Kuwasha Mwenge kunaashiria "Illumination, enlightenment, and guidance." Mwenge wa Uhuru ni muhimu sana katika taifa letu

Kuwasha Mwenge kunaashiria "Illumination, enlightenment, and guidance." Mwenge wa Uhuru ni muhimu sana katika taifa letu

Kwamba padre akisema kitu ndio sahihi? Au unadhani kila mtu anaamini hayo madini ya wazungu?
Biblia mzee inasema. Wewe unasimamia maandiko yapi:
Soma Kutoka 25:31-40 Mungu alimwagiza Musa kutengeneza kinara cha taa cha dhahabu
 
Kwa jinsi ninavyojua Marekani hawana mlima mrefu kama wetu huu Kilimanjaro. Labda unaweza kunisaidia kujua kama wameshawahi kuweko huo mwenge wao Juu ya Mlima
Torch of freedom ya marekani ni sigara don't take it serious bro!
 
Biblia mzee inasema. Wewe unasimamia maandiko yapi:
Soma Kutoka 25:31-40 Mungu alimwagiza Musa kutengeneza kinara cha taa cha dhahabu
Biblia ni kitu gani boss, au kwakuwa ww unaiamini basi unadhani wotea tuanamini hicho kitabu chako. Kama unaamini biblia iamini kimpango wako na sio kila mtu.
 
Mungu ni Mungu, yeye ni nuru. Nipe mstari unaisema tuwashe mwenge
Mbona unazunguka Kutoka 13:21
Inaeleza Mungu waliwaongoza wana wa Israel kwa Nguzo ya Moto iliyokuwa ikiwapa Nuru. Je, unakubaliana na hili?
Kubali au ukatae. kisha tuendelee na majadiliano mengine.
 
Biblia ni kitu gani boss, au kwakuwa ww unaiamini basi unadhani wotea tuanamini hicho kitabu chako. Kama unaamini biblia iamini kimpango wako na sio kila mtu.
Tueleze ushirikina ni nini? Maana Biblia huitaki.
 
Kinachofanya kitu kiwe kizuri au kibaya ni maana iliyo nyuma ya tukio. Manuizi gani yalisemwa siku mwenge wa kwanza unawashwa? Je, ilikua ni ibada? Kama ni ibada ni nani anapewa hayo madhabahu ya mwenge? Ni Mungu aliyejuu? Ni upande wa giza unaojifanya ni upande wa Nuru?
Kitu kimoja, toka nizaliwe sijawahi upenda mwenge. Sijawahi kutoka kwenda kuushuhudia na wala sijawahi shawishika kwenda kuuona. Kwa nini sijui ila sina amani nao.
 
Mungu ni Mungu, yeye ni nuru. Nipe mstari unaisema tuwashe mwenge
Biblia utaijua ukiwa umezeeka mzee. Soma bibli ndugu:

Mwanzo 15:17-21​

Jua lilipokwisha tua na giza kuingia, tanuri ifukayo moshi na mwenge uwakao moto vikapita katikati ya vile vipande vya nyama. Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu akafanya agano na Abramu akisema, “Wazawa wako ninawapa nchi hii, toka mto wa Misri hadi ule mto mkubwa wa Eufrate, yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, Wahiti, Waperizi, Warefai, Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.
 
Sahihi kabisa, na hata kwa wakulima au hata kwenye mbuga zetu Kuna wakati nyasi na mbuga fupi fupi huchomwa kwa lengo la kuruhusu majani mapya na Bora zaidi kuota. Viva Tanzania
 
Ishara kumi na mbili za dunia zimeunganishwa katika makundi manne (Moto, Ardhi, Hewa na Maji)
Kwakuwa tunataka tuijue nchi yetu zaidi kwa leo sitaongelea kwa undani zaidi hizo ishara Kumi na Mbili na makundi yote hayo manne, bali leo nitaongelea pekee kuhusu Moto

Kuwasha mwenge kunaweza kuashiria mwanga, mwangaza wa kiroho, na uongozi

  • Kuleta Mwanga kwa Mambo ya Siri: Kuwasha mwenge kunaweza kumaanisha kuangaza mambo ambayo hayajulikani au kuleta uwazi katika hali fulani. Inaweza kuashiria kipindi ambacho ukweli uliokuwa umefichika au siri zinafichuliwa.

  • Uongozi na Hekima: Mwenge mara nyingi huonekana kama ishara ya hekima au maarifa ya kiroho. Unaweza kumaanisha kuwa na mwongozo wakati wa kipindi cha giza au kuchanganyikiwa, kama vile jukumu la mwalimu au kiongozi wa kiroho.

  • Mabadiliko na Mwanzo Mpya: Mioto, kwa asili yake, inahusishwa na kipengele cha moto, ambacho ni kipengele cha mabadiliko katika unajimu. Kuwasha mwenge kunaweza kumaanisha mwanzo wa hatua mpya, hasa ile inayohitaji kuachilia mambo ya zamani ili kutoa nafasi kwa mapya.

  • Kuamka Kiroho: Katika muktadha wa kiroho, kuwasha mwenge kunaweza kuashiria kuamka au kupanuka kwa ufahamu wa mtu. Ni kuhusu kuwa na ufahamu zaidi wa tabaka za ndani za maisha na nafsi.

Taifa lisilokuwa na Utamaduni na Mila zake hilo ni Taifa mfu.

Nitaendelea kueleza zaidi....
Halafu watu wakienda kwa Pdiddy mnaanza kupiga kelele kumbe hata nchi nayo ina Pdiddwa ila kwa style nyingine
 
Mungu ni Mungu, yeye ni nuru. Nipe mstari unaisema tuwashe mwenge
Soma Biblia ndugu yangu acha uzembe:
Kutoka 3:2
“Malaika wa Bwana akamtokea katika mwali wa moto kutoka katikati ya kijiti. Akaangalia, na tazama, lile kijiti lilikuwa linawaka moto, lakini halikuteketea.
 
Hebu soma
Isaya 50:11
Swali langu halijajibiwa. Kwanza umekubali kuwa Mungu waliwatangulia wana wa Israel akiwa amewasha nguzo ya moto ili kuwapa nuru?

Hata hivyo kinachoongelewa kwenye Isaya ni tofauti kabisa:- Unatakiwa kusoma kuanzia mstari wa 1 - 10 ndio ujue alikuwa anaongelea nini
1729072207894.png
 
Hebu soma
Isaya 50:11
Someni Biblia acheni uzembe.

“Mlima Sinai wote ulifunikwa kwa moshi, kwa sababu Bwana alishuka juu yake katika moto. Moshi wake ukapanda kama moshi wa tanuru, na mlima wote ukatetemeka sana.” (Kutoka 19:18).
 
Hebu soma
Isaya 50:11
Usome Biblia uache kukariri mzee.

“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta ya zeituni safi yaliyo pondwa kwa ajili ya mwanga, ili taa ziwekwe kila wakati. Aroni na wanawe wataziweka katika Hema la Kukutania… kwa mbele ya Bwana.” (Kutoka 27:20-21).
 
Huo mwenge tokea ulipowashwa miongo hiyooo hadi sasa mbona tunazidi kwenda nyuma tu badala ya kusonga mbele?

Ishara kumi na mbili za dunia zimeunganishwa katika makundi manne (Moto, Ardhi, Hewa na Maji)
Kwakuwa tunataka tuijue nchi yetu zaidi kwa leo sitaongelea kwa undani zaidi hizo ishara Kumi na Mbili na makundi yote hayo manne, bali leo nitaongelea pekee kuhusu Moto

Kuwasha mwenge kunaweza kuashiria mwanga, mwangaza wa kiroho, na uongozi

  • Kuleta Mwanga kwa Mambo ya Siri: Kuwasha mwenge kunaweza kumaanisha kuangaza mambo ambayo hayajulikani au kuleta uwazi katika hali fulani. Inaweza kuashiria kipindi ambacho ukweli uliokuwa umefichika au siri zinafichuliwa.

  • Uongozi na Hekima: Mwenge mara nyingi huonekana kama ishara ya hekima au maarifa ya kiroho. Unaweza kumaanisha kuwa na mwongozo wakati wa kipindi cha giza au kuchanganyikiwa, kama vile jukumu la mwalimu au kiongozi wa kiroho.

  • Mabadiliko na Mwanzo Mpya: Mioto, kwa asili yake, inahusishwa na kipengele cha moto, ambacho ni kipengele cha mabadiliko katika unajimu. Kuwasha mwenge kunaweza kumaanisha mwanzo wa hatua mpya, hasa ile inayohitaji kuachilia mambo ya zamani ili kutoa nafasi kwa mapya.

  • Kuamka Kiroho: Katika muktadha wa kiroho, kuwasha mwenge kunaweza kuashiria kuamka au kupanuka kwa ufahamu wa mtu. Ni kuhusu kuwa na ufahamu zaidi wa tabaka za ndani za maisha na nafsi.

Taifa lisilokuwa na Utamaduni na Mila zake hilo ni Taifa mfu.

Nitaendelea kueleza zaidi....
 
Huo mwenge tokea ulipowashwa miongo hiyooo hadi sasa mbona tunazidi kwenda nyuma tu badala ya kusonga mbele?
Wakati unawashwa Dar es salaam hakukuwa na BRT wana hatukuwa na SGR ya umeme.

1729072615252.png

1729072579295.png
 
Serikali haina mfungamano wowote wa kidini, na wala haijali. Amini kwamba.

Mwenge wa uhuru ni PR stunt ya mwalimu Nyerere(yawezekana kwa ushauri wa waingereza waliokuwa ikulu kipindi kile) kwa ajili ya kulipa uzito suala la uhuru, ili kufanya watu wajali, ukizingatia kipindi hicho watanganyika wengi hawakuwa na elimu.

Ingekuwa tukio la uhuru ni kusign tu makaratasi, huenda lisingechukuliwa kwa uzito wake.

Na pia mimi naweza sema ilikuwa ni njia ya kufikisha habari kwasababu mwenge ulibebwa toka Dar mpaka kilimanjaro, wapiga picha na watangazaji redio wakiwepo.
 
Back
Top Bottom