Kuwarejesha Lukuvi na Profesa Kabudi ni kuwakosea vijana

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wazee kama hawa akina Lukuvi na Kabudi wameshafanya kazi za kutukuka kwenye taifa letu. Walitakiwa wawe wameshazalisha vijana wenye uwezo, mawazo na maono kama wao. Lakini kama hawajazalisha vijana wengine mpaka Leo wanaoweza kuchukua nafasi zao sio sawa.

Hata Kama waliteuliwa walipaswa kusema "hapana inatosha". Hii ingenusuru ajira za vijana wetu, Kama vijana hawawezi kufanya kazi kama au zaidi ya wazee hawa watakuwa Wana kasoro kubwa za kimalezi, kielimu, kizalendo na kimaono.

Soma Pia: Ujio wa Lukuvi ( Bunge), Prof Kabudi ( Katiba) na Makonda ( Utawala Bora) kunaifanya CCM kukamilika Idara zote kuelekea 2025
 
nchi lazima isonge mbele,
na wenye uwezo na uadilifu wataendelea kuaminiwa na kupewa dhama za kusimamia kwa niaba ya umma huku nanyi vijana mkijipanga kushika hatamu katika wakati muafaka..

ni muhimu zaidi kujikusanya mahali sahihi ili iwe rahisi kuwapokea hao wazee wa busara watakapong"atuka 🐒
 
Ni upuuzi, kwani wakifa nchi nayo inakufa? Ni heri wawe nyumbani kuota jua huku wakifungua milango kwa viongozi vijana kupata ushauri wao na maoni. Uwezo wao wa kufikiri na kutenda imeishia hapo. Ni chanzo cha matatizo ya sasa ya nchi hivyo hawawezi kuwa chanzo cha utatuzi wa matatizo waliyouatengeneza wenyewe.
 
Wazee kama hawa akina Lukuvi na Kabudi wameshafanya kazi za kutukuka kwenye taifa letu. Walitakiwa wawe wameshazalisha vijana wenye uwezo, mawazo na maono kama wao. Lakini kama hawajazalisha vijana wengine mpaka Leo wanaoweza kuchukua nafasi zao sio sawa.

Hata Kama waliteuliwa walipaswa kusema "hapana inatosha". Hii ingenusuru ajira za vijana wetu, Kama vijana hawawezi kufanya kazi kama au zaidi ya wazee hawa watakuwa Wana kasoro kubwa za kimalezi, kielimu, kizalendo na kimaono.

Soma Pia: Ujio wa Lukuvi ( Bunge), Prof Kabudi ( Katiba) na Makonda ( Utawala Bora) kunaifanya CCM kukamilika Idara zote kuelekea 2025
vijana wana mambo mengi.tenda ilitakiwa kiongozi wa serikali anagalau umri uwe 40-50.kama mtu anasema CCM inaibaga kura ,wewe unategemea mzee wa miaka 50 angeropoka hivyo? vijana wana mihemko ya bangi,pombe, michepuko nk
si unaona hata suleiman alipotawazwa kuwa mfalme na huku nikijana,muda mwingi alishinda akiwatia mimba mabinti za watu na mwishoe akaenda kufukiza uvumbe kwenye madhabahu ya baali jambo ambalo baba yake hakufanya.

mfano mwengini ni yule msanii wa UKRAINE.nchi imesambaratika kwa sababu ya utoto wa akili zake na mwili wake

Mfalme Solomoni kadiri ya Biblia alikuwa mfalme wa tatu na wa mwisho wa Israeli nzima, akitawala kuanzia 970 KK hadi 930 KK hivi.

Maisha yake​

Solomoni katika ikulu yake (kadiri ya Ingobertus, 880 hivi).
Alikuwa mwana wa Daudi na Bath-Sheba (Betsheba), aliyewahi kuwa mke wa Uria Mhiti.

Daudi alimchagua kuwa mrithi wake kwa sababu alikuwa uthibitisho hai wa msamaha aliopewa na Mungu kwa kuzini na hatimaye kumuua Uria.

Ufalme wake ulitazamwa na Wayahudi kuwa na ustawi usio na mfano, kutokana na hekima yake na amani iliyopatikana wakati wote wa utawala wake.

Ufalme wake uliweza kustawi kuliko ule wa baba yake kutokana na msingi imara aliouweka Daudi. Lakini mwenyewe aliudhoofisha na kusababisha mara baada ya kifo chake utokee utengano kati ya makabila ya Kaskazini na yale ya Kusini.

Kati ya kazi muhimu alizozifanya, mojawapo ni kujenga hekalu la Yerusalemu na kuliweka wakfu kwa sherehe kubwa ya siku saba, ambapo Mungu alionyesha kibali chake kwa kulijaza kwa sura ya wingu (1Fal 8). Polepole hekalu hilo likaja kuwa la pekee hata patakatifu pengine pote pakakatazwa chini ya mfalme Yosia.

Ingawa Solomoni anasifiwa kwa hekima yake, alishindwa kukwepa majivuno na tamaa, akataka kuwapendeza wake zake waliokuwa 700 (mbali na masuria 300), wengi wao Wapagani, hata akawajengea mahali pa kuabudia miungu yao akamchukiza Mungu hata akamtabiria mtoto wake atanyang’anywa sehemu kubwa ya ufalme (1Fal 11:1-13) ikawa hivyo.

Hata hivyo mwishoni aliweza kulaumiwa kwa kuzidisha fahari, hasa upande wa wanawake waliomvuta kwenda kinyume cha imani ya Mungu pekee.

Alianza kutawala akiwa na umri wa miaka thelathini na miwili. Alitawala huko Yerusalemu miaka minane.
 
Ni upuuzi, kwani wakifa nchi nayo inakufa? Ni heri wawe nyumbani kuota jua huku wakifungua milango kwa viongozi vijana kupata ushauri wao na maoni. Uwezo wao wa kufikiri na kutenda imeishia hapo. Ni chanzo cha matatizo ya sasa ya nchi hivyo hawawezi kuwa chanzo cha utatuzi wa matatizo waliyouatengeneza wenyewe.
nadhani ni upuuzi zaidi kuwaza vifo na kueendekeza roho za mauti kwa walio hai.

infact huo ni ushirikina kwa waliofilisika hoja, kufikia ukomo wa mawazo mapya na fikra mbadala,

by,
the way majivuno, ukaidi, kiburi, ujuaji mwingi, mihemko na ubishi wa vijana kung'ang'ana kutumikishwa pasipo na uelekeo, patawachelewesha sana na mtalalama sana 🐒
 
Sasa kuwapata vijana wenye capacity ya Kabudi na Lukuvi ndani ya CCM ni ngumu, labda tuwatafute uraiani, au vyama kinzani🤔
 
Kwani hao 2 wamefanya nn kikubwa mno. Kabudi alipaswa kurudi chuoni akafundishe na kufanya tafiti. Kama amefundisha miaka yote hiyo lakini hakuzalisha vijana wazuri kama yeye unadhani anayo faida?
 
Vijana mnapewa mnaanza kutongozana na kushinda TikTok....mnapewa utamisemi mnaanza kufila mabint wa vyuo wengine mnapatanao AJALI wanakufa

Tulieni kwanza
 
Wape vijana nafasi wenye sifa za uongozi.Msiwabane.
Lakini kama wana mapungufu yenye kashfa za uhaini,ufisadi, wanafiki,wasaliti,maboya watupishe.
Nchi iandae vijana wengi na iwe inawashindanisha kupata zao bora.
 
Prof muoga hafai kuongoza Kata sembuse wizara? Anapaswa kuacha alama hata atakapoondoka kwenye uongozi watu waseme naaaam alikuwepo mtu hapa. Hebu fikiria ni usomi gani kuwa sehemu ya wanaopita bila kupingwa, wanaozuia vyama vingine visifanye siasa wakati katiba inawaruhusu? Kwanini usitumie uprofesa wako kuwaambia wenzako hiyo na hii hapana la sivyo najiuzulu?
 
Wazee kama hawa akina Lukuvi na Kabudi wameshafanya kazi za kutukuka kwenye taifa letu. Walitakiwa wawe wameshazalisha vijana wenye uwezo, mawazo na maono kama wao. Lakini kama hawajazalisha vijana wengine mpaka Leo wanaoweza kuchukua nafasi zao sio sawa.

Hata Kama waliteuliwa walipaswa kusema "hapana inatosha". Hii ingenusuru ajira za vijana wetu, Kama vijana hawawezi kufanya kazi kama au zaidi ya wazee hawa watakuwa Wana kasoro kubwa za kimalezi, kielimu, kizalendo na kimaono.

Soma Pia: Ujio wa Lukuvi ( Bunge), Prof Kabudi ( Katiba) na Makonda ( Utawala Bora) kunaifanya CCM kukamilika Idara zote kuelekea 2025
Vijana hawa wa betting?
 
Vijana mnapewa mnaanza kutongozana na kushinda TikTok....mnapewa utamisemi mnaanza kufila mabint wa vyuo wengine mnapatanao AJALI wanakufa

Tulieni kwanza
Kazi ya kuwaonya na kuwalingania hao viongozi vijana wasiofanya vizuri ndiyo ingekuwa kazi ya akina Lukuvi (mentoring) wakiwa majumbani kwao wamepunka na kufanya reflection ya walikotoka, walipo na tunakoelekea.
 
Sasa kuwapata vijana wenye capacity ya Kabudi na Lukuvi ndani ya CCM ni ngumu, labda tuwatafute uraiani, au vyama kinzani🤔
Kwahiyo unataka kusema baada ya Lukuvi na Kabudi CCM itakufa.
 
Wazee kama hawa akina Lukuvi na Kabudi wameshafanya kazi za kutukuka kwenye taifa letu. Walitakiwa wawe wameshazalisha vijana wenye uwezo, mawazo na maono kama wao. Lakini kama hawajazalisha vijana wengine mpaka Leo wanaoweza kuchukua nafasi zao sio sawa.

Hata Kama waliteuliwa walipaswa kusema "hapana inatosha". Hii ingenusuru ajira za vijana wetu, Kama vijana hawawezi kufanya kazi kama au zaidi ya wazee hawa watakuwa Wana kasoro kubwa za kimalezi, kielimu, kizalendo na kimaono.

Soma Pia: Ujio wa Lukuvi ( Bunge), Prof Kabudi ( Katiba) na Makonda ( Utawala Bora) kunaifanya CCM kukamilika Idara zote kuelekea 2025
Hawa ni watiifu kwa mamlaka ya uteuzi, Lukuvi huwezi kuona amevaa tshirt yenye picha ya mama au baba ake lakini anavaa tshirt yenye picha ya Samia, mzee kama huyu anajipya gani?
 
Kazi ya kuwaonya na kuwalingania hao viongozi vijana wasiofanya vizuri ndiyo ingekuwa kazi ya akina Lukuvi (mentoring) wakiwa majumbani kwao wamepunka na kufanya reflection ya walikotoka, walipo na tunakoelekea.
Yes
 
Back
Top Bottom