Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Status ni muhimu sana watu wengine hutumia kama fursa kujitangaza kibiashara ,kuelimishana ,kuburudish n.k ila mimi kea sasa siweki kila siku kama zamani na kitu ambacho sipendi kwenye status mtu kuwa na Kazi ya kujipost kila wakati na kupost wasanii tu .
 
wengine huweka kutangaza kazi zao. Sioni tatizo sana. ila shida ni wale wanajaza status hata mambo yasiyo na msingi.
akienda kunywa chai kaweka, kula kaweka, kunywa kaweka.

ila kuna kauuhusiano ka kuweka weka status na maturity.
kiasilia kuna baadhi ya watu nimeacha tu kuwa naangalia status zao coz najua hakuna la maana.
Pia me huwa mwekaji status kiasi kidogo mara nyingi niwapo free.
 
Mwezi mmoja au miwili iliyopita ndio nimejua status Nini, Nilikua najua ndio profile pic.

Na watsup nimeanza kuitumia tangu enzi hizo za Nokia E72(Symbian).
Mimi hata kuweka hizo status nilikua sijui na mwezi April ndio nilifundishwa kuweka. Hii kitu inataka mazoea nilijitahidi kuweka kwa kipindi kifupi vyenyewe haiko akilini mwangu mbona nlijikuta naacha [emoji1787]

Wako watu wanaweka status daily naweza sema hii ni addiction, wengine hadi wakikwaruzana wanaweka status aisee ni hatari
 
mtazamo wangu naona kuna watu wa aina mbili kwenye swala la kuweka na kutoweka status.
kuna wale nadhani wana insecurity issues kwamba hawataki kuonekana kama walivyo na aibu pia.
lakini pia kuna wale pia naona ni watu wa privacy tu hawataki watu wajue wanafanya nini au wapo wapi au wanafikiria nini.
nawasilisha
 
Usishangae ni mambo ya preference tu! Mama yeyoo wangu ni mtu wa kuangalia status kila muda kuna muda namwambia Oya hivi huchoki? Anasema anataka kusoma mood za watu kupitia status [emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…