe lakini wamedinda hivyo mteuzi angewatengua mwenyewe ila hataki na anadharau kwa kusema "kifo ni kifo tuu" na kejeli zingine.
Hivi angetangaza kuwaweka pembeni uchunguzi ukiendelea kungekuwa na maandamano ya kesho?
Sasa kwa kumlinda Masauni na Wambura jee hawaoni kuwa kama busara haitakuwa kwa polisi maafa makubwa yaweza tokea?
Wanaweza kujeruhiwa waandamanaji au polisi na uharibifu wa mali sababu ya hao Masauni na Wambura!
Hii sio hao tuu, lakini hata Bi mkubwa anajiweka hatarini kuja kupelekwa The Hague siku zijazo na kula pension yake gerezani!
Jee kwa ajili ya hao wawili na wengine anataka aje (?!) kwenye debe na kuwa #1 wa kike duniani kukumbana na rungu la ICC wakati waliokuwa wanamshauri wako majumbani na familia zao wakila pension kwa furaha?