jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,556
- 25,342
Unataka kutuambia kuwa sheria nayo ni usanii?Mkuu CHIKIRA MTABARI jambo hilo la kumfikisha Mshtakiwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza mashtaka yake linaruhusiwa kisheria na kimahakama. Utaratibu huo, katika lugha ya kisheria, huitwa committal proceedings au preliminary inquiry. Hapo, Mshtakiwa hufikishwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kumsikiliza kwa lengo la kuiandaa kesi kwa kuipeleka mahakama mahususi na yenye uwezo wa kusikiliza kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Mfano, makosa ya mauwaji, uhujumu uchumi, ugaidi na utakatishaji fedha ni makosa ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu tu kwa mara ya kwanza (kabla ya rufaa kwenda Mahakama ya Rufani). Hatahivyo, washtakiwa waweza kupelekwa na kusomewa makosa yao Mahakama ya Hakimu Mkazi-kama Kinondoni, Ilala na Kisutu kwa ajili ya committal proceedings. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 246 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura Na.20 ya Sheria za Tanzania.
Lengo la committal proceedings ni kukamilisha upelelezi wa kesi husika; kuandaa ushahidi wa nyaraka na watu pamoja na mambo mengineyo ya kisheria. Yote yanapokamilika, jalada la kesi husika hupelekwa Mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi husika kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa. Kimsingi, pamoja na kuruhusiwa kisheria, committal proceedings ina changamoto zake. Mojawapo ni kutumika muda mrefu katika kupeleleza na kufanya mengineyo niliyoyataja.
Inasemwa kuwa, wakati mwingine, committal proceedings hufanywa kuwa njia ya kuwatesa washtakiwa kwa kuwaleta mahakamani na kuwarejesha rumande. Ingawa mahabusu hafanyi kazi kama alivyo mfungwa, ni vyema kukawa na uharaka wa kukamilisha committal proceedings ili kutenda haki kwa pande zote za shauri. Sheria inapaswa kutazama hasa upande dhaifu-upande wa Mshtakiwa.
Mahakama kunyimwa haki ya kuamua mustakabali wa mtuhumiwa kukaa rumande laki inapewa mamlaka ya kukazia kuwa mtuhumiwa akae rumande chini ya mlalamikaji katika mazingira katili yafananayo na adhabu akitendewa sawasawa na convict, ni sheria kukubali mahakama itumike kutesa watu wasio na hatia!
Kama ilivyo kwa katiba, hili nalo ni la kuliangalia.