Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
Jamiii forum tuwe tunaingia kwa interview sasa ukute kuna la saba wengi humu..... sasa hujui kuzaliana ni kwa ajili ya survival of the species .... rudi soma mtu anaitwa charles darwin......next time jamii forum muwe mnaomba vyeti vya member matunguli kama haya yanachafua jamii forum
 
Japo wanasemaga hakuna swali lakijinga lakini kwa hili nachelea kuamini ni swali la kijinga sana

Kama hakuna kuzaliana maana yake ni hakuna MAISHA
Yaani viumbe wa zamani kabisa wasinge zaliana maana yake kusingekuwa na kiumbe hai chochote duniani

Sasa kama unaona DUNIA hii na viumbe vyote tuliopo hatuna FAIDA yoyote kuwepo duniani basi hoja yako itakua na mashiko..

Kuna sababu kwanini sex is most pleasurable thing na ni jambo lenye msukumo mkubwa sana kwa viumbe hai wengi
 
Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
kuna siku nilijiuliza hili swali. mimi niliwaza kuhusu babu yangu aliyekuwa na watoto wengi kama 60 hivi na wajukuu wa kutosha
nikajiuliza babu alisahakufa, sasa watoto wake lukuki wanamfaa nini huko alipo
wenye uelewa watusaidie
ukisoma biblia utaona Mungu anamfariji Ibrahim ambaye alichelewa kuwa na mtoto, kwamba uzao wake utakuwa kama mchanga wa bahari, je hiyo kuwa wengi inamfaidia vipi mhusika
 
Jamiii forum tuwe tunaingia kwa interview sasa ukute kuna la saba wengi humu..... sasa hujui kuzaliana ni kwa ajili ya survival of the species .... rudi soma mtu anaitwa charles darwin......next time jamii forum muwe mnaomba vyeti vya member matunguli kama haya yanachafua jamii forum
mkuu nadhani hujaelewa vizuri swali lake,, kapitie tena upya.
 
Back
Top Bottom