Kuwarudisha Ndani Washitakiwa Kwa Madai Mahakama Haina Uwezo Wa Kusikiliza Kesi Hiyo, Ikoje?

Mkuu CHIKIRA MTABARI jambo hilo la kumfikisha Mshtakiwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza mashtaka yake linaruhusiwa kisheria na kimahakama. Utaratibu huo, katika lugha ya kisheria, huitwa committal proceedings au preliminary inquiry. Hapo, Mshtakiwa hufikishwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kumsikiliza kwa lengo la kuiandaa kesi kwa kuipeleka mahakama mahususi na yenye uwezo wa kusikiliza kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Mfano, makosa ya mauwaji, uhujumu uchumi, ugaidi na utakatishaji fedha ni makosa ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu tu kwa mara ya kwanza (kabla ya rufaa kwenda Mahakama ya Rufani). Hatahivyo, washtakiwa waweza kupelekwa na kusomewa makosa yao Mahakama ya Hakimu Mkazi-kama Kinondoni, Ilala na Kisutu kwa ajili ya committal proceedings. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 246 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura Na.20 ya Sheria za Tanzania.

Lengo la committal proceedings ni kukamilisha upelelezi wa kesi husika; kuandaa ushahidi wa nyaraka na watu pamoja na mambo mengineyo ya kisheria. Yote yanapokamilika, jalada la kesi husika hupelekwa Mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi husika kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa. Kimsingi, pamoja na kuruhusiwa kisheria, committal proceedings ina changamoto zake. Mojawapo ni kutumika muda mrefu katika kupeleleza na kufanya mengineyo niliyoyataja.

Inasemwa kuwa, wakati mwingine, committal proceedings hufanywa kuwa njia ya kuwatesa washtakiwa kwa kuwaleta mahakamani na kuwarejesha rumande. Ingawa mahabusu hafanyi kazi kama alivyo mfungwa, ni vyema kukawa na uharaka wa kukamilisha committal proceedings ili kutenda haki kwa pande zote za shauri. Sheria inapaswa kutazama hasa upande dhaifu-upande wa Mshtakiwa.
Unataka kutuambia kuwa sheria nayo ni usanii?
Mahakama kunyimwa haki ya kuamua mustakabali wa mtuhumiwa kukaa rumande laki inapewa mamlaka ya kukazia kuwa mtuhumiwa akae rumande chini ya mlalamikaji katika mazingira katili yafananayo na adhabu akitendewa sawasawa na convict, ni sheria kukubali mahakama itumike kutesa watu wasio na hatia!

Kama ilivyo kwa katiba, hili nalo ni la kuliangalia.
 
Pamoja sana Jembe, Ahsante kwa majibu yako..

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
Kama huwezi kuya challenge maelezo hayo kutokana na fani yako ya upishi usiwaaminishe wengine kuwa jamaa katoa bonge la point!
 
Urasimu

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu CHIKIRA MTABARI jambo hilo la kumfikisha Mshtakiwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza mashtaka yake linaruhusiwa kisheria na kimahakama. Utaratibu huo, katika lugha ya kisheria, huitwa committal proceedings au preliminary inquiry. Hapo, Mshtakiwa hufikishwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kumsikiliza kwa lengo la kuiandaa kesi kwa kuipeleka mahakama mahususi na yenye uwezo wa kusikiliza kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Mfano, makosa ya mauwaji, uhujumu uchumi, ugaidi na utakatishaji fedha ni makosa ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu tu kwa mara ya kwanza (kabla ya rufaa kwenda Mahakama ya Rufani). Hatahivyo, washtakiwa waweza kupelekwa na kusomewa makosa yao Mahakama ya Hakimu Mkazi-kama Kinondoni, Ilala na Kisutu kwa ajili ya committal proceedings. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 246 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura Na.20 ya Sheria za Tanzania.

Lengo la committal proceedings ni kukamilisha upelelezi wa kesi husika; kuandaa ushahidi wa nyaraka na watu pamoja na mambo mengineyo ya kisheria. Yote yanapokamilika, jalada la kesi husika hupelekwa Mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi husika kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa. Kimsingi, pamoja na kuruhusiwa kisheria, committal proceedings ina changamoto zake. Mojawapo ni kutumika muda mrefu katika kupeleleza na kufanya mengineyo niliyoyataja.

Inasemwa kuwa, wakati mwingine, committal proceedings hufanywa kuwa njia ya kuwatesa washtakiwa kwa kuwaleta mahakamani na kuwarejesha rumande. Ingawa mahabusu hafanyi kazi kama alivyo mfungwa, ni vyema kukawa na uharaka wa kukamilisha committal proceedings ili kutenda haki kwa pande zote za shauri. Sheria inapaswa kutazama hasa upande dhaifu-upande wa Mshtakiwa.
Mkuu ahsante kwa ufafanuzi ila nina swali kutoka kwenye maelezo yako.

Umesema kesi kama za ugaidi na utakatishaji pesa husikilizwa mahakama kuuu pekee, mbona ndama mtoto wa ng'ombe alisomewa mashitaka ya kutakatisha pesa mahakama ya kisutu na akakiri makosa akalipa fidia.

Kama hizo mahakama hazina uwezo wa kusikiliza na mtuhumiwa hatakiwi kujibu chochote ilikuaje kwa ndamà.
 
Kuna vitu watu wanashindwa kuelewa. Siyo kwamba DPP hajui kesi hiyo inaenda wapi ni anafahamu. Kuna baadhi ya makosa yanasikilizwa mahakama kuu. Ili ifike mahakama kuu lazima wafuate procedures kwanza kesi hizo zinafunguliwa mahakama ya chini yake. Mpaka pale upelelezi utakapo kamilika na mtu huyo amefanyiwa kitu kinaitwa "Commital", kesi hiyo ndipo itakapo hamishiwa mahakama kuu na kuanza kusikilizwa. Na ndio maana mtu atosemewa shtaka katika mahakama hiyo ya chini lakini ataambiwa asijibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza. Na kama kosa hilo halidhaminiki mtu huyo atarudishwa rumande. Ikumbukwe kuwa office ya DDP haifanyi upelelezi siyo kazi yake hiyo ni kazi ya Office ya DCI.
Umejibu vema Msomi!

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani sasa wabunge wetu Wana haja ya kupitisha sheria ya fidia kwa wale wote watao kuwa wakionekana hawana hatia,
 
Mkuu CHIKIRA MTABARI jambo hilo la kumfikisha Mshtakiwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza mashtaka yake linaruhusiwa kisheria na kimahakama. Utaratibu huo, katika lugha ya kisheria, huitwa committal proceedings au preliminary inquiry. Hapo, Mshtakiwa hufikishwa kwenye mahakama isiyo na uwezo wa kumsikiliza kwa lengo la kuiandaa kesi kwa kuipeleka mahakama mahususi na yenye uwezo wa kusikiliza kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Mfano, makosa ya mauwaji, uhujumu uchumi, ugaidi na utakatishaji fedha ni makosa ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu tu kwa mara ya kwanza (kabla ya rufaa kwenda Mahakama ya Rufani). Hatahivyo, washtakiwa waweza kupelekwa na kusomewa makosa yao Mahakama ya Hakimu Mkazi-kama Kinondoni, Ilala na Kisutu kwa ajili ya committal proceedings. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 246 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura Na.20 ya Sheria za Tanzania.

Lengo la committal proceedings ni kukamilisha upelelezi wa kesi husika; kuandaa ushahidi wa nyaraka na watu pamoja na mambo mengineyo ya kisheria. Yote yanapokamilika, jalada la kesi husika hupelekwa Mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi husika kwa ajili ya kusikilizwa na kuamuliwa. Kimsingi, pamoja na kuruhusiwa kisheria, committal proceedings ina changamoto zake. Mojawapo ni kutumika muda mrefu katika kupeleleza na kufanya mengineyo niliyoyataja.

Inasemwa kuwa, wakati mwingine, committal proceedings hufanywa kuwa njia ya kuwatesa washtakiwa kwa kuwaleta mahakamani na kuwarejesha rumande. Ingawa mahabusu hafanyi kazi kama alivyo mfungwa, ni vyema kukawa na uharaka wa kukamilisha committal proceedings ili kutenda haki kwa pande zote za shauri. Sheria inapaswa kutazama hasa upande dhaifu-upande wa Mshtakiwa.
Mkuu maelezo yako ni mazuri yamejibu maswali mengi, il mm nna swali: je, hizi procedures huwa zinatumika pia ktk mataifa yaliyoendelea? Au ni huku kwetu tu?

Sent from my SM-A700K using JamiiForums mobile app
 
....

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
 
Kama huwezi kuya challenge maelezo hayo kutokana na fani yako ya upishi usiwaaminishe wengine kuwa jamaa katoa bonge la point!
Nilichouliza nimepata jibu...so sioni haja ya kunitukana...mi cyo mpishi pili acha dharau hata huo ipishi ni fani kma fani zingine hvyo wape heshima zao, uzi nimeleta mimi kutaka kueleweshwa, kile Nilichouliza nimeeleweshwa ni jukumu lako wewe ku challenge pale palipo pinda ili watu waelimika cyo kutukana, nakuona huwa una misaada na majiby ya kiungwana sana humu jukwaani, hayo matusi ys kuwambia wenzko wapishi yanatoka wapi, plz tuheshimiane.

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
 
Kama huwezi kuya challenge maelezo hayo kutokana na fani yako ya upishi usiwaaminishe wengine kuwa jamaa katoa bonge la point!
Hlf cha ajabu ambcho hujakiona jamaa kajibu kulingana na sheria tulizo nazo wewe ulitaka ajiwekee sheria ajibu kitu ambcho hakipo kwenye katiba, sasa kma ulikuwa na majibu, hebu yaanike hpa chini niyaone, ndo utaonekana na wewe si mpishi..make hapa nimeuliza swali na ni ruksa mtu yeyote mwenye majibu kujibu, kma huna kma wewe ungepiga kimya tu, au unge prove alichokisema kuwa ni cha uongo kwa kutuletea vifungu vya sheria, hpo ntakuona wa maana na msomi.

"kulingana na sheria tulizonazo"

Huna ujasiri wa kutaja neno "sheria" maana unajua kuna ombwe kubwa mno!

Nipo kipande hiyo na wewe upo kipande inayokataza rais asishitakiwe nawe upo comfortable.
 
Kuna vitu watu wanashindwa kuelewa. Siyo kwamba DPP hajui kesi hiyo inaenda wapi ni anafahamu. Kuna baadhi ya makosa yanasikilizwa mahakama kuu. Ili ifike mahakama kuu lazima wafuate procedures kwanza kesi hizo zinafunguliwa mahakama ya chini yake. Mpaka pale upelelezi utakapo kamilika na mtu huyo amefanyiwa kitu kinaitwa "Commital", kesi hiyo ndipo itakapo hamishiwa mahakama kuu na kuanza kusikilizwa. Na ndio maana mtu atosemewa shtaka katika mahakama hiyo ya chini lakini ataambiwa asijibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza. Na kama kosa hilo halidhaminiki mtu huyo atarudishwa rumande. Ikumbukwe kuwa office ya DDP haifanyi upelelezi siyo kazi yake hiyo ni kazi ya Office ya DCI.

Mkuu naomba ufafanue kidogo. Kama upelelezi hauja kamilika, nini 'basis' au 'justification' ya mtu kukamatwa? Kwanini upelelezi usikamilike ndio akamatwe? Je, inamaana mtu akihisiwa tu anaweza kuwekwa ndani? Kama hamna "charge" mtu si ana uhuru wa kuondoka?
 
"kulingana na sheria tulizonazo"

Huna ujasiri wa kutaja neno "sheria" maana unajua kuna ombwe kubwa mno!

Nipo kipande hiyo na wewe upo kipande inayokataza rais asishitakiwe nawe upo comfortable.
Hujajibu kitu, jamaa kajibu nilichotaka kujua, sasa wewe Rais anaingiaje hpa sasa, fungua uzi wa aina hiyo. jikite kwenye hoja iliyopo mezani, ambyo nilitaka majibu yke mkuu.... ya mahakama kuwadeshi watu kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi fulani, kwa nini muda upotezwe kupelekwa kesi sehemu hizo wakati zinajua wazi kuwa haziwezi na kwa nini hizo kesi zisipelekwe sehemu husika, hiyo ndo ilikuwa hoja yngu, wewe ukaja na dharau zako za mambo ya upishi, mkuu heshimaa, kutukana tukana mtu ambye humjui cyooo..

Japo tupo kwenye tawi moja mtini, unachonikera ni kuzifurahia hizo sheria ambazo hatubishani kuwepo kwake.

Tumia elimu uliyonayo kuifanya akili yako nzuri ionekane kufanya kazi.

Usitumie elimu yako kuwathibitisgia walimwengu kuwa ulienda kusoma akili za wenzio huku wewe ukiwa na akili usizoweza kuziamini wala kuzitetea kisomi.
 
Hujajua na wala hujanisoma...siifurahii hii sheria kandamizi hata kidogo na SIUNGI MKONO, umenielewa isivyo ndo maana nikaleta huu uzi kupata mwanga na jamaa nimemuunga mkono kwa kunijibu kwa nini inakuwa hivyo kulingana ni sheria kandamizi zilizopo na hakwenda nje ya hpo...naona hujanisoma kikubwa nnachokitaka ni kubadilishwa kwa hii sheria ambyo inafanya watu wanakosa haki yao ya uhuru kwa kuendelea kusota ndani, thats all kma hunielewa hutanielewa tena.

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo upelelez kutokamilila ipo zaid kukomoa tu halafu hadi ifike hiyo hatua ya committal bas mtuhumiwa ameshasota vyakutosha mahabusu wengine inachukua hadi miaka 3-4 ndio kesi inaanza kusikilizwa au baada ya hapo inakuja acquittal proceedings na kuachiwa huru kwamba hana hatia wkt 4yrs amesota mahabusu hii si sahihi kabisa

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom