Katika kuwekeza kuna mambo makuu mawili:-
Muda na Mtaji.., wengi huwa wanaangalia mtaji tu lakini muda nao una nafasi yake kubwa sana.., sasa kama na muda pia hauna hii inaweza ikaleta shida kidogo
Ila kwa bahati kubwa nchi zinazoendelea labor cost ni ndogo sana.., ila tatizo la kumweka mtu akufanyie biashara yenye mtaji mdogo (mfano kuuza maji / barafu / uji /matunda au kusambaza chakula) ni rahisi sana huyo mtu baada ya kufanya kwa muda mfupi akakugeuka na yeye akaanza kufanya kile kile kwa wateja wale wale ukizingatia mtaji wake ni mdogo.., unless otherwise ni ndugu au mke wako.
Pia kama muda unao unaweza ukaanza biashara kwa mali kauli, kama wewe ni muaminifu unakwenda kwa mwenye mali unamwambia akupe mali na ukishauza ndio utamlipa. Au kwa watu wenye knowledge fulani kama mwalimu n.k. wanaweza kutengeneza study materials na kuziuza bila kuwa na kianzio cha pesa.
Hivyo basi utaona kwamba issue kubwa hapo huenda isiwe una kiasi gani cha pesa bali ni shughuli gani unaweza kuifanya na kwa kuwekeza muda wako kiasi gani. (Ukizingatia biashara za Bongo ni za kuigana igana na za msimu kwahio inahitaji sana ku-manage muda wako na kuuwekeza vizuri)