Kuweka akiba ya fedha kumeongezeka umaarufu katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na sababu kama ongezeko la gharama za maisha, maendeleo ya huduma za kifedha, elimu ya fedha, upatikanaji wa habari na mengine.Hata hivyo, kwa mtazamo wa mazingira yetu, wengi wanaona kuweka akiba kuwa changamoto kutokana na hali duni ya kiuchumi. Wakati mwingine, inaonekana kuwa ni tabia inayowezekana kwa wenye vipato vikubwa pekee.
Swali ni: Je, kuweka akiba ya fedha ni uwezo wa kila mtu, au ni tabia inayoweza kupatikana hata kwa wenye kipato kidogo?
Ni hivi, uwekaji akiba una mizizi katika tamaduni za Kitanzania kupitia mazoea kama upatu na vikoba, ambapo wanachama huchangia fedha kwenye mfuko wa pamoja kwa manufaa ya baadaye.