Kuwepo utaratibu kuwalinda watoto viwanjani wakati wa mechi

Kuwepo utaratibu kuwalinda watoto viwanjani wakati wa mechi

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Mara kadhaa nimeshuhudia watoto wadogo walioambatana na wazazi au walezi wao uwanjani wakiwa katikati ya watu huku akiwa amezungukwa na ile midude wanayopuliza almaarufu kama vuvuzela.

Nilikuwa sijui kero ya haya madude mpaka wakati fulani Bwana mmoja alikuja nalo mahali nilipokuwa nafuatilia Mechi ya moja ya timu kubwa kwenye Bar, kila alipokuwa anapuliza ule mdude basi nilitamani kuondoka sehemu ile kwani lina mlio mkubwa sana unaoumiza.

Sasa jaribu kumfikiria Mtoto wa miaka mitatu, minne, mitano n.k kuwepo katikati ya hayo madude zaidi ya kumi yakipulizwa hovyo, anahimili vipi Mtoto huyu kama sio kumuumiza tu?

Walau basi kuwe na Jukwaa moja litakalotengwa ambako wataruhusiwa wale waliofuatana na Watoto ambako hakutakuwa kabisa na Mtu atakayerusiwa kuwa na Vuvuzela.
 
Back
Top Bottom