Moaz
Member
- Apr 6, 2018
- 88
- 127
Kutokana na uongezeko la wasomi nchini imefika wakati sasa kungekuwa na mikataba kwa watumishi wa Serikali. Kuwepo kwa mikataba angalau ya miaka 2 baada ya mkataba kuisha kuwe na utaratibu wa kukagua utendaji kazi ambao kama ni wa kuridhisha katika kiwango ambacho kimeweka anaweza akaongeza mkataba mwingine huku akipanda ngazi na mwisho wa kuongeza mkataba katika eneo la kazi ni miaka 10 kwa maana kusiwe na Mtumishi akafanya kazi mahala kwa miaka zaidi ya 20.
Kwa watumishi ambao watakuwa hawajafika viwango stahiki hawataongezewa mikataba hivo kuweka nafasi wazi kwa ambao hawana ajira kuweza kupata kazi. Hii itasaidia kuongeza ufanisi na uwajibikaji makazini. Serikali itakuwa na kazi kubwa kusimamia uwajibikaji pasina kwa na presha kwa kuwa Mtumishi mzembe hatuweza kuongezewa mkataba.
Swala la watumishi kuwa na ukomo mpaka kustaafu kunatengeneza Watumishi ambao sio wawajibikaji ni muda sasa wa kuwa na mabadiliko kila baada ya miaka 2. Angalau kila Mwananchi aweze kuitumikia nchi. Nafikiri kama kutakuwa na utaratibu huu hakika itapunguza hili swala la kila Mwananchi kuamini katika kuajiriwa kwasababu ajira zitakosa huo ulinzi hivo kila mwananchi atakuwa na jukumu la kujitengenezea ustawi wake kwa kufikiria nje ya Box.
Watumishi watapunguza kuiba maana nchi yetu Watumishi wa serikalini ndio wanaongoza kuiba kuanzia juu mpaka chini kiasi imekuwa kama utaratibu wa kuwa Mwizi ndio kujiongeza. Kila mtumishi awe na miaka 2 akiiba hana ajira pamoja na taarifa ya wizi wake kiasi akisema aombe ajira sehemu nyingine hii sifa inakuwa sehemu ya CV yake kwamba alishawahi kuiba. Nafikiri hii inaweza kuleta mtazamo mpya nchini katika hii Karne ya 21. Ni muda sasa wa Kuivunja hii Security wanayoipata watumishi wa Serikali kwa kuwa ina hasara nyingi sana kuliko faida katika hii Karne ya 21.