Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Nilikuwa na mwanamke alinipost nilimfuata nikamkanya. Hajawahi nipost tena.
Kuna mwingine aliniumiza kihisia sana nikaamua kuachana nae. Kumbe kaumia sana akapost zile status za kujipa moyo ila unajua tu hapa kapata cha moto. Nililijua wala siku view niliona kwa mbali lile duara la status maneno fulani hivi be happy nk. Siku hiyo nimemuacha ndio nilitoa restriction ya kutoona status ili nujue atapost nini. Nilivoona kapost huo upuuzi nikaona case closed. Kumbe kaumia ukichek na me aliniumiza sana.
By the way siangalii status kabsa
 
Ni kama mimi naweza kukaa miezi 3 sijaingia FB ila wasap naingia daily, tatizo nna magroup kama matatu hivi ndo maana naingia mara kwa mara wasap ila FB aisee kwanza siipendi [emoji1787][emoji1787]
 
Kuna uhusiano na Maturity, tukiachana na wale ambao hawaweki kabisa ila hodari kuview - hawa nahisi wana aibu wanaona kuweka status kama labda ni utoto flani, pia insecurity( hawajiamini)

Ukiwa unaweka weka status mda wote na hazina cha maana ni utoto, kuna watu nilikuaga nawaheshimu mpaka niliposave namba zao aisee aibu niliona mimi πŸ˜‚πŸ˜‚.. maana huo msururu wa status za kila kinachojiri maishani kwake nilichoka hapo bado Hajaandika " niombeeni naumwa" mara mzee anaumwa anahitaji maombi yenu" daah
 
Sio anatumia gb watsup ana view lakini wewe huoni

Sasa wanahide nini wakionekana wameview? Social Media zimeongeza watu kuwa na matatizo ya afya ya akili....Mtu umemsave kwenye simu na yeye amekusave means ni mtu wako wa karibu au unamawasiliano nae sasa akiona umeview shida ni nini?
 
Hzo whatsap status ndio zimekuja kuondoa hamasa ya watu kujipost picha zao Facebook na Instagram, ndiomana saiv mtu anaweza kutaka namba yako tu ili aone unachopost
 
Ni njia nzuri ya kuweka mawazo na mtazamo wako kwa wote wanaokufahamu na wenye no yako.
 
Hivi Whatsapp Gb unaweza kuipakua huku ukiwa unatumia Whatsapp hii ya kawaida, au lazima Kwanza ufute hii officially
 
Hivi Whatsapp Gb unaweza kuipakua huku ukiwa unatumia Whatsapp hii ya kawaida, au lazima Kwanza ufute hii officially

Ukiwa na Duo Phone(Duble Duble line) unaweka fresh tu.

Mimi nina Whatsapp Meta ya Makizubegi na GBWhatsapp ya janikomu zipo kwenye simu moja duble line.
 
Ukiwa na Duo Phone(Duble Duble line) unaweka fresh tu.

Mimi nina Whatsapp Meta ya Makizubegi na GBWhatsapp ya janikomu zipo kwenye simu moja duble line.
ok, unafanyaje mkuu?, mjukuu wangu hayupo angeniwekea nione ya Dunia babu yake
 
ok, unafanyaje mkuu?, mjukuu wangu hayupo angeniwekea nione ya Dunia babu yake

Download GWhatsapp ,unaweza ukasearch Google to Latest GBwhatsapp apk ikija idownload then install kwenye simu ya double line ,ukishamaliza then unaingiza namba ya line nyingine kwenye gbwhatsapp,same procecess kama whatsapp OG ya meta.
 
Mimi mara nyingi naweka status za ujinga ujinga tu
Avatar yako inaonyesha wewe ni mtu wa aina gani haina haja ya kueleza unapost nini tuliosomea Cuba tunakua automatically..
 
Hivi wale wanaoweka quotes za biblia au quran wanaamini tunazisoma? Maana huwa nazipita kwa kasi ya 5g
 
Inategemea tuu na mazoea

Binafsi ni mtu niko private sana na maisha yangu, sasa profile picture tu sikumbuki hata mara ya mwisho kubadili ni lini.

Kupiga tu picha ni mtihani niliofeli kitambo mno.

Hizo status ndio kabisa kwanza nimemute status za watu wote kasoro za watu wa inner circle yangu tu.

Mazoea tu. Nikiweka picha basi najisikia tabu kama niko naked vile.
 
Avatar yako inaonyesha wewe ni mtu wa aina gani haina haja ya kueleza unapost nini tuliosomea Cuba tunakua automatically..
[/QUOTE]

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Sawa mtu wa maana
 
Ili mtu asijue kuwa nimeangalia status yake hii read receipts naiweka ON ama OFF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…