Kuwepo kwa mikataba angalau ya miaka 2 kwa Watumishi wa Serikali, baada ya mkataba kuisha kuwe na utaratibu wa kukagua utendaji kazi

Kutokana na uongezeko la wasomi nchini imefika wakati sasa kungekuwa na mikataba kwa watumishi wa Serikali. Kuwepo kwa mikataba angalau ya miaka 2 baada ya mkataba kuisha kuwe na utaratibu wa kukagua utendaji kazi ambao kama ni wa kuridhisha katika kiwango ambacho kimeweka anaweza akaongeza mkataba mwingine huku akipanda ngazi na mwisho wa kuongeza mkataba katika eneo la kazi ni miaka 10 kwa maana kusiwe na Mtumishi akafanya kazi mahala kwa miaka zaidi ya 20.

Kwa watumishi ambao watakuwa hawajafika viwango stahiki hawataongezewa mikataba hivo kuweka nafasi wazi kwa ambao hawana ajira kuweza kupata kazi. Hii itasaidia kuongeza ufanisi na uwajibikaji makazini. Serikali itakuwa na kazi kubwa kusimamia uwajibikaji pasina kwa na presha kwa kuwa Mtumishi mzembe hatuweza kuongezewa mkataba.

Swala la watumishi kuwa na ukomo mpaka kustaafu kunatengeneza Watumishi ambao sio wawajibikaji ni muda sasa wa kuwa na mabadiliko kila baada ya miaka 2. Angalau kila Mwananchi aweze kuitumikia nchi. Nafikiri kama kutakuwa na utaratibu huu hakika itapunguza hili swala la kila Mwananchi kuamini katika kuajiriwa kwasababu ajira zitakosa huo ulinzi hivo kila mwananchi atakuwa na jukumu la kujitengenezea ustawi wake kwa kufikiria nje ya Box.

Watumishi watapunguza kuiba maana nchi yetu Watumishi wa serikalini ndio wanaongoza kuiba kuanzia juu mpaka chini kiasi imekuwa kama utaratibu wa kuwa Mwizi ndio kujiongeza. Kila mtumishi awe na miaka 2 akiiba hana ajira pamoja na taarifa ya wizi wake kiasi akisema aombe ajira sehemu nyingine hii sifa inakuwa sehemu ya CV yake kwamba alishawahi kuiba. Nafikiri hii inaweza kuleta mtazamo mpya nchini katika hii Karne ya 21. Ni muda sasa wa Kuivunja hii Security wanayoipata watumishi wa Serikali kwa kuwa ina hasara nyingi sana kuliko faida katika hii Karne ya 21.
Hiu ni kwa ajiri tu sie watumishi wa kawaida au hata central government???? eg presdaa,vice,pm n k???
 
Nani kakwambia ukisoma na usipoajiriwa huwezi kuitumia nchi?? Vipi mkulima na mfanyabiashara hawaitumikii nchi??
Yeah swali zuri ila wasomi wengi wanasoma ilinwaje wawe watumishi wa serikali ni Kweli Wakulima na wafanyabishara wanalitumikia Taifa lakn itakuwa sio sawa Taifa linatengeneza madaktari, walimu, wafu wa usalama je na wao wawe Wakulima na Wafanyabishara? Kama ndio hivo kuna haja gani ya kuzalisha hizi nafasi ambazo kwa ndio walalamishi wa swala la ukosefu wa ajira?
 
Utaratibu wa kupima utendaji wa watumishi upo. Zamani ulikua unaitwa OPRAS na sasa umekuwa digitalised unaitwa PEPMIS. Je, utaratibu huu una ufanisi kiasi gani, hilo ni swala lingine.

Tukumbuke pia, watumishi wengi wa serikali wanafanya kazi kwa mazoea na kubweteka sana. Wengi wanajali muda aliokaa kazini (saa nane kwa mujibu wa kanuni) bila kujali amefanya kazi kiasi gani au ameshinda anachezea simu na kupiga porojo.

Hii inasababishwa na mambo mengi lakini kubwa ni kukosa motivation. Mtu anaelipwa mshahara wa take home 300k ambayo inabidi ilipe kodi, isomeshe watoto, ilipe nauli, ilipe chakula, ilipe umeme, maji, vocha, iweke na akiba, inunue na soda etc, lazima mtu atafanya tu bare minimum.

Hivyo, kipimo cha weledi na uchapakazi wa watumishi kiendane na motisha husika. Kama mtakubali kuendelea kuwalipa kidogo, tutaendelea kuona kukosekana kwa tija kwa sababu ni nature ya binadamu kuact their wage.​
Shukran Kwa Elimu Mkuu. Hoja yangu ya Kuwa na mikataba ni kwa ajili ya kuufanya hata huo mfumo wa PERMIS uweze kuleta matokeo mazuri kama Mtumishi atakuwa na mkataba halafu matokeo kutoka PERMIS ndio yatamfanya aweze kupewa mkataba na kuongezewa mshahara na kupanda daraja kwa pamoja nafikiri ingeupa mfumo heshima hata kutokana na mshahara mdogo watumishi wangejituma kwa kuwa wanajua fika asipoperform vizuri mshahara hautopanda na atapoteza kazi. Tunajua Watumishi au waajiriwa ndio watu rahisi sana kuwacontrol ni kumfanya asiwe salama na kazi yake tu maana watumishi ni waoga kupoteza kazi zao.
 
Hilo jambo zuri ila hasara itakayopata serikali wananchi ndio mtaumia zaidi.
Ndani ya miaka 2 kijana atakuwa ashajenga ghorofa lake zuri in case mkataba ukibuma analigeuza hotel.
Wafanye waone moto.
Mishahara midogo hiyo pesa itumike kwenye kila jambo.
Serikali yenyewe imebariki ufisadi indirect
 
Akili uzitoe wapi ? Sema wewe ni jobless .
Mpeni DP WORLD awekeze kwenye suala la ukosefu wa ajira. Mbwa nyie hakuna mnachoweza Sasa hivi tofauti na kukandamiza watanzania wenzenu. Mbwa nyie Ma CCM
 
Hilo jambo zuri ila hasara itakayopata serikali wananchi ndio mtaumia zaidi.
Ndani ya miaka 2 kijana atakuwa ashajenga ghorofa lake zuri in case mkataba ukibuma analigeuza hotel.
Wafanye waone moto.
Mishahara midogo hiyo pesa itumike kwenye kila jambo.
Serikali yenyewe imebariki ufisadi indirect
Kwamba wataiba Sana hii nchi inatengeneza sana wezi kila sehemu inafikia hatua hatuamini kama tunaweza kuishi bila kuiba.
 
Kutokana na uongezeko la wasomi nchini imefika wakati sasa kungekuwa na mikataba kwa watumishi wa Serikali. Kuwepo kwa mikataba angalau ya miaka 2 baada ya mkataba kuisha kuwe na utaratibu wa kukagua utendaji kazi ambao kama ni wa kuridhisha katika kiwango ambacho kimeweka anaweza akaongeza mkataba mwingine huku akipanda ngazi na mwisho wa kuongeza mkataba katika eneo la kazi ni miaka 10 kwa maana kusiwe na Mtumishi akafanya kazi mahala kwa miaka zaidi ya 20.

Kwa watumishi ambao watakuwa hawajafika viwango stahiki hawataongezewa mikataba hivo kuweka nafasi wazi kwa ambao hawana ajira kuweza kupata kazi. Hii itasaidia kuongeza ufanisi na uwajibikaji makazini. Serikali itakuwa na kazi kubwa kusimamia uwajibikaji pasina kwa na presha kwa kuwa Mtumishi mzembe hatuweza kuongezewa mkataba.

Swala la watumishi kuwa na ukomo mpaka kustaafu kunatengeneza Watumishi ambao sio wawajibikaji ni muda sasa wa kuwa na mabadiliko kila baada ya miaka 2. Angalau kila Mwananchi aweze kuitumikia nchi. Nafikiri kama kutakuwa na utaratibu huu hakika itapunguza hili swala la kila Mwananchi kuamini katika kuajiriwa kwasababu ajira zitakosa huo ulinzi hivo kila mwananchi atakuwa na jukumu la kujitengenezea ustawi wake kwa kufikiria nje ya Box.

Watumishi watapunguza kuiba maana nchi yetu Watumishi wa serikalini ndio wanaongoza kuiba kuanzia juu mpaka chini kiasi imekuwa kama utaratibu wa kuwa Mwizi ndio kujiongeza. Kila mtumishi awe na miaka 2 akiiba hana ajira pamoja na taarifa ya wizi wake kiasi akisema aombe ajira sehemu nyingine hii sifa inakuwa sehemu ya CV yake kwamba alishawahi kuiba. Nafikiri hii inaweza kuleta mtazamo mpya nchini katika hii Karne ya 21. Ni muda sasa wa Kuivunja hii Security wanayoipata watumishi wa Serikali kwa kuwa ina hasara nyingi sana kuliko faida katika hii Karne ya 21.
Huo nao utakuwa mlango wa rushwa na majungu kwa wenye nafasi na uwezo wa kuzitumia kwa manufaa yao na genge lao.Na pia itakuwa dirisha la fitna na majungu sehemu za kazi.
 
Tujikite kutengeneza fursa mpya kwa kizazi chetu kinachoendelea kuongezeka lakini sio kunyang'anya wenye nazo!
Hayo mawazo ya kimaskini yalishajaribiwa kwenye UJAMAA matokeo yalikuwa hasi sana!
 
Serikali hawawezi kuchambua nyaraka kila baada ya miaka miwili...

Cc: Mahondaw
Wakague ili iweje nyieeeeee!
Acheni zenyuuuuu😁😁!

Ukiingia ukayatimba hapo umejitafutia shida mwenyewe mbali na hapoo aaaaaahhh burudani kabisa!!

Mbeleeeee kwa mbeleeee
 
Tujikite kutengeneza fursa mpya kwa kizazi chetu kinachoendelea kuongezeka lakini sio kunyang'anya wenye nazo!
Hayo mawazo ya kimaskini yalishajaribiwa kwenye UJAMAA matokeo yalikuwa hasi sana!
Lengo la hoja sio kunyanganya watu tukiogopa kufanya mabadiliko ni kivp tutaweza kutengeneza hizo fursa? Unafikiri kama kutakuwa na mikataba ndio matatizo yataisha hapana lengo ni kuongeza ufanisi na uwajibikaji. Swala la UJAMAA na UBEPARI ni shule tofauti kabisa mpaka sahv wengi tunaaminishwa ujamaa ulifeli lakini hatujawahi kuuliza je huo UBEPARI umefaulu wapi?
 
Huo nao utakuwa mlango wa rushwa na majungu kwa wenye nafasi na uwezo wa kuzitumia kwa manufaa yao na genge lao.Na pia itakuwa dirisha la fitna na majungu sehemu za kazi.
Mabadiliko yana changamoto zake kama faida itakayopatikana ni kubwa kuliko hizo sababu kwann tusijaribu.
 
Back
Top Bottom