Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 2,971
- 9,437
Wakuu habari za jion? Waswahili walisema dunia hadaa ulimwengu shujaa, ndio hii sasa nakutana nayo mimi.
Nilikuwa muajiriwa wa kampuni (A) hivyo kampuni (B) walinitafuta sijui ni wapi walipata namba zangu.
Hr wa kampuni (B) alisistiza kuwa wanahitaji huduma yangu, na mimi pasina kusita nilienda kuwasikiliza, nilifanyiwa interview na mmoja wa viongozi wa kampuni hivyo nilipasi.
Maslai wakaniambia nikae na hr tuzungumze, basi tukaa na hr tukazungumza tukashindwana nikaondoka zangu, ikapita kama miezi miwili wakanitafuta tena, mara pili ofa aliyonipa hr haikukidhi, tukashindwa tena.
Mara ya tatu wakaniita tena, baada ya hr kuona hatuelewani kuusu maslahi akanipeleka moja kwa moja kwa boss wa kampuni.
Baada ya kukaa na boss akakubali kunilipa nilichokuwa nataka, haraka nikaiandika barua kampuni (A) kuvunja mkataba ndani ya saa 24, ulikuwa mvutano mkubwa, lakini nilifanikiwa kuachana nao.
Maisha yakaanza kampuni (B) nikakutanishwa na wafanyakazi wenzangu pale nikatambulishwa, majukumu ya kuitumikia kampuni yakaanza.
Ilikuwa nzuri sana miezi ya mwanzo, ushirikiano kazini ulikuwa wa hali ya juu, miezi mitatu ikapita, kuna wamba wanne wao ndio madoni wa kampuni, wamedumu kampuni kwa zaidi ya miaka nane, hivyo mzigo mrefu wanalipwa wao.
Kimbembe kinakuja pale walipokuja kugundua kuwa nawazidi mshahara, nyie , ghafla nilishangaa tu hawanisalimii tena, nikiwapa salamu kimya, nikajiuliza kimoyo kulikoni? Wana wananichunia tena?😀
Ushirikiano ukaanza kuwa hafifu baina yangu na wao, na mimi baada ya kugundua wana wamenichunia, nikajisemea kimoyo mtajua wenyewe, ikawa mimi na kazi home, mkataba wa kwanza ukaisha maboss wakaniita mezani, nikaongezwa 22% mshahara mkataba mpya.
Alooo hapa sasa ndio niliamsha makucha yao, ile chuki ndio ikaongezeka zaidi, wakuu nimeongea nao vizuri ile miezi ya mwanzo tu ila mpaka sasa nina miaka minne tunafanya kazi kampuni moja wana wameninuni 😀
Hii imenishangaza kuona watoto wa kiume wanamnunia kidume mwenzao, alafu watoto wa kike fresh tu tunashirikiana vizuri, stori vicheko vya hapa na pale ila wana wamununa.
Ikitokea nimetoa boko kidogo basi wataandamana hadi kwa boss, hii amefanya fulani. Basi chuki zao zimenifanya niongeze bidii zaidi na umakini wa hali ya juu. Kweli tembea uone.