Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Hili jukumu nakuomba ulifanye wewe, mimi napita katika mapito yangu, kisha tutakuja kuulizana maswali, ili tuone nani mkweli katika hili.

Hakuna shida Boss, Cha Muhimu Reference tuwe tunaweka.
 
Hakuna shida Boss, Cha Muhimu Reference tuwe tunaweka.
Safi kabisa, mimi kama nilivyo tangulia katika utangulizi wangu hapo, ni kuwa haya ninayo andika au nitakayo yaandika siyo mapya bali nanukuu toka kwa wakubwa zangu, na mwisho nitaweka marejeo ya vitabu viwili ambavyo kwangu mimi nimeona vimenishibisha juu ya historia ya watu hawa.
 

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Hapo kuna Masuala mawili tayari yamejitokeza

1. "Nukuu toka kwa Wakubwa Zangu" hapa lazima watakua wanazuoni wa Ki-Islamu
2. " Mrejesho wa vitabu viwili ambavyo kwangu mimi nimeona vimeshibisha historia ya hao watu"....natarajia hivyo vitabu viwe Quran na Hadithi

Nway hilo suala nimekisia tu, nangojea hoja zako Boss.
 
Sahihi kabisa, kama ambavyo wewe umerejea katika Biblia, na mimi marejeo yangu ni huko huko, ila tutakuja kuachana katika kujibu maswali na kujenga hoja, sababu ukweli ni mmoja tu siku zote.
 
WAYAHUDI wanajinasibisha na NABII MUSA kwa Mantiki ya kwamba Wao ni Muendelezo wa Uzao wa Kabila la YUDA(Ref Biblia Kitabu Cha MWANZO 29:35),
Unaweza kunipa ushahidi ya kuwa uzao wa Yahuudha (Yuda) upo mpaka leo ? Ili kauli yako iwe na nguvu ya kuwa Uyahudi ni muendelezo wa uzao wa Yahuudha ?

Pili, je ni lini Uyahudi ulikuwepo au ulianza kuwepo, je kipindi cha Musa Uyahudi ulikuwepo ?
Na YUDA alikua ni Mmoja kati ya Watoto Kumi na Wawili wa Uzao wa YAKOBO(ISRAEL), Katika hao Watoto 12 wa YAKOBO mmoja wao Aliitwa LEVI( Ref Biblia kitabu cha MWANZO29:34)
Hili nakubaliana na wewe bila shaka yoyote.
Na Huyu AMRAM ndo Baba Mzazi wa NABII MUSA.....Kwahiyo Ukiangalia hii Family Lineage utaona WAYAHUDI na NABII MUSSA Ulikua Muendelezo wa Uzao wa YAKOBO( ISRAEL)
Nacho taka hapa unithibitishie ya kuwa kipindi cha Musa Uyahudi ilikuwepo, maana hii ni dini, na tunajua Musa hakuwa Myahudi kwa dini.
Hapa unawaongelea wana wa Israeli,yaani Kuamu ya Musa,na ai Wayahudi kama dini. Inabidi tuelewane uzuri hapa.
 
Safi kabisa, je kila myahudi ni wa ukoo wa Israeli ?

Je kuna sehemu yoyote inayo sema ya kuwa Musa alitumwa kwa Wayahudi au Musa alitumwa kwa Wana Wa Israeli ?
Bila shaka haya umeyatoa katika Biblia na si katika vitabu vya Wayahudi, sasa ni kipi kinachokujulisha haya yanawakusudia Wayahudi na si Wana wa Israeli ?
 

Hiyo aya haiwataji "Wana wa Israeli" aya inawataja "Mayahudi",Qur'aan haijawahi kujichanganya hata kidogo, mnaojichanganya ni nyinyi, anasema Allah aliye juu :


30. Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa! (at-Tawbah : 30)

Ukisoma katika Tafsiri "at Tankir" ya Ibn Ashuri au Tafsiri ya Ibn Kathiri utaona ya kuwa walio kuwa wanaongelewa hapo ni kikundi cha Mayahudi wanne walio enda kwa mtume ndiyo walikuwa wana dai ya kuwa Uzair ni mwana wa Mungu na kadhalika kikundi kingine cha Mayahudi wa al Isfahani walikuwa wana dai hilo. Mara nyingi aya katika Qur'aan zilikuwa zinashuka kwa sababu maalumu.
 
Sehemu ya pili

Hakika ni ngumu sana kuwazungumzia Wayahudi pasi na kumzungumzia nabii Yakub na ndiyo maana hili likawa vazi lao la kujipamba na kujinasibu na ukoo wake, hali ya kuwa ukweli ni kwamba wako mbali nao,kama tutakavyo lionyesha hili huko mbeleni.

Tunapo lizungumzia tamko "Israeli/Israili" basi huyo ni Yakub mtoto wa Is'haaq mtoto wa nabii Ibrahiim. Yakub aliishi Palestina, pale ambapo babu yake aliishi, lakini walikuwa wana hama hama katika maeneo tofauti tofauti ndani ya Palestina. Kwa jina hili la "Israeli" ndiyo linalo tumika kuwanasibu "Wana wa Israeli au Ukoo wa Israeli (Banu Israili).

Kupitia hili, sasa ndipo tunaanza kuielezea historia ya Uyahudi kutokea kwa nabii Yakub na mpaka walipoingia katika ardhi ya Misri.

Safari ya nabii Yakubu kuelekea Misri.
Nabii Yakub alianza safari hii akiwa na watu wake wa karibu pamoja na watoto wake kuelekea Misri baada ya wito wa mtoto wake kipenzi nabii Yusuf (Hapa kuna historia ndefu kiasi ya ilikuwaje nabii Yusuf akafika Misri, ila kwa ufupi alienda kule kama mtumwa lakini Mola akampa utukufu na kuaminiwa na mmoja wa viongozi na akaja kuwa kiongozi). Hili lilifanyika baada ya nabii Yusuf kumakinika huko Misri.

Wayahudi katika vitabu vyao wanasema ya kuwa, kipindi nabii Yakub anaingia katika ardhi ya Misri jumla yao walikuwa ni watu sabini na wote walikuwa ni waumini. Wakaishi humo maisha mazuri mno yenye kutajika, lakini baada ya kufariki nabii Yusuf, hali ikabidilika na kuanza kuishi kwa dhiki na mateso yasiyo na kifani chini ya utawala wa kifirauni.

Mateso haya yalikuwa yakifanywa na "Faraina/Firauni", hili ni jina maalumu kwa ajili ya Watawala wa Misri kwa wakati huo. Mateso kwa wana wa Israeli yalikuwa makali mpaka ikafikia hatua watoto wa kiume wanao zaliwa na wana wa Israeli wanauliwa na watoto wa kike wakiachwa hai, huu ni miongoni mwa ufisadi mkubwa sana kufanywa katika uso wa ardhi. Hali hii ya dhiki na mateso kwa wana wa Israeli ilienda kwa kitambo kirefu sana mpaka alipokuja nabii Musa. Nabii Musa akawa anawafundisha watu imani ya kweli na kuwausia juu ya subira (Hii ni baada ya Wana wa Israeli kuishi katika dhiki, ikawafanya wachupe mipaka na kuanza kumuasi Mola wao) na kuwakemea juu ya kuwaabudu watu na nafsi zao. Hali ya mateso kwa Wana wa Israeli ikaondoka na waka amriwa na nabii Musa kuondoka katika ardhi ile ya Musa, na hii ni desturi ya Mola wetu muumba katika kuwatakia kheri waja wake, huwa ana waamuru waondoke katika ardhi ambayo wanaishi kwa dhiki.

Lakini mafirauni wakaanza kupata majanga, matufani, dhiki na mabalaa na umwagaji wa damu ukakithiri lakini kwa haya yote Mafirauni hawakutanabahi kwayo basi wakawa wanaleta kiburi na kujiona,na Mola wetu mlezi akamfunulia nabii Musa ya kuwa awaamuru wana wa Israeli watoke katika ardhi ile.

Baada ya hapa, tutakuja kuangalia katika sehemu ya tatu, ilikuwaje safari yao ya wao kutoka Misri.

Itaendelea....
 
Tofauti na Mahindu na Mabudha hawa hawajinasibishi na mtume yeyote ila Mayahudi wanajinasibisha na nabii Musa hali ya kuwa hawana uhusiano wowote na nabii Musa,hili nitalithibitisha huko mbeleni panapo majaliwa.
Hapa tayari uongo hapo
 
Hapo nimekuelewa
 
Soma biblia kitabu cha Nabii Samweli hata kutoka pia
 
Ukweli ni upi kaka mkubwa.
Ukweli ni huu Wayahudi ni watoto wa kabila la Yuda. Yuda ni miongoni mwa watoto 12 za Mzee Yakobo jina lingine Israel. Musa ni Mtoto wa ukoo huo huo wa Israel ila yeye ametoka kabila Lawi. Lawi ni miongoni mwa watoto hao 12 pia. Sasa ukisema Wayahudi hawana uhusiano na Musa huoni hapo tayari ni uongo?
 
Uyahudi ni ukoo au ni dini ?

Je kuna kitabu chochote kabla ya Musa au kipindi cha Musa kimetaja jina la "Uyahudi"hata katika vitabu vyao wenyewe Mayahudi ?
 
Unaweza kutuwekea hapa hayo maandiko ili tusome wote.
Bila shaka kwa sio tuliosoma biblia mwanzo mwisho historia ya Adamu hadi Yesu. Huwa ipo wazi kabisa na maandiko yake yapo ndio maana nlikupa vitabu hivo uvisome kama mtafiti halafu ulete marejeo.

Na kama ni kukuandika humu mistari tutachoshana tu Soma vitabu vyote hivo utaelewa Chimbuko la Hilo kabilà
 
Uyahudi ni ukoo au ni dini ?

Je kuna kitabu chochote kabla ya Musa au kipindi cha Musa kimetaja jina la "Uyahudi"hata katika vitabu vyao wenyewe Mayahudi ?

Ukisema Uyahudi ni sawa useme Umasai au Uchagha Ila wayahudi ni kabila na ni ukoo wa Wayuda. 2.Ndio Vitabu vyote vya Musa vimetaja jina La kabila la Yuda.
 
Naona hujaelewa suala la mjadala likoje, mwenzako nimeona huko juu ana fata adabu za mjadala, anaweka na vifungu.
 
Ukisema Uyahudi ni sawa useme Umasai au Uchagha Ila wayahudi ni kabila na ni ukoo wa Wayuda. 2.Ndio Vitabu vyote vya Musa vimetaja jina La kabila la Yuda.
Tupe andiko linalosema Uyahudi ni kabila au ni mila fulani.

Siongelei jina la Yuda na ongelea tamko Uyahudi, sababu uyahudi unaingia katika sifa na si jina la mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…