heisicolly
New Member
- Jun 16, 2024
- 1
- 1
Mpaka hivi sasa watu wengi wanatumia vifaa mbalimbali vya sayansi na teknolojia katika kufanya shughuli zao.
Ukuaji wa sayansi na teknolojia umekuwa hivi sasa kulinganisha na miaka kadhaa iliyopita. Uwekezaji katika matumizi ya vifaa vya sayansi na teknolojia utaleta matokeo chanya kwani dunia ya sasa inamtaka kila mwanadamu awe na uelewa wa kutumia vifaa hivyo kurahisisha shughuli za kila siku.
Katika kuwekeza kwenye matumizi ya vifaa vya sayansi na teknolojia ni vyema kujikita kutoa mafunzo katika taasisi kama vyuo vikuu, vyuo vya kati, vyuo vya ufundi pamoja na shule za sekondari na msingi. Pia katika kuwekeza kwenye matumizi ya vifaa vya sayansi na teknolojia ni vyema kutoa semina ya mafunzo kwa wafanyakazi wote nchini kwa kuzingatia vitengo vyao na nafasi za kazi walizonazo.
Serikali itusaidie kupunguza gharama za matumizi ya mtandao (internet) ili kuwafanya wananchi wote waweze kumudu kutumia mtandao (internet) katika shughuli mbalimbali.
Napenda kuipongeza serikali yetu ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, pia nitoe pongezi kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, pia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye kwa kuhakikisha wanapambana katika kuboresha matumizi ya sayansi na teknolojia hapa nchini.
Mwisho nitoe pongezi kwa Jamii forums kwani imetupa nafasi kubwa ya kuwasilisha mawazo yetu katika kujenga nchi yetu ya Tanzania.

Upvote
3